Mashtaka 85 kwa kigogo wa TANESCO

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mashtaka 85 kwa kigogo wa Tanesco
Tuesday, 01 February 2011 21:27

ATUHUMIWA KUIBA, KUHUJUMU UCHUMI
Tausi Ally
MHASIBU wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Lilian Chengula (42) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 85 ya wizi wa zaidi ya Sh1.3 bilioni na uhujumu uchumi.Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mustapha Siyani, Wakili wa Serikali, Zuber Mkakatu alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 84 ya wizi wakati akiwa mtumishi wa umma.

Pia Chengula anakabiliwa na shtaka moja la uhujumu uchumi kwa kuisababishia mamlaka iliyowekwa kisheria, hasara ya zaidi ya Sh1.3 bilioni. Chengula alirejeshwa rumande hadi kesho Februari 3, mwaka huu, wakati Hakimu Siyani atakapotoa uamuzi iwapo apewe dhamana au la.

Mawakili wa Lilian, John Lawrance na Matongo waliiomba mahakama impatie dhamana mteja wao kwa sababu makosa yote yanayomkabili yanadhaminika.

Ombi hilo lilipingwa na wakili wa Serikali, Mkakatu aliyedai mahakamani hapo kuwa shtaka la 85 la uhujumu uchumi linalomkabili Chegula haliwezi kupatiwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kwamba wenye uwezo wa kutoa dhamana kwa kosa hilo ni Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Matongo aliiomba mahakama itupilie mbali hoja iliyotolewa na upande wa mashtaka kwa madai kuwa imepitwa na wakati, hivyo hakimu Siyani kuahirisha kesi hiyo hadi kesho.

Mapema wakili wa Serikali alidai kuwa mshtakiwa Chengula alifanya makosa hayo kati ya mwezi Septemba, mwaka 2009 na mwezi Septemba, mwaka 2010.

Mkakatu alidai kuwa Chengula ambaye ni mwajiriwa wa Tanesco akiwa mhasibu kwa nia ya kudanganya, alighushi hati mbalimbali za malipo na kujipatia fedha hizo ambazo ni mali ya mwajiri wake.

Katika shtaka la uhujumu uchumi, Chengula anadaiwa kulisababishia Tanesco hasara ya Sh 1,312,717,717.70.

Baada ya Wakili wa Serikali kusoma shtaka la uhujumu uchumi, hakimu Siyani aliuhoji upande wa mashtaka kama una kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kinachowaruhusu kufanya hivyo.

Wakili huyo wa Serikali alisema upelelezi wa makosa 84 ya wizi yanayomkabili Chengula bado haujakamilika na kwamba bado wanasubiri kibali kutoka kwa DPP kinachohusiana na kosa la 85 la uhujumu uchumi.

Kukamatwa kwake………

Habari za kukamatwa kwa Chengula ziliandikwa na gazeti hili katika toleo lake la Jumatatu wiki hii, huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando, akithibitisha kukamatwa kwa mhasibu huyo.

Mhando alisema ofisa huyo anatuhumiwa kutenda makosa kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali waliokuwa wakinunua umeme katika ofisi hizo.

“Ni kweli huyo mtu tunaye na anatuhumiwa kushirikiana na ma-vendor wetu (wauzaji wa rejareja). Inaonekana alikuwa akiwauzia umeme mwingi kuliko umeme aliotakiwa kuutoa kulingana na gharama walizolipia,” alisema Mhando.
Alisema suala hilo lilibainika baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa ndani ambao uliwezesha kugundulika upotevu wa kiasi hicho kikubwa cha pesa na kwamba baada ya kubaini tatizo hilo hatua zilizochukuliwa ni kumhamishia afisa huyo makao makuu ili kupisha uchunguzi.
“Kwa kawaida huwezi kumfukuza tu mtu kazi kienyeji, kwa hiyo kwanza “tulim-charge” tukamtaka aandike maelezo ni kwa nini asifukuzwe kazi ,” alisema Mhando.
Alisema baada ya timu iliyoundwa kushughulikia suala hiyo kukaa na kupitia maelezo yake ilibainika kuwa ofisa huyo ana hatia na kwamba hatua iliyokuliwa ni kukatisha mkataba wale wa ajira.
“Lakini kwa kuwa hizo ni pesa nyingi na ni za umma tukaona ku-terminate (kukatisha) tu mkataba wake haitoshi hivyo wakaguzi wakaamua kumfikisha polisi kwa hatua zaidi za kisheria;“Kwa hiyo baada tu ya kukatisha mkataba wake na askari wakamkamata hapo hapo ofisini,” alisema Mhando.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa vyanzo hivyo ofisa huyo alitiwa mbaroni Ijumaa iliyopita akiwa ofisini kwake makao makuu ya Tanesco ambako alihamishiwa wakati uchunguzi wa tuhuma zake ukiendelea .“Mpaka ninavyokwambia hivi sasa yuko Central (Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam), kilidokeza chanzo chetu na kuongeza kuwa huenda leo ofisa huyo akapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo zinazomkabili,".
Habari zaidi zilidai kuwa polisi wanaendelea kuwasaka washirika wa Chengula katika tuhuma hizo ili nao waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Wizi kupitia mashine za Luku
Septemba 7, mwaka jana
Tanesco lilitanga kubaini kuwepo kwa mtandao wa wezi wa umeme kupitia mashine za Luku na vituo feki vya kuuzia umeme huo.

Kufuatia hali hiyo, shirika hilo lilianzisha operesheni endelevu ya kuwasaka wahusika wakiwemo watumishi wake wanaohisiwa kuhusika.

Katika siku ya kwanza ya utekelezaji wa operesheni mashine 7 kati 11 za Luku ambazo awali zilibainika kuwa na tatizo, zilihakikiwa katika maeneo ya Mwenge na Kariakoo zilihusishwa na wizi wa umeme.

Msemaji wa Tanesco, Badra Masoud alisema kupitia kitengo maalumu cha Luku kilichoanzishwa na shirika hilo walikuwa wakifuatilia taarifa za kuwepo kwa hujuma katika shirika hilo kupitia Luku na mita za kawaida, zinayofanywa na baadhi ya wafanyakazi halali wa shirika hilo.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites


Last Updated on Tuesday, 01 February 2011 21:34 Comments

12



0 #20 Fredrique 2011-02-02 17:44 Nawapa pongezi jeshi la Polisi< wakaguzi na uongozi wa TANESCO kwa mafanikio hayo. mmeonyesha kufahamu na kuzingatia maadili ya kazi kwa makosa ya mama huyu.
Nina mashaka kama suala hili mmelifanya kwa kujikosha. kiukweli ni kwamba hamna nia ya dhati kuwakomboa watanzania na kero za ubadhilifu zinazotukabili. Kwanini hua mnakua wepesi kuwashughulikia wabadhilifu wadogo huku wale wakubwa mkiwaacha wakitamba? Mbona mnatengeneza matabaka katika jamii ya watnzania? nin tofauti ya huyo mama na Mawaziri wa zamani (Basil Mramba na Daniel Yona)? Tena hao vigogo wamechota mabillioni ya VIJISENT lakini hawafanywi kit. Mbona mnatunyanyasa watu wa daraja la kati na chini?

Quote









0 #19 Grace 2011-02-02 17:01 Kama tunataka haki, kabla ya mama Chengula kushtakiwa na kukamatwa nadhani waliosaini mikataba ya RICHMOND na DOWANS wenyewe wako hapo hapo makao makuu na wengine wamepewa uwaziri na vyeo vingine... Je wao ni lini watashtakiwa maana kuilipa DOWANS hakuepukiki (ni majibu ya watawala) kwa hiyo tayari walishatuingiza mkenge na tunajua wala si siri tena. WAkamatwe na waanzie mahakama ya mwanzo ili siku zao za kukaa ndani kabla ya kuruhusiwa kupewa dhamana wawe ndani tu. Pa kuanzia ni Igunga hapo nitasema kweli tunajali HAKI. Kama si hivyo Chengula anaonewa tu maana hayo majambazi mbona yameachwa tu.
Quote









0 #18 jackson 2011-02-02 16:36 uyu mama katika billion 94 za rostam ndio kashaanza kujichukulia za kwake big up mama yangu walio lala usiwaamshe
Quote









0 #17 jackson chengula 2011-02-02 16:29 kama kweli sheria inazinga[NENO BAYA] nchi hii anzeni na mh. kikwete ndie ashtakiwe kwa kufuga na kuruhusu mikataba feki ata mimi ningekuwa huyu mama ningejichotea mahana bila kufanya hivyo atuwezi hii ni monopoly the imperialist world so get wat u can ila usiue lakini yote tuna muachia mungu angalieni misri na tunisia na amini ipo siku tanzania ita kuwa ya wanyonge ipo siku itarudi kwa wanyonge amini nakwambia
Quote









0 #16 Embu 2011-02-02 15:40 Tanesco ilimpata Dr wa Ufisadi (Idrisa)na ndio kukazaliwa Rchmond na Dowans, sasa wanafunzi wake wanaonyesha wamefaulu somo!
Quote









0 #15 koko master 2011-02-02 15:29 wezi wa ukweli mnawaogopa... huyu mama mnamuonea tu! anajaribu kuwafungua macho na nastahili pongezi!mama hongera kazi nzuri maana kila siku wao tu??? Idris yuko wapi? hembu nyie shirika la ugavi wa giza fanyeni kazi tupate mwangaza sie!
mwacheni huyo mama akalee familia yake.

Quote









0 #14 isaya masaki 2011-02-02 14:35 mi sioni haja ya huyo mama kukamatwa kamateni kwanza akina rostam aziz waizi wakubwa.
Quote









0 #13 isaya masaki 2011-02-02 14:32 mi coni haja ya hu7yo mama kuwekwa ndani yakamatwe kwanza mapapa halafu dagaa washulikiwe bwana kiongozi.
Quote









+3 #12 Mpoki 2011-02-02 14:31 Tanesco should also sue Management of Dowans, Richmond and all staffs who participate in making those null and void contracts of these 'handbag companies'
Quote









+1 #11 BENSON 2011-02-02 14:24 HAWA NDIYO WANAOTUFANYA TUICHUKIE TANESCO. WANATAFUNA PESA ZA SHIRIKA, MATOKEO YAKE SHIRIKA LINAPATA HASARA, UMEME UNAONGEZWA BEI, WANANCHI WANALIA. HAWA WATAKUWA WAPO WENGI TU. MTU MMOJA TU BILIONI 1.3 !! DU! FAIDA YA MWAKA MZIMA NA ZAIDI KALA YEYE TU? JAMANI TUMUOGOPE MUNGU JAMANI. HIVI MTU KAMA HUYU HASIKII UCHUNGU KUWASABABISHIA WATU MASIKINI WA NCHI HII KUINGIA GHARAMA ZISIZO NA TIJA KWA KUITIA HASARA TANESCO KIASI HICHO?
Quote









+1 #10 nelson kaserwa 2011-02-02 13:18 najua huu ni mkakati wa kukusanya bil94,huyu mama ahukumiwe kwa mujibu wa sheria na kufilisiwa mali zake zoote kwani kumuweka jela miaka mi3 atatumikia tu ila akitoka tutamkoma..wengine pia wahukumiwe hasa wa epa wote wanaojulikana waliorudisha hela wote ni wezi wafilisiwe na dowansi pia.tuache siasa hapa
Quote









-1 #9 mjenzi 2011-02-02 13:01 This has been the order of the day in our country where public service is synonymous with theft, greedy, and grand corruption.
Ms Chengula is just a small "fish" in the "sea" of corruption. I wonder why that "huge net" of Tanzanian justice with those "big holes" does catch small fishes only. This is inconceivable!! What about those big "fishes" in Dowans, EPA, and many others. We urge the authorities to act fairly by bringing all the suspects to trial! Vinginevyo huu ni usanii unaoendelea katika nchi ya kisanii. Hili la Chengula lisitufumbe macho tukasahau Dowans!!!!!!!!

Quote









0 #8 nick 2011-02-02 12:53 hongera mama wwe kabilioni 1.3 wanakufikisha mahakamani wakati wao wanalazimisha malipo yacyo halali ya bilioni 94 na bado wapo uraiani, imeandikwa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.
Quote









0 #7 raphae 2011-02-02 12:26 Kazi nzuri sana Mamaaaaaaaaaaaa a!Sehemu ambayo kuna uozo sioni ajabu kwa huyo mama kufanya alichofanya!hap o TANESCO pananuka rushwa ya kila aina. Hakuna dira ya nishati Tanzania,Mbona hao wanaoitwa wamiliki wa dowans hawaambiwi wahujumu uchumi.
Quote









+1 #6 Naigwa 2011-02-02 11:46 kukata umeme kila wakati bila hata kuwajulisha wananchi siyo uhujumu uchumi? hasara kiasi gani tanesco mmeshaisababish a kwa wananchi! mbona nyie hamjajipeleka police! na huyu mama kweli ni yeye pekee aliyeiba! nani alikuwa anasign vibali kuruhusu mauzo ya umeme? haiwezekani kabisa kuwa yeye ndiye kila kitu! tunasubiri kusikia wengi zaidi wanaingia kwenye kesi hii.tatizo lenu ni kulindana. kwanini mnashinikiza asipewe dhamana! mnaogopa kwamba wengi mtaumbuka! uongozi wa tanesco, hongereni, lakini wananchi tunahitaji kuona mnawapeleka mahakamani pia wale viongozi wenu walioshiriki kusign dowans. siyo muishie hapa!!
Quote







12
 
Kumrundikia mtuhumiwa mashitaka zaidi ya 15 kwa kesi moja ni kumvunjia haki zake za binadamu.......................zipo kesi nyingi ambazo watuhumiwa walikuja kufutiwa mashitaka kwa sababu ya utitiri wa Hati ya Mashitaka..................................

Hii siyo mbinu ya kumwokoa mtuhumiwa ili ije isemekane alishitakiwa kupita kiasi na hivyo kumnyima haki yake ya asili ya kujitetea?
 
Kigogo aliyeiibia TANESCO kizimbani


na Happiness Katabazi


amka2.gif
MHASIBU wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Lilian Chengula, amepandishwa kizimbani mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kuiba fedha za shirika hilo sh bilioni 1.3.
Aidha mshtakiwa huyo alisomewa mashitaka 85 jana mbele ya hakimu Mustapha Siani na moja kati ya mashitaka hayo likiwa la uhujumu uchumi na yaliyobaki ya wizi.
Chengula alidaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2009 hadi Septemba 2010 katika ofisi za shirika hilo wilaya ya Kinondoni, akitumia wadhifa alionao.
Ilidaiwa na waendesha mashitaka, Zuberi mkakati, Inspekta wa polisi Ema Mkonyi na Beatrice Mpangala waliosoma mashitaka hayo kwa kupokezana kuwa Chengula alikuwa akiliibia shirika hilo kwa kutumia vocha alizokuwa akiziwakilisha kwa nyakati tofauti.
Katika shitaka la uhujumu uchumi, mshitakiwa alidaiwa kusababisha hasara kwa mamlaka iliyowekwa kisheria ambayo ni mwajiri wake Tanmesco Sh 1,312,717,717.70 kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.
Mshitakiwa alikana mashitaka yote isipokuwa la uhujumu uchumi ambalo mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza isipokuwa kwa kibali toka kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP), mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina kibali cha kusikiliza kesi hiyo.
Mahakama hiyo itatoa maamuzi juu ya dhamana ya mshitakiwa kesho baada ya mwendesha mashitaka kuiomba mahakama isimpe dhamana kwa madai kuwa haina uwezo wa kusikiliza moja ya mashitaka yanayomkabili na ipuuze maombi ya mshitakiwa ya kutaka apewe dhamana.
 
PHP:
Kigogo aliyeiibia TANESCO kizimbani

Hiki kichwa cha habari kinawalakini................................huyu jamaa bado ni mtuhumiwa tu na kamwe kwa hatua iliyofikiwa hajawa mwizi na kubambikwa jina la ....................aliyeiibia Tanesco............................
 
wanamuonee tu mama watu kama angekuwa ameiba si tungemuona angenunua shangingi lakini ndio kwanza ana kavits ka mkopo wamembambika tu huyu mama wa watu waibe wao wabamike wengine pole mama yetu
 
Back
Top Bottom