Mashine ya kumwagilia ile ya kurusha maji juu

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
16,132
31,125
Wadau nalima tikiti maji kanda ya ziwa, ziwani kabisa.

Nategemea kiwe cha umwagiliaji heka tatu. Changamoto iliyopo namwagiliaje? Water pump ya kawaida naona itakuwa kazi sana.

Nimewaza ile ya kurusha maji juu. Sijui nko sawa na kama nko sawa, naipataje na bei yake je? Au kama kuna wazo jingine jinsi ya kumwagilia.

Nategemea kupanda mbegu week hii.
 
Unaweza kumwagilia kwa sprinkler (kurusha na kusambaza Maji kwa juu) au drip irrigation

Hivi vifaa vipo vingi
 
  • Thanks
Reactions: amu
unaweza kumwagilia kwa sprinkler (kurusha na kusambaza Maji kwa juu) au drip irrigation

hivi vifaa vipo vingi
Ahsante hata jina nlikuwa siijui.....sasa hiyo naweza pata kwa sh ngapi......sprinkler
 
Sikushauri kurusha maji juu. Njia bora ni kutumia matone. Unakuwa na chanzo nchako cha maji, unavuta maji kwa pampu alafu unasambaza kwa kutumia mabomba madogo yenye matundu madogo ambayo yatatoa matone ya maji kwenye mashina ya miche tuu.
 
Sprinkler kati 10,000 na 20,000. Jitahidi utengeneze mfumo wa umwagiliaji wa matone baada ya kukuza mtaji.

Kwa sasa Hongera sana.
More grease to your elbows
 
Ahsante sana .....hii ndo mara ya kwanza na je naanza kumwagilia baada ya mda gani?????
 
Sikushauri kurusha maji juu. Njia bora ni kutumia matone. Unakuwa na chanzo nchako cha maji, unavuta maji kwa pampu alafu unasambaza kwa kutumia mabomba madogo yenye matundu madogo ambayo yatatoa matone ya maji kwenye mashina ya miche tuu.
Faida ya kutumia matone badala ya kurusha maji ni ipi?

In terms of cost, which is cost effective?
 
Wadau nalima tikiti maji kanda ya ziwa..ziwani kabisa nategemea kiwe cha umwagiliaji ....heka tatu...changamoto iliyopo namwagiliaje ....water pump ya kawaida naona itakuwa kazi sana.....nimewaza ile ya kurusha maji juu.....sijui nko sawa na kama nko sawa naipataje na bei yake je....au kama kuna wazo jingine jinsi ya kumwagilia ....nategemea kupanda mbegu week hii....
Sprinkler tatizo ni kutumia maji mengi na pia husababisha magonjwa mengi ya ukungu maana ni kama unalima msimu wa mvua ,drip inatumia maji machache na pia ni bora sema cost yake iko juu tofauti na sprinkler,so ukiamua kutumia sprinkler andaa na dawa za kuzuia na kutibu ukungu mancozeb-mancozeb+metalaxyl-azoxystrobin-difenoconaxole-azoxystrobin+difenoconaxole (hizo ni active ingredients za dawa utaanza na dawa za kuzuia ukungu mwanzo wa msimu na mashambulizi yakianza unaanza kutibu kuanzia ya nguvu ndogo mpaka kufika kwenye yenye nguvu zaidi)
 
Hata kipindi cha kiangazi nako kunashida zake maana wadudu wanakua wengi sana
so kipi ni kipindi ambacho kinagharama nafuu zaidi. mie ninataka kufanya kipindi cha masika ili kupunguza gharama ya nguvu kazi ya kumwagilia maji.. maana ndo msimu wangu wa kwanza
 
Matone (drip irrigation) inasaidia sana kubana matumizi ya maji. Pia, kama hakuna mvua ina maana majani hayataota hovyo shambani mwako utakuwa umepunguza tatizo la kupalilia mara kwa mara. Hii ni kwa sababu matone yanadondokea kwenye shina tuu na unyevu hauendi mbali.

Lingine ni kama alivyozungumza mdau kwamba sprinkler inasababisha magonjwa kwenye majani na matunda.
 
Hapo drip irrigation inahusika, chakufanya tafuta wataalamu wa kilimo watakushauri ipi njia nuzri ya urahisi na yenye bei nafuu
 
Jitahidi utengeneze mfumo wa umwagiliaji wa matone baada ya kukuza mtaji.

Kwa sasa Hongera sana.
More grease to your elbows
Naunga mkono wazo lako. Mfumo wa umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ni cost effective zaidi ukilinganisha na wa sprinkler, hasa kwenye matumizi bora ya maji. Ukitumia sprinkler, utalazimika kutumia maji mengi, kwa sababi mengine yatamwagilia hata sehemy ambazo hazina mimea. Ila ukitumia mfumo wa matone, maji yanakwenda kumwagilia mmea husika moja kwa moja, bila kupotea.
 
Nawaza kuanza Kilimo hicho pia naomba kuwa mgeni wako siku moja nije kujifunza kwako Niko Nyegezi Mza. Ntakupataje? 0753101293
 
Matikiti maji hayahitaji maji mengi saana na ukitaka kutumia njia ya umwagiliaji inahtaji uwe ba initial capital kubwa

Kwa eneo la heka tatu na ukitaka umwagilia kwa kutumia sprinkler method inayomwaga maji 6*6 m itakubid utumie jetgun (boom sprayer) ambayo inahtaj pump yenye uwezo mkubwa

Drip irrigation ni sufficient kama eneo ni dogo na mahtaji yake sio makubwa saana
BUT
Kabla hujaanza kutumia any method ya irrigation jiulize maswal haya;

1: type of crop u what to grow
2: Soil type
3: water requirement of the crop
4: source of water nk
Hapo waweza angalia una kias gan mfukon na ukaamua baaada ya kufatilia kwa makin.
NAPITA TU
 
Hata mie nimepata changamoto jinsi ya kunwagilia na capital yangu ni ndogo...so nimeamua kwa kua ni pembeni ya ziwa.. nachimba bwawa najaza maji kisha naanza kumwagilia kwa mkoni kwa kutumia ile can yenye matundu matundu......nija vijana watatu watamwagilia asubuhi na jioni na mie mwenyewe nikiwepo.....hiyo sprinkler haifai maana wataalam wamesema haifai
 
Jamani tusipende kukariri theories. Ni kweli sprinkler sio nzuri compare na drip irrigation. Lakini wenzetu wenye mashamba makubwa katika nchi zilizoendelea hawatumii drip irrigation maana inakuwa soo expensive compare na sprinkler. Sprinkler inatumika vizuri kama utafata taratibu za kiutaharamu. Mi sio mtaharamu wa kilimo, lakini moja ya utaharam wa kutumia sprinkler ni unabidi umwagilizie asubuhi na sio jioni. Unapomwagilizia asubuh jua linapowaka ule unyevunyevu unakauka kutoka kwenye majani ya mimea na hata unapungua kwenye udongo. Ukimwagilizia jioni kwa sprinkler ule unyevu hukaa mpaka next suny day ambyo husababisha risk kubwa sa kusambaa kwa magonjwa. Sasa basi mimi ushauri wangu ni kwamba kwakuwa upo karibu na chanzo cha maji ya kutosha waweza tumia sprinkler vizur kwa kufata masharit yake na utafanikiwa 2. Kumbuka drip irrigation orgin yake ni Israel ambapo hwana maji ya kutosha kwa kilimo. So ili kupunguza matumizi ya maji ndyomaana wakaja na iyo drip irrigation. Ila katika nchi kama USA, China etc kilimo kikubwa wanatumia sprinklers.
 
Unataka lima kisiwa gani?
Kuna fursa za kuwezeshwa kama utapenda lima kwa umwagiliaji katika visiwa vya ukara, yani unakopeshwa mashine ya umwagiliaji na wasambaza umeme visiwani ( JUMEME). Kama haiko specific na kisiwa unachotaka lima kamatia hiyo fursa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom