Mashine za kuuzia mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine za kuuzia mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Apr 22, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Apr 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUTOKANA na kampeni za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa la ukimwi, Watanzania wanatarajia kufungiwa mashine za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' nchini kote.

  Mashine hizo zinatarajiwa kufungwa na Shirika la PSI- Tanzania ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa mipira hiyo kiurahisi.

  Taarifa zilizotoka Makao ya Makuu ya Shirika la PSI nchini zimesema kuwa mashine hizo zenye mfano kama wa kutolea fedha wanatarajia kufunga mapema mwezi ujao.

  Taarifa hizo zilisema kuwa mashine hizo zitaanza kufungwa Mkoani Morogoro katika baa mbalimbali zilizoko Mkoani humo.

  Meneja wa PSI Mkoani Morogoro, Godwin Msafiri alithibitisha na kusema mashine hizo zitaanza kufungwa mkoani humo.

  Alisema kuwa shirika hilo litaanza kufunga mashine hizo zipatazo 15 katika baa mbalimbali za mkoani humo na zingine kufungwa katika mji wa kitalii Mikumi mapema mwezi ujao.

  Alisema lengo la kuanzisha kufunga mashine hizo ni kuinua Waatanzania walio wengi ambao wanadharau matumizi ya mipira hiyo kwa kuwa janga la ugonjwa wa ukimwi umekuwa ni tishio nchini.

  Alisema kwa kuwa watu wengi huwa wanaona kazi kufika dukani na kununua zana hiyo ambayo ni muhimu kwa wale ambao wanafanya ngono zembe hivyo mashine hizo zitawarahisishia.

  Alisema Shirika hilo litasambaza mashine hizo nchini kote nzima ila wameanza Morogoro.

  Source: Nifahamishe.com
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Toba ya rabi!!! Uzinifu sasa unatengezewa mashine...
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh wanachekesha.... walianza na kusambaza mipira hiyo kila hoteli na maguest watu wakawa hawatumii sasa za ATM, Yaani mtu utoke uende kwenye atm, labda kama zitaunganishwa na zile za pesa ili watu wasijue lengo lako ni nini (maana aibu ya kununua condom dukani na ile ya kusimama kwenye foleni ya ATM condom ni sawa)

  Nafikiri kwanza wangehamasisha kutokomeza aibu hii na kifanya mtu kutamka condom hadharani ni kitu cha kawaida.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yaani jinius
  ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni. Kwani Uganda waliwezaje? au nao walihamasisha condom? Hivi ni kweli kuwa watanzania tumeshidwa kabisa kuelewa lugha ya Abstinance and being Faithfull (A&B)? Tunakazania Condomize?
   
 5. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa hii ni fungulia ngono
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Apr 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe...ni ATM au Vending machines?
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  naamini hizi vending machine zitakuwa zinauza sana nyakati ya usiku na sikukuu.
  lakini hebu tuulizane
  kuna mtu humu ndani anatumia kondom?? mie naona ujinga kuitumia.
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,582
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Msanii unahatarisha maisha yako.

  Hizo Vending machine zitawekwa karibu na baa zote ambazo huwa zinakuwa na wateja wengi sana nyakati za usiku.
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nazo zitahitaji uwe na card ya kuchukulia?
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Speaking from a secular point of view, nadhani ni hatua nzuri tu katika jitihada za kusambaza condoms ili mtu akiacha kutumia basi iwe ameamua kutotumia lakini si kwa sababu ameshindwa kuzipata. Itakuwa vema kama wataweka machine hizi sehemu ambazo kwa kiasi zina faragha ili kuruhusu watumiaji kujihudumia bila aibu.

  Ningewashauri pia kusambaza condoms katika mahoteli and gesti hapa nchini na kuhakikisha vyumba vya mahoteli/gesti vinakuwa na condoms za kutosha muda wote. Pia kuwepo jitihada za makusudi kuongeza uhamasishaji wa matumizi ya condom za kike.
   
  Last edited: Apr 22, 2009
 11. Makonyagi

  Makonyagi Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waweke ndom mpaka kwenye public toilets hic!
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Sielewi watatumia njia gani I mean sehemu zitakazo wekwa hizi mashine lakini the best place would be in toleits and alike,kuchukua no need of using special cards,just use your coin as it was during call boxes,nowdays juke boxes au kama umewahi kuona tangazo moja la cocacola,jamaa anaweka sarafu then akibonyeza sehemu inatoka soda.Therefore the same will apply to those CONDOM VENDING MACHINES(CVM)
  hilo jina nimetunga mimi.
  Swali:Kama takwimu za watu wenye VVU/HIV inaongezeka pamoja na matangazo mengi kwenye vyombo vya habari,warsha,makongamano nk kuhusu matumizi ya KONDOMU,je wananchi hawaelewi matumizi sahihi ya kondomu au hawazipati kwa wingi na kwa muda muafaka?
  Kama hawajui matumizi sahihi kwanini wakati warsha na makongamano yamefanyika?
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mhhhh.. hapa swala ni kumrejea muumba tu, hiyo mipira hata itandazwe bara bara nzima tena bure mtu unajichukulia, bado watu wanapenda ile direct contac! simulizi nyingi ambazo nimekuwa nikizisikia kuhusu ndomu,
  wengi huivaa mwanzoni vikinoga huhisi zinawakera na kuirusha kando na husonga mbele, si unajua wakati huo decision huwa zinafanywa na 'mr small head'

  Wengine huzitumia kwa mara za mwanzo na demu, muda ukipita hujisahau/huzoea na kumua upgrade mawazoni kwamba yu salama na kwamba yeye ndiye huyo mpenzi mmoja mwaminifu!
  Sasa hapo hata iweje, kama hatutubu na kumrejea maulana tutakwisha tu pamoja na marobota na ma ATM ya kondomu yatuzungukayo!
   
 14. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka Pinda alisema juzi juzi hapa kwamba takwimu zinaonyesha kupungua, tofauti na ulivyoandika kuwa zinaongezeka !!
   
 15. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwani Pinda alitumia takwimu zipi? au hizi za kampeni ya kupima kwa hiari.
  Kumbuka TZ hatuna takimwi sahihi za mambo mbalimbali huwa tunafanya assumption na mara nyingi reference inakuwa kutoka kwenye kitu/sehemu ya hisia
   
 16. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mmmmh Bongo tambarare...
   
 17. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hapa panahitaji utafiti wa kina juu ya ufanisi wake maana si kushabikia tu...
   
 18. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  HUKO ASIA WANAZO HIZI CHEKI HAPA:

  -------------------------------------------------------------------------------------

  Now, condoms available at the drop of a coin inVizag

  As many as 400 machines have been installed in city
  Inspiration comes from Bangalore
  SEED project director sees steady rise in use of condoms in Vizag
  Over a decade later, the perception of youths seems to have changed little when it comes to buying condoms across the counter. This is in contrast to the disco and pub culture fast catching up in the metro.

  Relax! There is no longer need to feel shy to buy condoms. They can be drawn from a machine like cash from an ATM. Surprised? The CVMs (Condom Vending Machines) are here to literally deliver the `goods' at the drop of a coin. Over 400 such machines have been installed in the city and district for the convenience those who need them.

  The present CVM s installed are of two varieties -- the bigger ones which deliver three different varieties or the smaller ones which issue single variety pouches," he says. The Mahila Vikasa Samstha has installed free boxes for supply of condoms at public places like Collectorate junction.

  Source: The Hindu
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hii safi sana. Ila waangalie sehemu za kuziweka bongo maana jua kali sana liataharibu ndomu.
   
 20. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa nchi nyingine siyo jambo geni kihivyo...ila kwa hapa kwetu litahitaji awareness campaign kwa sana
   
Loading...