Mashirika yanayolipana Mishahara Minono kwa mwezi

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Mishahara ya wakuu wa taasisi zifuatazo ni zaidi ya kufuru..... Hapa ndipo panga la Rais Magufuli linashuka kwa ukali wote

NHC..... 36M
EWURA..... 36M
NSSF......... 36M
TANESCO.... 36M
BOT............. 24M

Asante Rais Magufuli. Tumenyonywa vya kutosha!
1459400237768.jpg
 
Mishahara ya wakuu wa taasisi zifuatazo ni zaidi ya kufuru..... Hapa ndipo panga la Rais Magufuli linashuka kwa ukali wote

NHC..... 36M
EWURA..... 36M
NSSF......... 36M
TANESCO.... 36M
BOT............. 24M

Asante Rais Magufuli. Tumenyonywa vya kutosha!

Mimi sio CCM hata Katika ndoto, lakini Kwa Hili Nampigia Makofi sana Mh Magufuli, Namuunga Mikono yangu yote! Haiwezekani Mkuu wa NSSF, alipwe mara 1000 zaidi ya Mwalimu, Je ana Akili mara 1000 zaidi ya Mwalimu wa Sekondari, Je Mchango wake kwa Taifa, ni Mara 1000 zaidi ya Mwalimu wa Sekondari? au Nesi? au Polisi\? au Askari wa Jeshi? Hapana hii ni Kufuru! Hizi ni tabia chafu za Magharibi Unakuta CEO ambaye Kazi nyingi kama sio zote zinafanywa na walio chini yake, Lakini yeye anazoa $ 25,000,000 kwa Mwaka wakati Wanaotoa Jasho wanyonywa Jasho na Damu, Na inawabidi wafanye Kazi mbili au tatu Kumudu Maisha. Hii ni Dhambi. Niseme Tena Asante Rais Punguza Pia Mshahara wako Zaidi ya Nusu! Pamoja na Wakuu wa Mikoa na Mawaziri, Ili wajue sio ulaji Kuwa Kiongozi Ila ni Utumishi Kwa Umma. Labda hii itasaidia Kuondoa Wanasiasa "Mafisi"
 
Ni jambo la kawaida kuweka ukomo kwenye mishahara kwa taasisi za umma...pia lazima ziwajibike kupeleka ziada serikalini kufadhili bajeti.Marekani na ulaya walitunga sheria ili kudhibiti malipo makubwa ya mishahara,bonasi na marupurupu..na walijifunza kutokana na mdororo wa kiuchumi 2007/08 kwani ruzuku iliyotolewa nyingi ililipia malimbikizo ya mishahara na marurupu...na ndio maana waliacha baadhi ya benki zianguke tu,"wage bill ilikuwa kubwa".
 
Duh...ni noma...
Ila Mheshimiwa Rais amekata hii mishahara kwa maneno makali sana...
Kuna baadhi yao walipigiwa magoti kurudi Tz kushika hizo nafasi...
Ni kweli hii mishahara haiingii akilini...lakini tusifanye waonekane kama majambazi
Sio kweli..... Watanzania wapo wenye uwezo mkubwa sana tena wanaofanya kazi nchini kwa uaminifu mkubwa sana...
 
Rais=36M
PM= 26M
VP = 32M
Mawaziri=16M
Makatibu wakuu=15M
Hapo vipi?

Wakati huohuo Rais, PM na VP wakistaafu wanakula 80% ya mshahara wa rais, VP na PM wa wakati huo (ambao unapanda kila siku) hadi anaingia kaburini wakiti CEO wa kampuni akistaafu ndo basi: Hivi hao viongozi e. g VP ana kazi gani nchini ama ni kutoa tu matamko na kuhudhuria hafla?
 
Sheria za kazi zinasemaje Bora awaachishe wote ateue wengine maana wapo wengi wenye vigezo kuliko kuja baadae kupelekana mahakamani tuje kuwalipa tena Mimi ccm siiamini kabisa maana hàwa viongozi ni makada Wa chama kwenda mahakamani kitu cha kawaida
 
Mishahara ya wakuu wa taasisi zifuatazo ni zaidi ya kufuru..... Hapa ndipo panga la Rais Magufuli linashuka kwa ukali wote

NHC..... 36M
EWURA..... 36M
NSSF......... 36M
TANESCO.... 36M
BOT............. 24M

Asante Rais Magufuli. Tumenyonywa vya kutosha!

Mshahara wa mkuu wa kaya ni 32Milion.
 
Sio kweli..... Watanzania wapo wenye uwezo mkubwa sana tena wanaofanya kazi nchini kwa uaminifu mkubwa sana...
Sawa...hata mimi sikuwa naona sababu ya kung'ang'ana na hao walio nje...
Lakini kama uliwaomba warudi treat them with respect...
Maana watakuwa wanajuta kilichowaleta Tz...

Siwaungi mkono sababu hata ningekuwa mimi ni either ningekataa kurudi au ningekubali mshahara ambao ni realistic...si 40m toka kwa kanchi masikini...

Lakini kama ni kweli waliombwa warudi...regardless waliombwa na rais wa awamu ipi...wasiwe treated kama wezi...
Mshahara ungeweza kupunguzwa bila maneno makali...kama wataachia ngazi kivyao...
 
Panga lipite,inawezekana wanastahili lakini sio kwa nchi changa kama hii,ila pia isije ikawa tunamuweka mzungu au foreigner yoyote kushika hiyo nafasi halafu mnamlipa tena 36m hapo hatutamuelewa mheshimiwa Rais.
 
Back
Top Bottom