Leo ninawaenzi mashujaa wote waliopigania uhuru wa nchi yetu na wale wanaoendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
Mashujaa si wale tu walioandika historia, bali pia ni wazazi wanaolea watoto kwa kujituma, vijana wanaopambana kutimiza ndoto zao, na wananchi wanaojitolea kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.
Tukumbuke kuwa kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa shujaa kwa matendo yake, uadilifu wake na mchango wake kwa taifa.
Heri ya Siku ya Mashujaa kwa Wakenya wote!