Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Yakiwa mekundu umeumizwa mno!
Yakiwa manene kwisha khabari kabisa!
Yakiwa yamepasuka katikati miguno!
Yakiwa zambarau wahoji waficha nini!
Yakiwa ndani ya "lip-bum" maswali kibao!
Hivi mashavu ya mdomo yaashiria nini?
Shavu la mdomo wa chini sasa gumzo!
Eti mpingo tii yawaje awe nalo jekundu?
Ati hiyo ni dalili maini na figo zimeliwa!
Sijui huyo tabibu mahiri wamemtoa wapi?
Bado napekuwa vitabu kujua ukweli wake!
Hivi mashavu ya mdomo yaashiria nini?
Kwa mustakabali huu, kunyanyapaana sera!
kwa mustakabali huu, chuki kuongezeka sana!
Kwa mustakabali huu, nani ni mzima basi?
Kwa mustakabali huu, maambukizi kudumishwa!
Kwa mustakabali huu, usalama sasa uko wapi?
Hivi mashavu ya mdomo yaashiria nini?
Uso utasuguliwa kuficha majeraha.
Meno yatatakaswa kulinda fizi zote.
Ulimi utakwanguliwa kufukuza harufu.
Kigele cheupe kuchochewa na jiwe kali!
Mkorogo kufunika mengi bila zengwe!