Mashine ya kunyanyua matiti yaingia nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine ya kunyanyua matiti yaingia nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tembeleh2, Mar 12, 2012.

 1. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii sayansi na teknologia sasa inatupeleka pabaya. Hivi karibuni wataalam toka china wameleta mashine maalumu ya kunyanyua matiti (yawe na muonekano wa saa 6) ambayo itawasaidia kina dada/mama wenye maziwa yaliyoanguka au kusinyaa kuwa na muonekano mzuri. Huduma hii imeshaanza kutolewa hapa nchini maeneo ya sinza. Wana JF hivi hawa wachina wanatutakia mema kweli??? Je wanaweka wazi madhara yanayoweza kuwapata baadae hao watakaonyanyua matiti yao??? je shughuli hii ina tija kwa watanzania???
   
 2. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...walete na mashine za kunyanyua akili za wanafunzi wetu ili ufaulu uongezeke kwani mtokeo ya akina "Mwanaasha" ni janga la kitaifa...
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mashine ya kuinua matiti ya wanawake yaingia nchini Send to a friend
  Sunday, 11 March 2012 10:19

  WANAWAKE WAFURIKA KUPATA HUDUMA
  Na Julieth Kulangwa
  BIASHARA huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo, imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero wanawake wenye matiti yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.

  Wachina wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini, zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele, kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.

  Huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam.

  Haikuwa rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
  Mbali na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.

  Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.

  Jinsi matiti yanavyosimamishwa
  Mashine hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona pichani.

  Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.
  Pang anasema, zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita, inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.

  Mtaalamu huyo ambaye anazungumza Kichina na kutafsiriwa na meneja wa saluni hiyo, anaelezea namna anavyofanya kazi ya kuyarudisha matiti kwa muda huo.

  “Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja wetu akifika hapa, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer za nywele,
  “Baada ya kumlaza katika kitanda kile, tunachukua kitu mfano wa bakuli (cups) mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” anasema Pang.

  Mtaalamu huyo anasema mashine hiyo ikiwashwa inavuta kama ‘vacuum’, na inaweza kuongezwa kasi au kupunguzwa kama inavyofanyika kwenye mashine za kufanyia mazoezi.

  “Tunaiwasha mashine kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika,”anasema Pang.

  Tangu mashine hiyo iwasili nchini, takribani mwezi mmoja uliopita, Pang anasema ana wateja wanane anaowahudumia kwa nyakati tofauti ambao wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo.

  Ni kweli mashine hii inasaidia?
  Akizungumza kwa njia ya simu, mmoja wa wateja anayepata huduma hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu Irene anasema, ni wiki ya tatu sasa tangu aanze kupata huduma hiyo, anakiri kuwa matiti yake sasa yameanza kuwa magumu tofauti na mwanzo.

  “Kusema kweli nilikuwa na matiti yaliyosinyaa wala si kulala tu kama ulivyouliza, ila naona sasa yameanza kuwa magumu na kurudi juu kidogo,” anasema Irene.

  Akizungumzia ugumu anaoupata katika zoezi hilo, anasema safari za kila wiki saluni na zile dakika 45 za kukaa kwenye mashine zinamchosha, lakini kwa kuwa amedhamiria, amejitoa mpaka zoezi hilo litakapokamilika.
  Matiti yanaweza kulegea tena?

  Pang anasema kama matiti yanalegea kwa sababu fulani mfano uzazi wa watoto wengi, basi yanaweza kulegea tena kama mtu atajifungua na kunyonyesha kwa muda huo.Aidha anasema wanawake wenye matiti makubwa, ni rahisi kuanguka kama hawatayavalisha sidiria kwa muda mrefu.

  “Wanawake wenye matiti makubwa huwa nawashauri kuvaa sidiria hasa wakati wa mchana na usiku wanaweza kuacha kuzivaa, hii inasaidia kuimarisha misuli inayoyabeba matiti,” anasema Pang.

  Jamii inazungumziaje jambo hili
  Baada ya kusikia kuwepo kwa mashine hii nchini, wanawake mbalimbali wamesema wanatamani kupata huduma hiyo lakini wengine, walionyesha woga juu ya matokeo yake.

  “Ni kweli baada ya kunyonyesha watoto wawili sasa matiti yamelegea kabisa, natamani yarudi kama wakati ule wa usichana wangu, lakini nahofia huenda mbele ya safari nikapata madhara,” anasema Linda Masatu.

  Linda anaongeza kusema kuwa ni vizuri mwanamke akawa na matiti yaliyojaa vizuri, lakini anahofia njia zinaweza kuwa na madhara, huku akisema kama ingetokea njia nyingine ya asili asingesita kuifuata.

  Naye Batuli Famau, anasema mwanamke anapokuwa na matiti yaliyosinyaa mvuto wake hupungua, hata anapovaa sidiria anakuwa amebadili mwonekano wa nje tu, lakini ndani bado anakuwa vilevile.

  “Mwanamke mrembo ni yule mwenye matiti mazuri, sasa inapobidi kutumia njia fulani ili yarudi kama tulipokuwa vigoli, tutafanya tu ili mradi kama njia hizo hazitatuangamiza,” anasema
  Wanaume nao wameonekana kuunga mkono zoezi la kusimamisha matiti ingawa wengine hawaungi mkono utumiaji wa mashine hii.

  Augustino Magara anasema: “Ni kweli mwanamke mwenye matiti magumu anavutia kuliko yaliolegea na kulala, lakini sasa tuwe makini kabla wake zetu hawajaumia katika mashine, hizi”

  “Wote tunajua sababu zilizosababisha matiti ya wake zetu yalegee, sioni sababu ya kusema tunataka yaliyomagumu, tuwapende wake zetu hivi hivi na tuwape moyo,” anasema Nganara.

  Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.

  “Ingelikuwa mazoezi hayo yanachukua muda mfupi, kweli tungepata wasiwasi kwa kuwa, unapoisimamisha misuli kwa haraka ni lazima madhara yatokee, lakini hili la mazoezi, bado sifahamu,” anasema Dk Mosha.

  MY TAKE

  Sisi wanaume ndiyo chanzo cha matatizo haya yote kwa wanawake wetu. Kama wanaume tungekuwa hatutaki, MATITI yaliyosimama, MAKALIO makubwa, MKOROGO/KUJICHUBUA hii Biashara yote leo isingalikuwapo. Wanaume TUBADILIKENI!
   
 4. S

  Shansila Senior Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tija ipo,kwani kama mtu maziwa yake yalishasurrender akiyanyanyua huoni kuwa atavutia zaidi?Ishu muhimu hapa ni kujua kama kuna madhara,mama zetu waachane nazo.
   
 5. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Ngono ni natural habit ya kiumbe hai. Hili ni eneo ambalo halina utashi wa busara bali utashi wa uhitaji. Wanawake wanaishi ili wawapendeze wanaume. Ukiangalia wanawake walio kwenye ndoa na ambao umri wao umesonga hawapendi kuzeeka! Wangependa wapambane na vigori! Wanaume na sisi huwa tunapenda kitu kipya hasa matiti yaliyosimama! Kwenye ngono hakuna busara bali ni uhitaji tena wa kitambo! Ubaya wake uhitaji haukomi! Hapo ndipo china anapofaidikia!
   
 6. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Swali: kwa nini wanawake wengi huwa wanakimbilia kuzitumia technolojia wasizosifahamu bila kuchunguza madhara yake?
   
 7. J

  Jqnakei Senior Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwemakini na kutumia kitu ambacho mwisho wake haujui. Isije ikawa aibu zaidi kwa watumiaji penda kuhakisha makeo mpaka mwisho wake ni nn?
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hili si jambo jipya, na warembo wengi na celebs walishapata huduma hii kitambo. Ondoa mashaka , mpeleke mkeo akasimamishe mewata awe kama W. Houston(RIP), et cetera.
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  TANGAZO LA BIASHARA (kichinachina!
  Are your lakes a.k.a milk, sleeping? Do you want them standing ?
  Come to us, we will stand them up 6 hours.
   
 10. n

  ndughuri msuya Senior Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  [JFMP3][/JFMP3]Hii ni hatari kama hatutakuwa makini,mishipa imepungua nguvu alafu unaisimamisha kwa nguvu'CHUNGA SANA.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mimi sivutiwi na matiti katika mwanamke!
  Haya dada zetu, tenda hiyooo!
  arousal01.jpg
   
 12. K

  Kemugesi New Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dada zangu tuwe makini na hizi mashine zinazokuja,baada ya urembo kinachofuata ni kansa.tujiulize mara mbili kabla ya kwenda huko
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Majuto ni mkukuu!
  Kulazimisha mishipa kukaza kunaweza kuzalisha hali hii kwenye picha!
  kansa ya titi.jpg
   
 14. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hapa na ndoa ndo itafikia ukomo aisee!
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Acha hiyo tech ifanye kazi. Utakuta mdada mzima, anajua kuwa tayari 'malapulapu yameshatamalaki, yeye anavaa suruali yake na kitop chake halafu bila sidiria huyooooo anaingia mtaani..........yaani unamuangalia unajiuliza hivi huyu hana mpenzi amwambie walau avae sidiria? Halafu utakuta anadai eti ana gundu mbona hatokewi! nani akutokee wakati mtu akikuangalia tu 'hamu' yote inaisha!

  Jamani kina dada ambao kifuani ni kama kandambili, nendeni mkapate hiyo huduma walau wageni wakija waone kuwa kanchi ketu pamoja na kuwa kamejaa ufisadi wlau kina warembo wanaovuti bwana, aaaaaah!
   
 16. canaan

  canaan Member

  #16
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Makubwa haya! Napita tu mie
   
 17. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wanawake wakiwezeshwa wanaweza. MEWATA MPO?
   
 18. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Kutokujiamini tu, km kupendwa utapendwa tu hata km una malapa kifuani.
  Na mbona mazoezi yanasaidia sn!? Unaweza ukatengeneza mwili vizuri tu kwa kufanya mazoezi
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hata uume ukisisimshwa huwa kama hivyo mashine inavyofanya.lakini msisimko ukiisha misuli hulegea na mzunguko wa damu kupingua na kurudia ile ile hali ya msinyao
   
 20. MissyNana

  MissyNana Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndo waliwaoooooo!
   
Loading...