Mashekhe waliwekwa kizuini na kuhukumiwa kunyongwa misikiti haikufutiwa usajili ,Kakobe alihisiwa sio raia lakini kanisa lake halikufutiwa usajili ,

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
2,308
Reaction score
4,687
Hii inamaana kwamba makanisa 2000 nchi nzima na wachungaji na maaskofu wote wa kanisa la ufufuo na uzima kuanzia dar mpaka huko ujiji na maeneo ya katonto huko sumbawanga wote wanaadhibiwa Kwa kosa la mtu mmoja !! Kanisa linafutwa !! Amekosea tundu lissu amekamatwa lissu na taasisi inaendelea na oparesheni zake,miaka michache iliyopita kakobe aliingia kwenye mzozo mkubwa na serikali ,walakini serikali haikulifuta kanisa la full gospel Bali wali Dili na Zachary kakobe walivyoweza wao ! Miaka ya nyuma zaidi alizuka askofu mtikila wa kanisa la full salvation church yeye alikuwa na mapambano ya wazi na serikali na mara nyingine aliwekwa ndani na kufungwa hatukuwahi kusikia kanisa la full salvation limefutiwa usajili, askofu severin niwemugizi wa huko ngara aliingia kwenye mgogoro na serikali ya jpm ,hatua kadhaa zilichukuliwa dhidi yake lakini kanisa lake halikufutiwa usajili ,mapadri wa kanisa katoliki walitoa waraka kwa serikali wakiwa kanisani ,hatukusikia kanisa katoliki limefutiwa usajili Tanzania ,mchungaji na askofu ndugu mbarikiwa mwakipesile wa huko mbeya aliwekwa gereza lakini kanisa lake halikufungwa Wala kufutwa !! Ninani amemshauri msajili kufanya maamuzi ya aina hii ? Kama ni shinikizo limetoka Kwa nani na ninani au ni taasisi Gani itafuata? Maaskofu wa makanisa mengine najua mtasema hili haliwahusu lakini tambueni kwamba hatujui ni taasisi ipi itafuata baada ya hapa ! Mungu ibariki Tanzania
 
Hapo ndo mnakosea kuingiza waislamu katika hi issue ya siasa, kila mtu anaona ni siasa wewe unaongiza Dini ili tugawanyike kwanini?
 
Muache ajaribu kulifuta Kanisa la Mungu ili naye afutwe na Mungu
 
Ni mihemko tu bila shaka wataenda mahakamani.
 
Hapo ndo mnakosea kuingiza waislamu katika hi issue ya siasa, kila mtu anaona ni siasa wewe unaongiza Dini ili tugawanyike kwanini?
Safi sana tunalipiza mlivyofanya MwembechaišŸ”„šŸ”„šŸ”„
 
Mtu ameshaingia kwenye 18 anatengenezewa ajali ya kisiasa huku mwenyewe anakenua anaona anasaidiwa.
 
Hapo ndo mnakosea kuingiza waislamu katika hi issue ya siasa, kila mtu anaona ni siasa wewe unaongiza Dini ili tugawanyike kwanini?
Hata waislam nao ni dini sijataka mgawanyike nimetoa mifano halisi
 
Misikiti haisajiliwi kama kanisa wala hailipi kodi mna tunaenda kufanya ibada na kuondoka

Ila makanisa m naona kma ni biashara flani hivi kwanini yalipe kodi wakati ni sehemu za ibada?

Anaejua atwambie
 
Misikiti haisajiliwi kama kanisa wala hailipi kodi mna tunaenda kufanya ibada na kuondoka

Ila makanisa m naona kma ni biashara flani hivi kwanini yalipe kodi wakati ni sehemu za ibada?

Anaejua atwambie
Kanisa gani linalolipa kodi?
 
Walichotakiwa kufanya serikali ni kujibu hoja za Gwajiba lakini kuchinda kujibu na kukimbilia mambo ya ajabu ni wazi kuwa:
Serikali inahusika au inajua hawa wanaoteka na kuua watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…