Mashine za kuuzia mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo

A condom machine is a vending machine for the sale of condoms. Condom machines are often placed in public toilets, subway stations and airports as an effort of health protection. Many pharmacies also keep one outside, for after-hours access. Rare examples exist to dispense female condoms.[1]

Soure: Weekpedia
 
Cheki baadhi ya mifano yake...
 

Attachments

  • 180px-Condom_vendor.jpg
    180px-Condom_vendor.jpg
    9.5 KB · Views: 42
  • 458px-Condom_vendor.jpg
    458px-Condom_vendor.jpg
    41.3 KB · Views: 41
Hii safi sana. Ila waangalie sehemu za kuziweka bongo maana jua kali sana liataharibu ndomu.
Kang ushauri wa kitaalamu ni huu:

According to the United States Food and Drug Administration, when using condoms from a machine, one should check the expiration date, that the condoms are latex and labelled for disease prevention, and that the machine is not exposed to direct sunlight or other source of extreme temperatures.
 
Nazo zitahitaji uwe na card ya kuchukulia?

Mkuu,

Kama hizo machine zitakuwa ktk mfumo wa vending machine hakutakuwa na haja ya kutumia kadi. Wasiwasi wangu ni pale ambapo hizi machine zitakapowekwa mahali pa wazi kiasi cha hata watoto wadogo kuweza kuzi-access.
 
Kang ushauri wa kitaalamu ni huu:

According to the United States Food and Drug Administration, when using condoms from a machine, one should check the expiration date, that the condoms are latex and labelled for disease prevention, and that the machine is not exposed to direct sunlight or other source of extreme temperatures.

Dar na Moro ni maeneo ambayo sometimes joto huwa kali sana, sijui ni kwa jinsi gani quality ya hizo condoms zitatunzwa kwa vipi ktk mazingira kama haya, pia ikizingatiwa hali ya kukatikakatika kwa umeme. Naona hiki ni kama chambo flani hivi cha wazungu kukiteketeza kizazi cha mtu mweusi.
 
Kwani Pinda alitumia takwimu zipi? au hizi za kampeni ya kupima kwa hiari.
Kumbuka TZ hatuna takimwi sahihi za mambo mbalimbali huwa tunafanya assumption na mara nyingi reference inakuwa kutoka kwenye kitu/sehemu ya hisia

Takwimu nyingi zinakuwa based on sampling. Huwezi kumpima kila mTz ili kujua ni wangapi wenye maambukizi. Sina hakika kama sampling ndio hisia.

Hata hivyo kuna aina nyengine ya takwimu, hizi zinatambulika kitaalamu kama takwimu za kupika. Yaani mtakwimu anabuni takwimu ili kukidhi majumuisho anayoyakusudia.

Ukweli unabaki tu kuwa all-in-all takwimu nyingi hapa bongo ni fwamba.
 
Dar na Moro ni maeneo ambayo sometimes joto huwa kali sana, sijui ni kwa jinsi gani quality ya hizo condoms zitatunzwa kwa vipi ktk mazingira kama haya, pia ikizingatiwa hali ya kukatikakatika kwa umeme. Naona hiki ni kama chambo flani hivi cha wazungu kukiteketeza kizazi cha mtu mweusi.
Mkuu ndio maana nilisema ni jambo linalo hitaji utafiti wa kina...PSI kama wamefanya utafiti na kuanza ktk hiyo mikoa basi ny vyema.

otherwise kama tunaendelea kutumika kama dampo la mashine mbovu za ulaya na asia basi kama kawaida itakuwa ni dalili ya ufisadi mwingine...nawakalisha
 
Kuepuka matumizi kwa watoto labda waziweke hivi :)
 

Attachments

  • a331_c1.jpg
    a331_c1.jpg
    34.3 KB · Views: 41
KUTOKANA na kampeni za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa la ukimwi, Watanzania wanatarajia kufungiwa mashine za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' nchini kote.

Mashine hizo zinatarajiwa kufungwa na Shirika la PSI- Tanzania ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa mipira hiyo kiurahisi.

Taarifa zilizotoka Makao ya Makuu ya Shirika la PSI nchini zimesema kuwa mashine hizo zenye mfano kama wa kutolea fedha wanatarajia kufunga mapema mwezi ujao.

Taarifa hizo zilisema kuwa mashine hizo zitaanza kufungwa Mkoani Morogoro katika baa mbalimbali zilizoko Mkoani humo.

Meneja wa PSI Mkoani Morogoro, Godwin Msafiri alithibitisha na kusema mashine hizo zitaanza kufungwa mkoani humo.

Alisema kuwa shirika hilo litaanza kufunga mashine hizo zipatazo 15 katika baa mbalimbali za mkoani humo na zingine kufungwa katika mji wa kitalii Mikumi mapema mwezi ujao.

Alisema lengo la kuanzisha kufunga mashine hizo ni kuinua Waatanzania walio wengi ambao wanadharau matumizi ya mipira hiyo kwa kuwa janga la ugonjwa wa ukimwi umekuwa ni tishio nchini.

Alisema kwa kuwa watu wengi huwa wanaona kazi kufika dukani na kununua zana hiyo ambayo ni muhimu kwa wale ambao wanafanya ngono zembe hivyo mashine hizo zitawarahisishia.

Alisema Shirika hilo litasambaza mashine hizo nchini kote nzima ila wameanza Morogoro.

Source: Nifahamishe.com

Hizi mamlaka zinahamasisha ngono then zinaipinga. Au wanafanya tafiti? KWani hizo kondom ukishanunua unaenda kutumia na nani? mkeo? La hasha, ni wapitanjia tu ambao wengi wao ni makahaba ambao mamlaka zinajifanya kuwapiga vita. Hapa kuna bonge la picha, tena ya kihindi.
 
Mimi nafikiri cha kwanza kabisa ni kubadili tabia, kuwa na mpenzi mmoja, kumtumikia MUNGU na mwisho kiwe CONDOM...maana hatakuzitumia huwa hatuzitumii huwa tunazivaa wakati wa stori tuu...
 
This is good news hasa kwenye sehemu za starehe... ingawa tumechelewa lakini si haba kwa wenzetu kuho duniani zilikuwepo since the 90s
 
Condom is just a Philosopy. Why use it? lets nature takes its course.
 
Toba ya rabi!!! Uzinifu sasa unatengezewa mashine...

Yale yale ya Benedictus kukataza utumiaji wa kondom bila kujua kwamba wanaokufa wengi na ugonjwa huu ni afrika ambako ndiko kwenye waumini wengi wakikatoliki.

God Bless Benedictus.
 
mimi nadhani hamna anayeelewa haswa madhara ya hizi condoms . hivi kwanini kujificha kama ufanyacho ni sahihi ??!!

maambukizi yanakwenda juu exponentially na condoms zipo still mnaleta vending machines ?? jiulize kwanza nini sababu ya maambukizi kuongezeka sio kuongeza condoms . watz bwana malimbukeni sijawahi ona ?? hivi inamaana wote waliopata maambukizi hawakujua haswa namna ya kutumia maana wanasema eti matumizi mabovu ???

wengine eti wanajisahau kutumia ??

wengine mkwanja wako ??

kama ndivyo hata wangeleta za chuma bado haisaidii sana sana inahamasisha hata wale wa mwaka mmoja kujaribu . mmenisoma izraeli amefika hakuna atakayepona hapa ???? toba natamani ningeweza piga marufuku . unajua ukipiga marufuku utumiaji wa condoms watu watakuwa na simile /displini wasemavyo waswaenglish . vinginevyo hata wakuzika hatakwepo itabaki fisi wakatuzike. elimikeni mlio malimbukeni or A & B don"t go "C" for sure you will die
 
Jamani hili jambo kwa kweli linanishangaza. Mimi binafsi kwa kweli naona kama serikali hapa imeteleza au inajaribu kupoteza muda na fedha na sio kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Nasema hivi kwa sababu suala la kutumia kondomu ni la binafsi sana. (Personal). Sio kwamba watu hawana kondomu wakati wanajamiiana, wanakuwa nazo huko chumbani waliko ila kutumia hawataki. Kwa kuweka hizi ATM za kondomu watu watanunua na wataishia kuziacha chumbani kwao au vyumba vya wageni bila kuzitumia na hapa kinachotakiwa sio takwimu kuwa kondomu zinachukuliwa nyingi hivyo zinatumika. ni kujidanganya. Kama ni kutumika ni kwa asilimia chache sana.
Mimi binafsi naona labda approach nyingine ingetumika kupigana na hili tatizo na hasa nguvu ielekezwe kwa wanaume kwani wao wakibadilika nina hakika hili tatizo litapungua sana.
Wana JF hapo nyie mnasemaje
 
Mimi binafsi naona labda approach nyingine ingetumika kupigana na hili tatizo na hasa nguvu ielekezwe kwa wanaume kwani wao wakibadilika nina hakika hili tatizo litapungua sana.
Wana JF hapo nyie mnasemaje


Aisee Wakwetu.

Una uhakika kwamba wanaume ndio kikwazo kwa vita ya ukimwi?

Kivipi ndugu?

Mimi nilidhani kwamba unagomba na hizi ATM, kumbe ugomvi wako ni jinsia?

Hujawahi kupata taarifa kwamba kuna condom za kike (CARE) ambapo wanawake ndo wa kwanza kuziponda?

Hoja niionayo mimi ni Je, wamefanya study gani iliyopelekea uamuzi kwamba ATM zitafanya utumiaji wa Condom uongezeke?

Mbona zimejaa hadi kwenye maduka ya vijijini, so the issue is not availability!

Mtu akienda dukani, atavunga kuagiza hata lawalawa, kisha akachukua Condom, lakini kwenda pale kwenye ATM mchana wa jua kali, inagharimu roho, na mtu anaonekana waziwazi kwamba anaelekea kufanya uzinzi!

Lakini pia hizo ATM zitawekwa wapi,vijijini zitapelekwa?
'Refill' yake itakuwa reliable? au in no time yatakuwa mazalio ya mende na 'nsyeleni', kama callbox za TTCL?

 
Back
Top Bottom