Mashujaa day: Live on TBC1

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
867
Maadhimisho ya siku ya mashujaa, Yamemalizika Mnazi mmoja, Jk BWM naviongozi wengi wastaafu wamehudhuria. Hii ina maana gani kwa Tanzania ya Leo.?
 
Maadhimisho ya siku ya mashujaa, Yamemalizika Mnazi mmoja, Jk BWM naviongozi wengi wastaafu wamehudhuria. Hii ina maana gani kwa Tanzania ya Leo.?
Tutaendelea kukosa umeme kwasababu wanatarajiwa watoe maamuzi "wanasherehekea" siku ya mashujaa
 
Sikukuu zingine zimebaki kuwa Sikutuuu! Yani si kitu mbele ya uhalisia wa maisha ya leo. Watanzania wamebanwa na maisha kiasi moyo wa uzalendo unapotea na kupotea... Ngoja siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru utakubaliana nami. Watoto wa shule na mamluki wa magambaz na wanasiasa ndo watajaza uwanja.
 
Mtangazaji alipomtaja Waitara kama Mkuu wa majeshi, ni ulimi uliteleza au alikuwa anamaanisha Mkuu wa majeshi mstaafu?
 
Mtangazaji alipomtaja Waitara kama Mkuu wa majeshi, ni ulimi uliteleza au alikuwa anamaanisha Mkuu wa majeshi mstaafu?

Yalikuwa marudio ya siku ya mashujaa 2007. Kesho tarehe 25/07 ndio siku ya mashujaa. Kitu ambacho sikuelewa ni kwanini TBC1 wameona ni vema kuonesha marudio ya maadhimisho ya sikua ya mashujaa 2007 na sio 2008 au 2009, au 2010 au hata 2000? why 2007?
 
nawapongeza mashujaa wote wa nchi hii ambao walijitoa na wanajitoa kuilinda nchi hii
 
Mtangazaji alipomtaja Waitara kama Mkuu wa majeshi, ni ulimi uliteleza au alikuwa anamaanisha Mkuu wa majeshi mstaafu?
WOS....Salama?Nadhani mleta thread aliona tukio TBC1 then akakurupuka kuileta thread hapa jamvini....Yale yalikuwa ni marudio ya mojawapo ya maadhimisho ya miaka ya nyuma wakati Jenerali(rtd) Waitara akiwa CDF...Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa kwa mwaka 2011 yanafanyika kesho(tarehe 25/07/2011) katika viwanja vya Naliendele Mtwara
 
Ingependeza sana km hiyo siku tuivurushe hii serikali fisadi ya CCM madarakani tukawa huru!!!
 
WOS....Salama?Nadhani mleta thread aliona tukio TBC1 then akakurupuka kuileta thread hapa jamvini....Yale yalikuwa ni marudio ya mojawapo ya maadhimisho ya miaka ya nyuma wakati Jenerali(rtd) Waitara akiwa CDF...Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa kwa mwaka 2011 yanafanyika kesho(tarehe 25/07/2011) katika viwanja vya Naliendele Mtwara

Salama sana Bala!!
Nilikuta tangazo liko katikati hivyo nikashindwa kuelewa ni nini kinaendelea.Niliposikia Mkuu wa majeshi wa zamani anatajwa ..nikashangaa iweje mtangazaji asijue Mkuu wa sasa ni Mwamunyange!

Asante kunishtua kuwa ni marudio ya maadhimisho yaliyopita.
 
Mtangazaji alipomtaja Waitara kama Mkuu wa majeshi, ni ulimi uliteleza au alikuwa anamaanisha Mkuu wa majeshi mstaafu?
point of correction kesho ndio siku ya mashujaa na kitaifa itafanyka Naliendele Mtwara hyo iliyoonyesha leo ni ya miaka ilyopta ndio maana hata mkuu wa majeshi ulisikia ni Waitara na meya kuwa ni A.KIMBISA.
 
Kuwaenzi mashujaa kwa matendo ndo suala la msingi wazalendo wa kweli walioifia nchi yao!
 
Apology great thinkers.! This year heros' day is tommorow at mtwara. The Tv broadcast was a repetition.! Sorry for any incoveniences.!
 
By the way, je tunahitaji kweli kusherekea sikukuu ya mashujaa wakati hatuenzi kitu ambacho mashujaa wetu walifia? Akina mkwawa, mirambo, na wengineo walipigana vita kwa ajili ya uhuru wa kweli.

Walikufa ili tuwe huru kisiasa na kiuchumi.

Je tuko huru kisiasa na kiuchumi?
 
Am lost jamani .Hili nalo ni kitu gani ? Naomba ufafanuzi .Kwa nini 2007 na si siku za nyuma siku chache baada ya kupata uhuru ?
 
Nyie siku ya Mashujaa ni trh 25 July ya kila mwaka, safari hii shughuri itafanyika Mtwara, hyo ya mnazi mmoja ilikuwa ya 2007..
 
Back
Top Bottom