Masikini CHADEMA- Kwishnei

Masikini CHADEMA- Kwishnei

sio swala la kupiga kura tu!
Kama unapenda siasa jitahidi kuelewa sio kukariri!kazi ya upinzani sio kuwasifu ccm !dhaifu ni pamoja na hoja za kingakinga kama hizi!
Nilijua unahoja ya maana kumbe ni udhaifu tu!sasa chadema kwishnei wapi
 
Nani kawapa leseni ya kufanya biashara?
Ni wajibu wa nani kukusanya kodi?

Kodi zenu indeed!
Nani kawapeleka bungeni?
Hizo kodi zenu wanazokula, wanaiba au wanapewa?

masopakyindi, ihurumie nchi yako na wahurumie Watanzania...yawezekana huna habari kuwa Chadema hawajawahi kukamata dola! Haijawahi kutokea popote duniani eti bajeti ya Upinzani ikajadiliwa bungeni, ni hapa Tanzania tu ambapo hata kwa akili ya kawaida, ujinga unaofanywa na Wabunge wa CCM unaweza kuvumilika na masopakyindi akashangilia...kweli, the country has gone to the dogs!

Mkuu wewe ni mmoja wapo wa wale tunaoita lopsided political commentator ambaye unayaona tu yale unayoyapenda na unayatolea maneno mazuri ya kuyapaka mafuta.
Lakini lile la msingi you remain to be mum, hata kama lina kugusa.
Unaingia katika mtego wa shallow thinkers kufikiri kwamba sympathy ya wananchi wote katika mustakabali wa nchi hii lies with CDM!
Far from it.

Nimesubiri suala la bajeti lipite , matokeo yake tuyaone na wewe na kundi lako muanze kufunguka kimawazo na kutambua kuwa YOU ARE ON THE LOSING SIDE!
Baada ya matokeo haya ya kupita bajeti ndio utaona kuwa yale maneno ya kifeduli, kijinga na mengine ya kukosa heshima kwa ujumla, were all in naught.
Na mbaya zaidi watu wenye akili kama wewe wala hamkunyanyua kalamu zenu kulaani yale ambayo kimsingi hayafanywi na watu waliostaarabika.

Turudi kwenye mada, sasa ule msimo wa wabunge wa CCM wewe unauita UJINGA! na mimi na shangilia.
LOOK at it from the other side, the CCM side.
Ule UJINGA uliofanywa na wabunge CDM na ngebe zote za kuitana dhaifu,zimezimwa!
Sasa hapo nani mjanja.

Mag3, the problem is you are in love with CDM, put your higher faculties to task.
 
Baada ya bajeti hii kupita kwa kishindo, CDM itakuwa imevunja rekodi ya kuwa Chama kinachosimamia mambo hewa yasiyokuwa kila kukicha, itabidi sasa wabadili jina!!! Napendekeza kiitwe CHAMA HEWA!!... bahati mbaya sana cdm kimeshindwa kukwepa hatima hii mbaya na mbovu..

Kuolewa kubaya sana! kila kitu cha mume wako inabidi ukisifie! mbaya zaidi bwana mwenyewe CCM! Huna umeme, Huna maji, Shule za kata zimekuwa guest house za kuzalisha mimba! Bado majitu majinga kama wewe yanajiona yana akili! MBUNGE WA CCM MMOJA NI SAWA NA WA CHADEMA 40!

Una roho ngumu mdogo wangu, lakini nafikiri kuna mambo ya msingi huwezi kuyatilia maanani kwa sababu huyajui kwani huyaoni na hata ukiyaona hutayatambua. Haya yote ni matokeo ya athari ya tume iliyoundwa tarehe 28 Januari, 1964 na kutoa ripoti yake tarehe 22 Machi, 1965. Tupo wengine wetu tuliokuwepo wakati huo ambao pamoja na nia nzuri ya Mwalimu ya kujenga taifa lenye umoja, tuliona athari ambazo hadi leo zinaendelea kuwatafuna Watanzania wenzetu kama wewe.

Mwalimu alipotaka kung'atuka mwaka 1975, hofu kubwa ilitanda nchini swali kubwa likiwa je, Tanzania bila Mwalimu inawezekana? Miaka kumi baadaye iliwezekana na Ali Hasan Mwinyi akawa Raisi wa pili Tanzania! Mwalimu huyo huyo kwa kutambua kwamba ili dunia iendelee kuwapo mabadiliko hayazuiliki, hakusita kuunga mkono upepo wa mageuzi. masopakyindi, kwa kipindi kirefu Watanzania walio wengi walikuwa wameathirika kiasi cha kutokuwa tayari kupokea mfumo nje ya ule waliouzoea.

Watawala wakatumia kikamilifu uoga wa ujinga wa wananchi walio wengi kuwaaminisha kuwa Tanzania bila CCM haiwezekani. CCM ndiye baba, ndiye mama na ndiye mlinzi wa amani na utulivu.
Kwa leo naacha hapa masopakyindi, ila ukae ukijua kuwa moto wa mabadiliko hauzimwi kwa ubabe, hauzimwi kwa ulaghai na hauzimwi kwa kubeza mwamko wa wananchi. CCM inaelekea kubaya na kadri siku zinavyosonga ndivyo hali inazidi kuwa mbaya...watanyanyasa na hata kuua lakini yote ni kama kumwaga petroli motoni!

Is that so!
Mkuu Mag3, unarudia kosa lile lile la watu wanaojaribu kudistort historia ya nchi hii ili ku achiieve their own narrow goals.
Achana na mambo ya 1963 hadi 1965, na 1975-hapo tutawapoteza wengi tu humu JF.
Usijidai kuwa ulikuwepo peke yako , tulikuwepo wengi tu!
Turudi hapa karibuni, 1991.
Ever heard of Tume ya Nyalali?
Tume ya Rais ya kukusanya maoni juu ya kuanzisha vyama vingi nchini?

Tume ya Nyalali ilibaini kuwa asilimia 80 ya maoni ya Watanzania yalionyesha wangependa kuendelea na mfumo wa chama kimoja, na asilimia 20 tu ndio waliotaka yafanyike mabadiliko ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, kwa kuzingatia ukuaji wa demokrasia duniani, pamoja na maoni ya wengi (80%) kutaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja, Tume ya Nyalali, kwa busara zake, ikapendekeza kwamba ni vema nchi yetu ibadilike na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Tume hiyo iliwasilisha Taarifa yake kwa Rais mnamo tarehe 17 Februari,15 ,1992 na kusababisha nchi kubadili rasmi mfumo wake wa siasa kutoka chama kimoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi mnamo tarehe 1 Julai, 1992.

Na ni baada ya hapo ndio kukazaliwa vyama kama NCCR, TADEA, CUF CHADEMA etc na utitiri mwingi tu!

Mbadailiko yote haya yalifanyika chini ya uangalizi wa kisiasa wa CCM na serikali yake.

Sasa leo, Mag3, unakuja na baseless allegations kuwa ati, I quote,
"Watawala wakatumia kikamilifu uoga wa ujinga wa wananchi walio wengi kuwaaminisha kuwa Tanzania bila CCM haiwezekani. CCM ndiye baba, ndiye mama na ndiye mlinzi wa amani na utulivu"

I am sorry , but such statements make me sick, more so when it comes from one whom I thought to be head and shoulders above small time petty thinkers.
 
Hiyo "K" kwenye jina lako inasadifu uliyoyaandika bz unawaza kwa kutumia masaburi
 
Kumbe ndio sababu. Kumbe hujaenda shule ndio maana mawazo yako ni duni kiasi hiki!!!!! Kweli CCM imetuangusha, miaka 50 ya uhuru bado adui ujinga anasumbua watu!!!! Afadhali umetujulisha hilo ili tusikulaumu bure. Watu kama wewe ndio mtaji wa CCM. Lakini wasomi na wajanja ni mwiba mkali kwa hao magamba. Pole sana ndugu yangu. Lakini zama za ujinga zinahesabika. Zitakoma siku Chadema itakapoingia madarakani.

Naomba kuuliza,hivi CDM wataingia lini madarakani?
 
Is that so!
Mkuu Mag3, unarudia kosa lile lile la watu wanaojaribu kudistort historia ya nchi hii ili ku achiieve their own narrow goals.
Achana na mambo ya 1963 hadi 1965, na 1975-hapo tutawapoteza wengi tu humu JF.
Usijidai kuwa ulikuwepo peke yako , tulikuwepo wengi tu!
Turudi hapa karibuni, 1991.
Ever heard of Tume ya Nyalali?
Tume ya Rais ya kukusanya maoni juu ya kuanzisha vyama vingi nchini?

Tume ya Nyalali ilibaini kuwa asilimia 80 ya maoni ya Watanzania yalionyesha wangependa kuendelea na mfumo wa chama kimoja, na asilimia 20 tu ndio waliotaka yafanyike mabadiliko ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, kwa kuzingatia ukuaji wa demokrasia duniani, pamoja na maoni ya wengi (80%) kutaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja, Tume ya Nyalali, kwa busara zake, ikapendekeza kwamba ni vema nchi yetu ibadilike na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Tume hiyo iliwasilisha Taarifa yake kwa Rais mnamo tarehe 17 Februari,15 ,1992 na kusababisha nchi kubadili rasmi mfumo wake wa siasa kutoka chama kimoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi mnamo tarehe 1 Julai, 1992.

Na ni baada ya hapo ndio kukazaliwa vyama kama NCCR, TADEA, CUF CHADEMA etc na utitiri mwingi tu!

Mbadailiko yote haya yalifanyika chini ya uangalizi wa kisiasa wa CCM na serikali yake.

Sasa leo, Mag3, unakuja na baseless allegations kuwa ati, I quote,
"Watawala wakatumia kikamilifu uoga wa ujinga wa wananchi walio wengi kuwaaminisha kuwa Tanzania bila CCM haiwezekani. CCM ndiye baba, ndiye mama na ndiye mlinzi wa amani na utulivu"

I am sorry , but such statements make me sick, more so when it comes from one whom I thought to be head and shoulders above small time petty thinkers.
masopakyindi, mbona hakuna hata kimoja nilichosema ambacho unakipinga? Unasema
Tume ya Nyalali ilibaini kuwa asilimia 80 ya maoni ya Watanzania yalionyesha wangependa kuendelea na mfumo wa chama kimoja, na asilimia 20 tu ndio waliotaka yafanyike mabadiliko ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
Na mimi nilisema hivi, kwa kipindi kirefu Watanzania walio wengi walikuwa wameathirika kiasi cha kutokuwa tayari kupokea mfumo nje ya ule waliouzoea. Je ndugu yangu kama ulikuwepo, unakumbuka nguvu nyingi iliyotumika kupinga mageuzi yasitokee Tanzania? Unakumbuka kampeni iliyofanywa na CCM kuwaomba, kuwaonya na kuwatisha wanancnhi kuhusu athari ya vyama vingi?

Kwa mara ya kwanza kabisa TV zikiwa zimeruhusiwa ja unakumbuka vipindi vya ITV na CTN kuhusu vurugu na mauaji ya Rwanda ili kuwaogopesha wananchi juu ya harati ya vyama vingi? masopakyindi unakumbuka ziara za Waziri Mkuu, John Cigwiyemisi Samweli Malecela chini kuwaonya, kuwatisha na kuwafananaisha wanamageuzi na sisimizi? Je, kulikuwepo na ulazima wa kuundwa kwa tume ya Nyalali kuwauliza wananchi kama wanataka uhuru zaidi? Unakumbuka kuwa kuna mwanamageuzi, Mabere Nyaucho Marando alimkatalia Mwinyi uteuzi wake kwenye tume na sababu alizotoa?

masopakyindi, unasema ninapotosha historia na kwamba ulikuwepo, naomba nikuulize swali, je Mwalimu asingewakemea viongozi na kusema kuzungumzia vyama vingi si dhambi, Mwinyi angeunda tume? Je unakumbuka juhudi za Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya ndani, Agostino Lyatonga Mrema, kupambana na wanamageuzi? Unakumbuka FFU ilivyotumika kuzima harakati za wanamageuzi na kuwapa vilema vya maisha wengine kwa kudai uhuru wa mawazo tu? Ndugu yangu unadai napotosha historia, jibu haya halafu tuendelee!
 
Baada ya bajeti hii kupita kwa kishindo, CDM itakuwa imevunja rekodi ya kuwa Chama kinachosimamia mambo hewa yasiyokuwa kila kukicha, itabidi sasa wabadili jina!!! Napendekeza kiitwe CHAMA HEWA!!... bahati mbaya sana cdm kimeshindwa kukwepa hatima hii mbaya na mbovu..

Karibu mirembe mkuu, nakupa ofa ya kuja kutibiwa akili hapa Mirembe Dodoma kwa gharama zangu, watanzania ni ndugu.
 
Kweli? Huwaga naamini eti ukiona dhiki imepindukia ujue neema i-karibu.Lakini hapa naona mambo na kazi bado sababu watu kama rafiki yangu mtoa mada hii sijaona hoja yake ya msingi ambayo amelenga kuitoa kwa umma bali ni kama mtu wa porojo anayetumika kama mpira wa kiume utumikavyo na unaishia jalalani,kitu cha mhimu ni kuangalia je,kama ccm wametumia wingi wao bungeni kupitisha bajeti isiyojali maisha halisi ya mtanzania huku ndo kuimarika zaidi kwa ccm na kufa kwa chadema,la hasha,huku ni kujichimbia kabuli jingine labda kwa kuona dhahiri kabuli la mwanzo walokuwa wanalichimba limefikia kwenye miamba hivo linaweza kuchelewa kukamilika sababu adhabu au zawadi ccm inazotoa kwa wanancho ndiyo kipimo hicho watakachoipimia na wao mda ukifika,kweli ukeleketwa wa chama ni suala moja lakini hutakiwi kuliruhusu likakufanya ushindwe kuyaona mambo kiuhalisia eti kila linaloibuka wewe unaangalia nani kalianzisha,wa chama gani na chama changu kinasemaje,huko ni kumwachia mtu awe anafikiria kwa maisha yako na uishi kama yeye anavofikiria badala ya wewe kucheza nafasi yako kikamilifu,naumiaga sana ninaposoma watu wanashambuliana wao kwa wao badala ya kugombanisha hoja zenye maana,mashiko na manufaa kwa umma"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA NA WATU WAKE"
 
masopakyindi, mbona hakuna hata kimoja nilichosema ambacho unakipinga? Unasema Na mimi nilisema hivi, kwa kipindi kirefu Watanzania walio wengi walikuwa wameathirika kiasi cha kutokuwa tayari kupokea mfumo nje ya ule waliouzoea. Je ndugu yangu kama ulikuwepo, unakumbuka nguvu nyingi iliyotumika kupinga mageuzi yasitokee Tanzania? Unakumbuka kampeni iliyofanywa na CCM kuwaomba, kuwaonya na kuwatisha wanancnhi kuhusu athari ya vyama vingi?

Kwa mara ya kwanza kabisa TV zikiwa zimeruhusiwa ja unakumbuka vipindi vya ITV na CTN kuhusu vurugu na mauaji ya Rwanda ili kuwaogopesha wananchi juu ya harati ya vyama vingi? masopakyindi unakumbuka ziara za Waziri Mkuu, John Cigwiyemisi Samweli Malecela chini kuwaonya, kuwatisha na kuwafananaisha wanamageuzi na sisimizi? Je, kulikuwepo na ulazima wa kuundwa kwa tume ya Nyalali kuwauliza wananchi kama wanataka uhuru zaidi? Unakumbuka kuwa kuna mwanamageuzi, Mabere Nyaucho Marando alimkatalia Mwinyi uteuzi wake kwenye tume na sababu alizotoa?

masopakyindi, unasema ninapotosha historia na kwamba ulikuwepo, naomba nikuulize swali, je Mwalimu asingewakemea viongozi na kusema kuzungumzia vyama vingi si dhambi, Mwinyi angeunda tume? Je unakumbuka juhudi za Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya ndani, Agostino Lyatonga Mrema, kupambana na wanamageuzi? Unakumbuka FFU ilivyotumika kuzima harakati za wanamageuzi na kuwapa vilema vya maisha wengine kwa kudai uhuru wa mawazo tu? Ndugu yangu unadai napotosha historia, jibu haya halafu tuendelee!

Mkuu Mag3, siasa is never static.
Kama ilivyo mawazo ya binadamu, siasa vile vile hubadilika kutokana na mazingira yanayowasibu wananchi wake.

Tusisahau kuwa mnamo 1961, baada ya TANU kushinda viti VYOTE,mwaka 1962 katiba ilibadilishwa ili nchi iwe ya chama kimoja.
Hayo yalikuwa matakwa ya wakati ule na hakulazimishwa mtu.

Hata 1991 , hata kama kuna watu waliopinga na umewatolea mifano, wisdom prevailed. Na hakuna mtu anajutia hilo, kwamba tumeingia mfumo wa vyama vingi-ndio matakwa ya mazingira ya sasa.
Pamoja na haya yote mawazo mbadal ya uongozi wa Taifa hili haukuanza na vyama , bali watu binafsi.
Nawakumbuka kina Mapalala,Mtikila na wengine ambao hata vizuizini walikwenda.

Kwa hiyo kama kuna viongozi-tena wazito, walilipinga hilo hizo zaweza kuwa sababu za kibinafsi zaidi kuliko matakwa ya umma.

Na naomba unielewe , tena vizuri sana.
Vyama vya upinzani vitaendelea kuwepo ingawaje kushinda uchaguzi na kuunda serikali hilo ni suala jingine.

Na si kwamba havijafanya vizuri, vimejitahidi but they are not good enough.
In actual fact CCM is gaining from theur existance.Baada ya CCM kupotoka na kuanza ku-court matajiri, ni vyama vya upinzani vimewaamsha na kuona hiyo fallacy!

Tatizo la vyama vya upinzani ni uchanga wao kimawazo, kiitikadi na viongozi wenye uzoefu na umahiri wa kujenga hoja za kimsingi.
Mara zote wapinzani wameona ni sifa kubwa KULAUMU TU bila kuwa na sera mbadala, sera ambazo hata leo hawana.
Kwa sasa hivi mimi binafsi sijaona chama chenye uwezo,umahiri, na hata utaalam wa kuendesha serikali, na wabakie kukosoa tu kwa afya yao.
 
Mkuu Mag3, siasa is never static...
Kama ilivyo mawazo ya binadamu, siasa vile vile hubadilika kutokana na mazingira yanayowasibu wananchi wake.
Kwa hiyo kama kuna viongozi-tena wazito, walilipinga hilo hizo zaweza kuwa sababu za kibinafsi zaidi kuliko matakwa ya umma...

Mara zote wapinzani wameona ni sifa kubwa KULAUMU TU bila kuwa na sera mbadala, sera ambazo hata leo hawana.
Kwa sasa hivi mimi binafsi sijaona chama chenye uwezo,umahiri, na hata utaalam wa kuendesha serikali, na wabakie kukosoa tu kwa afya yao.
Phew! I almost made the greatest mistake of my life. I almost thought you were for real masopakyindi kumbee... ni wale wale! Unaweza kusemaje kuwa, kama kuna viongozi-tena wazito, walilipinga hilo, hizo zaweza kuwa sababu za kibinafsi zaidi kuliko matakwa ya umma...! Wakati huo huo unasema asilimia 80% ya huo umma ulionyesha wangependa kuendelea na mfumo wa chama kimoja! Je unakumbuka tamko rasmi la CCM kuhusu mageuzi kabla hawajakemewa na Mwalimu? Vyoyote vile utakavyodai, ukweli ni kuwa CCM ililazimika kupokea mageuzi shingo upande na si kwa mapenzi yake, waliyaogopa na wanaendelea kuyaogopa hadi leo.

Vipengele vyote vilivyopendekezwa na tume ya Nyalali kuwa vilikuwa vina ulazima wa kufanyiwa kazi kabla ya mfumo rasmi wa vyama vingi kupitishwa vilikataliwa na serikali ya CCM, kwa nini? Misingi ya kuhakikisha kuna haki na usawa katika kuendesha siasa ya vingi haikuridhiwa na serikali ya CCM, kwa nini? Huwezi kuzaa mtoto ukamnyima lishe bora na bado ukategemea mtoto awe na afya nzuri! Lakini daima usisahau matunda ya mateso anayopata na hatari itakayokukabili kama huyo mtoto pamoja na taabu zote hizo ata"prevail" , usishangae akikukana!

Kazi ya vyama vya upinzani duniani kote ni kukosoa na kama upinzani unainyima CCM usingizi kwa hili, basi upinzani unatimiza wajibu wake ipasavyo. Hivi unaelewa sera ni nini? Sera ni maneno tu na bila matendo sera haina maana yoyote, sera ya upinzani itaonekana wakishika madaraka. Hii inanikumbusha watu wanaotaka kutoana macho eti kwa bajeti mbadala uliotolewa na Mh. Zitto halafu watu wenye mawazo kama yako eti wakaanza kuijadili na kuikosoa! masopakyindi, huu ndio ulimbukeni at its best, unaikosoa au kuijadili ili iweje? Matokeo yake...fisadi Ngeleja kutuzwa bungeni!
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuuliza,hivi CDM wataingia lini madarakani?
Wataingia madarakani siku watanzania walio wengi watakapowapitia kura za ndiyo. Hii ina maana kwamba ni lazima watanzania walio wengi wawe wameelimishwa na kuelewa umuhimu wa mabadiliko ya kisiasa kwa ajili ya maendeleo yao.
 
Back
Top Bottom