Mashangingi ya CHADEMA!!

Mashangingi ya CHADEMA!!

Bora mmeyaeleza hayo magamba kwani kiakili huwa sio timamu kabisa.
 
Nakumbuka Slaa alitaja zaidi ya mara moja kuwa bei ya gari moja (hayo unayoyapigia kelele) ni zaidi ya shilingi milioni 200, je, kuna gari lolote CDM imelinunua kwa bei hiyo, ili hoja yako ipate uhalali wa kujadilika?

chadema ina kiwanda chake????
acha kudanganya watu,hawa jamaa wanaangalia maslahi hizo zingine ni sound tu
 
Kuna mh mmoja kaleta hoja kuhusu magari yanayotumiwa na baadhi ya viongozi wa CDM. Naomba nimfahamishe kuwa namba
1. Si lazima magari haya yawe ya chama, Sugu ana gari kama hilo nadhani kama sikosei na Halima pia.
Kwa gari la Mbowe na Dr inawezekana ni ya chama.
2.Magari haya hususani la Dr nimeyaona kwa karibu, haya si magari yaliyokuja mapya, ni 2nd hand za Dubai, Japan au UK. Kutoka UK unazeza kufikisha hilo gari hapa baada ya kodi kwa TZS 50 to 60m.
3.Magari kama hayo hayo ya serikali (nazungumzia VX wala sio VX/GX V8 za sasa) tunayopigiwa kelele ya mwaka 2004 yalikuwa yanagharimu TZS 145M hapo ni kwa serikali. Serikali inanunua mapya.

Elewa kwanini tunapiga kelele, ya kina Dr ni kama 60m wakati ya Serikali mwaka 2004 yalikuwa 145m. Haya ma vx/gx v8 ya sasa ndio itakuwa balaa, nadhani itakuwa kwenye 200m!
When you want to be frugal, usi ige matajiri.
Nikifikiri ingefaa hao unao watetea wangenunua corolla au Mark II na watafikapopote Nchi hii.
Hebu mweleze mkulimawa Arumeru million 60 in a sifuri ngapi mbele Yake.

Jamaa hawajashika serikali na matanuzi ndo hayo, wakishika serikali je?
 
Akili yako mbovu,chadema iliadress yale yanayonunuliwa kwa kodi za watz.kuelewa kugumu sana ndgu yangu...kiazi

Safi sana ndugu yangu,unajua mijitu mingine ni ya kuyaombea kwa Mumgu yapewe weledi wa kuelewa mambo ya msingi.TUAMKE WATZ JAMANI.
 
posho matokeo ni yale yale,ni zitto tu ndio hachukui posho huko chadema,kiongozi wa upinzani bungeni ndio kiongozi wa kuchukua posho za kukaa kitako pale bungeni pia!

Tundu Lissu, yeye uwa anasema wanamuwekea kwenye Account yake lakini hataki.
 
CHADEMA ilitoa hoja za msingi sana wakati wa Kampeni za Mwaka 2010 na zikakubalika na wananchi wa Tanzania.

Mgombea Urais wakati huo MH: Willbroad Peter Slaa na wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge walikuwa wanatoa tuhuma kwamba serikali iliyopo madarakani inafuja fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari aina ya Land Cruiser VX na V8 wakati fedha hizo zingetumika vizuri zingeleta maendeleo kwa wananchi. Katika kukoleza hoja hiyo ikaaminishwa kwamba kama CHADEMA ikishika madaraka basi magari hayo ya kifahari yatauzwa na madala yake yatanunuliwa magari madogo ya bei rahisi.

Slaa alikuwa anasema aina ya magari yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya na Mikoa thamani yake ni sawa sawa na gari moja kujenga Zahanati Nne vijijini. Wanachi waliambiwa kwamba magari hayo yatauzwa na fedha itakayopatikana itatumika kuwekeza kwenye Elimu.

Baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA hawatumii VX au V8 kwa matumizi ya kichama na yao binafsi, au thamani ya magari hayo imeshuka baada ya wao kuanza kuyatumia?

UKIKEREKA SEMA UPENDAVYO!!

Sijaelewa unataka nini ndugu yangu,ila tatizo niserikali iliyopo madarakani na watanzania walio irudisha tena madarakani.Kama uliwachagua hao magamba basi na wewe ni sehemu ya tatizo. Over
 
Hoja hujibiwa kwa hoja za si matusi na kejeli
Kama mtu kauliza hoja nyepesi basi ijibu kwa weledi hadi mleta hoja ajione kachemka na si kejeli na matusi
 
Mimi wakati mwingine huwa siwaelewi watanzania. Wao wanadhani ukweli ni lile jambo unalolipenda au kulikubali.

Kuna watu wanadai kwamba wameshindwa kunielewa lakini hata mimi sielewi kwa nini hawa nielewi kwa swali dogko kama hili. Nianze na hoja ya nini maana ya mkopo. wote tunajua kwamba mkopo ni dhamana anayopewa mtu na anatakiwa kuirudisha wakati maalum uliochaguliwa unapofika.

Lakini mkopo wa fedha walizopewa wabunge kununulia magari ni fedha zinazotokana na Kodi za watanzania. Na makato watakayokatwa ili kuulipa mkopo huo ni kutokana na Kodi za Watanzania. Kwa hiyo tofauti ya fedha zinazotumika kununulia magari ya serikali na zile zinazotolewa kama mkopo kwa wabunge haipo kwani zote zinatoka kwenye fuko moja,ambalo ni Hazina ya serikali kwa chanzo kile kile TRA.

Kama wabunge wangetumia fedha zao binafsi au za mishahara yao baada ya kujikusuru basi bila ya shaka hoja yangu hii ingekosa mashiko. kwa waislamu nguruwe ni haramu bila ya kujali kama nguruwe huyo amechinjwa au aliuliwa kwa rungu. Hao wanaowatetea wabunge wa CHADEMA watuambie basi mtu kama Silinde anamiliki aina gani ya gari na kama gari lenyewe amelipata kwa fedha gani kama si kwa kodi zetu?

Kuna wengine wamekwenda mbali zaidi kwa kutuambia kwamba wabunge wa CHADEMA hawamiliki magari haya ya kifahari, watu hawa wahasemi UKWELI. Na ni kujidharau kudhani kwamba kila anayesema kitu cha kuikosoa CHADEMA si mwana CHADEMA. Wengi tunashangilia sana kauli ya Mwalimu aliposema "CCM si mama yangu" lakini leo Zitto Kabwe akisema "CHADEMA si mama yangu" sijui kitampata nini??

Kuna watu wanataka kila KINYWA KIKIRI kwamba CHADEMA ni chama KITAKATIFU na kimeshushwa na MUNGU kwa makusudi MAALUM na kinaongozwa na MALAIKA toka MBINGUNI!!
 
Kaka kuna vitu unavisukimia chini ya kapeti na napata hofu kuwa unafanya hivyo kwa makusudi kabisa.
1. Si sahihi kulinganisha magari yaliyopigiwa kelele na CDM na magari wanayotumia viongozi wa CDM kwa sasa.
2. Chanzo cha fedha za kununulia magari hayo.

Kusema viongozi wa CDM ni wanafiki vile wanaendesha magari ya 60m na wao walipigia kelele magari ambayo then yaliigharim serikali 150m unalinganisha vitu viwili tofauti kabisa na unajua hutendi haki. Kumbuka hiyo ni zamani haya ya sasa ni more than 200m!

Hoja ingekuwa kama ni sawa kwa wabunge kutumia magari yanayogharimu 60m na je mishahara ya wabunge na posho zao zinazowawezesha kukopa na kulipa magari ya thamani hiyo ni haki? Je wabunge kuendesha magari ya 60m wamejitoa toka daraja la wananchi wa kawaida? Kama serikali ingenunua magari ya 60m tungeokoa 90m kwenye kila gari hapo nyuma, kama viongozi wetu wangetumia shangingi kama la Sugu ikilinganishwa na bei ya haya ya sasa tungeokoa at least 110m kwa kila gari!
 
MBOWE anatumia gari la kiongozi wa upinzani bungeni (KU) aina ya Land cruser V8 alilotangaza kurudisha bungeni na kweli alirudisha lakini kalichukua kimya kimya bila kutuambia ameamua kulichukua......siasa bana.

Dk. Slaa anadaiwa kulipwa mshahara zadi ya milioni 7 kwa mwezi ambao unazidi mshahara wa mbunge.

Tukipata maelezo yao dhidi ya tuhuma hizi itapendeza.
Subiri mitusi yao maana hawapendi kuambiwa vitu kama hivyo.Ngoja tuone!!
 
Hoja yangu inatokana na maneno ya viongozi wa CHADEMA wakati wa kugombea mwaka 2010 na si vinginevyo.

Kati ya watu wanaopinga matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi mimi ni mmoja wao. Kuna watu wanataka tuamini kwamba wabunge wanatumia fedha zao "binafsi" lakini hawatuambii kama hizo fedha zao "binafsi' wamezipata kwa kufanya biashara gani au fedha hizo zinatokana na wao kuwa wabunge na kodi zetu sisi watanzania.

Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA walikuwa na mawazo ya kuanzisha Pool kwa ajili ya magari ya serikali halafu kwa Dar es salaam watendaji wa serikali wangetumia "saloon". Lakini ni wabunge wangapi wa CHADEMA wanatumia Saloon kama magari yao ya kikazi?
 
Kuna watu wanataka kila KINYWA KIKIRI kwamba CHADEMA ni chama KITAKATIFU na kimeshushwa na MUNGU kwa makusudi MAALUM na kinaongozwa na MALAIKA toka MBINGUNI!!

Kauli nzito sana hii
Kama una ubongo wa kondoo huwezi kuielewa katu.......
 
Mada kama hii ni ya kitoto sana!!
Ambapo ukimpa mtoto mmoja wa CDM ambae ni sawa na 8 vya gambas anakuchambulia ndani ya 5min na wote mtarizika,,,,,,,,,
 
Hivi magari yanayotumiwa na CHADEMA ni ya pesa binafsi au ruzuku, Misaada toka kwa SABODO na zile zilizochangishwa kwa bakuli kusaidia kampeni? Nafikiri kama ndizo hizo, basi nazo ni kodi za wananchi au mnasemaje wadau wenzangu?

Kuna kitu mkuu unakichanganya. Kama unauliza magari ya chama mengi ni vitara rena vitara zilizochoka kwelikweli. Najua Heche anatumia Nissan Patrol lakini nayo imechoka na ni kuu kuu kupita maelezo. Kama unamaanisha magari binafsi ya wabunge wa chadema hapo utakuwa unachanganya desa. Mbunge anakopeshwa na bank na dhamana yake ni mshahara na posho zake. Akifukuzwa ubunge mkataba wa mbunge husika na Bank iliyomkopesha utaamua alipeje. Na tatizo hapa sio mbunge kukopa pesa kununua V8, tatizo ni posho zinazomfanya awe na uwezo huo kwa sababu Mshahara wa Mbunge ni less than 2M kwa Mwezi, ambao hauwezi kumpa sifa ya kukopa 90M kwa miaka mitano, lakini miposho imezidi. Sasa hapo ndipo utakapokuja kuwakumbuka CDM waliokuwa wanapiga kelele posho zitolewe. Zikitolewa posho hata wabunge wa CCM watashindwa kununua V8 binafsi wataishia kununua Starlet tu
 
In other way arround........You got a point in here dude.............
 
When you want to be frugal, usi ige matajiri.
Nikifikiri ingefaa hao unao watetea wangenunua corolla au Mark II na watafikapopote Nchi hii.
Hebu mweleze mkulimawa Arumeru million 60 in a sifuri ngapi mbele Yake.

Jamaa hawajashika serikali na matanuzi ndo hayo, wakishika serikali je?

Mkuu lazima utakuwa na mtindio wa akili, yaan uwezi fikiri hata kidogo, kwenye 145m kuna 60 ngapi? au kwenye 200m ya vx/Gx v8 kuna 60 ngapi? 3 na kuenelea, hivo ni economical.

Pia hata wakikubali kununua corrola utamambia kwa nn wasinunue pikipiki? na wakinunua pikipiki utambia wana2mia pesa vibaya, kwa nn wasinunue baiskeli na mwendelezo unakuwa hivo.
 
Kuna kitu mkuu unakichanganya. Kama unauliza magari ya chama mengi ni vitara rena vitara zilizochoka kwelikweli. Najua Heche anatumia Nissan Patrol lakini nayo imechoka na ni kuu kuu kupita maelezo. Kama unamaanisha magari binafsi ya wabunge wa chadema hapo utakuwa unachanganya desa. Mbunge anakopeshwa na bank na dhamana yake ni mshahara na posho zake. Akifukuzwa ubunge mkataba wa mbunge husika na Bank iliyomkopesha utaamua alipeje. Na tatizo hapa sio mbunge kukopa pesa kununua V8, tatizo ni posho zinazomfanya awe na uwezo huo kwa sababu Mshahara wa Mbunge ni less than 2M kwa Mwezi, ambao hauwezi kumpa sifa ya kukopa 90M kwa miaka mitano, lakini miposho imezidi. Sasa hapo ndipo utakapokuja kuwakumbuka CDM waliokuwa wanapiga kelele posho zitolewe. Zikitolewa posho hata wabunge wa CCM watashindwa kununua V8 binafsi wataishia kununua Starlet tu

Ebu fafanua vizuri wabunge wamekopeshwa na bunge milioni 90 kwa manunuzi ya magari yao sio benki...halafu hapo hapo wabunge wamekopa benki mikopo binafsi na mdhamini wao ni bunge, kuna wengine wamekopa milioni 30 wengine milioni 50 na malipo yao kwenye mikopo yao inatoka na kodi zetu, nikirudi kwenye hoja ya Kigarama, mbunge wa Chadema ambae anatembelea gari la bei ndogo ni John Mnyika, Toyota Vitz.
 
jaman mi naombeni mnijuze tu.ina maana chadema haina mapungufu hata kdogo?
 
Back
Top Bottom