Mashangingi ya CHADEMA!!

Mashangingi ya CHADEMA!!

Ni vema kijadili vitu vya ukweli kuliko kuleta ushabiki usio na tija. Kama kweli mboye kalichukua gari la kiongozi wa upinzani bungeni basi atakuwa amewaadaa wana CDM wenzake. Nasikia mpaka posho wanasaini kuzichukua kimya kimya nyinyi wana CDM wengine mnadanganywa wala hamjielewi. Bado miaka 3 kabla ya uchaguzi mpaka leo hakuna hata halimashauri moja iliyo chini ya CDM inayotoa elimu bure sijui mtawaambia nini wananchi mwaka 2015.
 
jaman mi naombeni mnijuze tu.ina maana chadema haina mapungufu hata kdogo?
Hilo swali ndilo wengine tunajaribu kulijibu kwa kuonyesha mapungufu ya CHADEMA. Tatizo mashabiki wengi wa CHADEMA siasa walianza mwaka 2010 wakati Slaa akiwa mgombea Urais. Wao macho yao yote yako 2015 bila ya kujali baada ya 2015 kwa CHADEMA hii kitatokea nini.
 
Ebu fafanua vizuri wabunge wamekopeshwa na bunge milioni 90 kwa manunuzi ya magari yao sio benki...halafu hapo hapo wabunge wamekopa benki mikopo binafsi na mdhamini wao ni bunge, kuna wengine wamekopa milioni 30 wengine milioni 50 na malipo yao kwenye mikopo yao inatoka na kodi zetu, nikirudi kwenye hoja ya Kigarama, mbunge wa Chadema ambae anatembelea gari la bei ndogo ni John Mnyika, Toyota Vitz.

Hapo kwenye red, hivi kuna mbunge ambaye analipiwa marejesho ya mkopo (loan instalments) kwa fedha za walipa kodi ??
Duh !!, JF kuna kazi kweli kweli.
 
Ukipinga matumizi ya magari ya kifahari kwa watumishi serikalini, unakataza pia matumizi ya magari hayo kwa matumizi ya watumishi hao isipokuwa kwa ambao siyo watumishi. Sasa kama cdm waliyapinga halafu leo ndo wanayatumia si usaliti? Naonga mkono hoja
 
Ni vema kijadili vitu vya ukweli kuliko kuleta ushabiki usio na tija. Kama kweli mboye kalichukua gari la kiongozi wa upinzani bungeni basi atakuwa amewaadaa wana CDM wenzake. Nasikia mpaka posho wanasaini kuzichukua kimya kimya nyinyi wana CDM wengine mnadanganywa wala hamjielewi. Bado miaka 3 kabla ya uchaguzi mpaka leo hakuna hata halimashauri moja iliyo chini ya CDM inayotoa elimu bure sijui mtawaambia nini wananchi mwaka 2015.

Kwani Chadema ndio inaongoza nchi ?
 
Jimbo la Iringa mjini ni miongoni mwa majimbo yatakayorudi CCM
 
Ndugu Wana JF,

Ninapenda kuwashauri mtu anapoleta hoja yake hapa kwanza tuitafakari na kuielewa,ndio tuanze kutoa maoni yetu.

Kwanza nianze kwa kusema Mimi ni Mtanzania,lakini mimi sio mwanachama wa chama chochote,nimeona kwanza nionyeshe msimamo wangu,mimi sio CCM wala si CHADEMA.Ni kweli tumeona uozo wa CCM lakini hata hawa watawala watarajiwa walisema kwamba wao hawata tumia haya Ma v8,kama kweli ni watu wenye nia njema hili wangelifanya tungewaamini zaidi,Naunga hoja iliyotolewa hapo juu,kukosoa au kukosolewa ni sehemu ya UWAJIBIKAJI,vingine mimi ninasema hatuna wawakilishi wa wananchi,hakuna anayejaliwa matatizo ya wananchi awe ni mwana CCM au CHADEMA,kila mtu anatafuta kula yake,kwa hiyo usidanganyike hata wakichukua CHADEMA nchi wataleta ASALI NA MAZIWA,kiongozi mzuri unamjua pale anapotekeleza yale aliyosema kwenye kampeni zake za kutafuta kura,Vinginevyo CHADEMA ni CCM - B,au ni wale wale,Mapinduzi ya kweli katika nchi kwanza yanaanzia kwenye Mawazo na kuwa na Uchungu na walala hoi,yaani WANYONGE,lakini hawa wenzetu yaani CCM na CHADEMA wanakuwa na uchungu na wananchi wanapotafuta kura.Hizi siasa zimepitwa na wakati,Mtu akitaka uongozi tumuulize atatufanyia nini wananchi na sio ahadi hewa,na atatoa hizo fedha wapi za kutuendeleza,ingekuwa ahadi ndio maendeleo,Tanzania tungekuwa mbali.
 
Mkuu lazima utakuwa na mtindio wa akili, yaan uwezi fikiri hata kidogo, kwenye 145m kuna 60 ngapi? au kwenye 200m ya vx/Gx v8 kuna 60 ngapi? 3 na kuenelea, hivo ni economical.

Pia hata wakikubali kununua corrola utamambia kwa nn wasinunue pikipiki? na wakinunua pikipiki utambia wana2mia pesa vibaya, kwa nn wasinunue baiskeli na mwendelezo unakuwa hivo.

Ndugu yangu, sitaingia katika mkumbo wa ku-argue kama lumpen proletariat, mtu ambaye shule ilimpitia kwa mbali.
Swala nililoliweka hapo wala hujalielwa, kama ambavyo mkulima wa Arumeru hataelewa kuwa katika milioni 60 kuna sifuri ngapi.
Na hapo ndio unafiki wa wazi utakuwa peupe kwa kila mtu kuona ukweli.
Shangingi ni shangingi tu, na kwa mawazo ya mtu anyependa shangingi akiingia madarakani atanunua LC200, hiyo ni argument yangu.
Kwa vile hukuelewa , basi uelewe hivyo, bila kujijua kuwa actually mtindio unaozungumzia ni ule wa wewe kushindwa kuelewa a simple and logical argument.
Ni pole tu.
 
Hapo kwenye red, hivi kuna mbunge ambaye analipiwa marejesho ya mkopo (loan instalments) kwa fedha za walipa kodi ??
Duh !!, JF kuna kazi kweli kweli.

Nisome vizuri au inawezekana umerukia usichokijua...hao ulipo bold posho, mishahara, na viinua mgongo vya wabunge ni kodi zetu, sijui kama unafahamu mbunge akimaliza kipindi chake bunge anapewa zaidi ya milioni 40? Unadhani zinatoka wapi.
 
Nadhani mleta uzi anatkiwa kufikiri zaidi. Hili suala la mashangingi ni la kimfumo zaidi na serikali ya CCM ndiyo iko madarakani suala la wabunge wa CDM ooh Vx halina maana yoyote ni suala kama la posho, kama CDM walikuwa wanazipinga na leo zinawekwa kwenye akaunti zao wakulaumiwa nani?
 
Nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa Kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya CHADEMA yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata Baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.

Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi Milioni 90 na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?

Nakuunga mkono pia kuwa hayo Mashangingi yananunuliwa kwa fedha wanayopewa RUZUKU wanayopokea kila mwezi kutoka Serikalini na ni kODI YA WANAINCHI WOTE WA TANZANIA hivyo Chadema kama Chama wameacha jambo ambalo waliwaaminisha Watanzania kuwa watalitekeleza na si mpaka wapate madaraka ya Uraisi ndo maana hawa jamaa wa magwandwa mimi huwa si waamini sana mambo yao wanayosema wakiwa majukwaani wakati wa kuomba kura!
 
Kweli watu wagumu kuelewa. Mtu kasema akishika nchi ndio atakataza vx na v8. Leo hajashika bado watu wanashikilia kauli.
 
Nisome vizuri au inawezekana umerukia usichokijua...hao ulipo bold posho, mishahara, na viinua mgongo vya wabunge ni kodi zetu, sijui kama unafahamu mbunge akimaliza kipindi chake bunge anapewa zaidi ya milioni 40? Unadhani zinatoka wapi.

Yaani mpaka nakuhurumia jinsi unavyotoa 'hoja'.
Iko hivi:-
Mshahara, posho, viinua mgongo, etc. ni malipo ya kazi ya Ubunge. Hivyo ni kama malipo yoyote ya mishahara ya wafanyakazi wowote wengine.
Hivyo, mpokeaji mshahara ana uhuru wa kutumia mshahara wake vyovyote anavyopenda (bila ya kujali pesa za kulipa mshahara zinatoka wapi), yaani kununua fenicha, kununua gari, kulipia marejesho ya mkopo, etc.
Kwa hiyo, unachosema wewe ni kwamba wabunge hawana uhuru wa kutumia mishahara yao wapendavyo !!! Yaani wakitumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo, inakuwa issue !!!
Jiulize, wafanyakazi wa serikali huwa wanakopa?? Hivi wakikopa, wanaruhusiwa kutumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo ??
Kwa wewe, ungesema wasitumie mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo maana, hiyo mishahara yao ni pesa zetu za kodi !!!
 
Kweli watu wagumu kuelewa. Mtu kasema akishika nchi ndio atakataza vx na v8. Leo hajashika bado watu wanashikilia kauli.
Mkuu Acha hadithi za sungura.

Sungura(CDM) alisema, mkiniingiza shamba la zabibu( mkinipa Nchi), nikakula zabibu mbichi tu Kama Nina njaa(CDM hatanunua mashangingi).
Leo tu CDM wanakula zabibu za jana( mashangingi yaliyozeeka), wakipata nchi we fikiria mwenyewe itakuwaje,watakula zabibu za jana au za Leo leo?
 
Acha kufikiria kwa kutumia ma***** huko vijijini utaenda na Corolla au GX 100?

Naona uwezo wako wa kuchallenge ni mdogo. Unafikiri kijijini ni VX na V8 Landcruiser ndio gari nzuri za kwenda huko? Mbona kuna gari nzuri kama RAV4, Hilux Puck double cabbin, Isuzu wagon, Tata 4W, na nyingine nyingi. hata serikali ina uwezo wa kuoda aina ya magari inayotaka.
 
CHADEMA ilitoa hoja za msingi sana wakati wa Kampeni za Mwaka 2010 na zikakubalika na wananchi wa Tanzania.

Mgombea Urais wakati huo MH: Willbroad Peter Slaa na wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge walikuwa wanatoa tuhuma kwamba serikali iliyopo madarakani inafuja fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari aina ya Land Cruiser VX na V8 wakati fedha hizo zingetumika vizuri zingeleta maendeleo kwa wananchi. Katika kukoleza hoja hiyo ikaaminishwa kwamba kama CHADEMA ikishika madaraka basi magari hayo ya kifahari yatauzwa na madala yake yatanunuliwa magari madogo ya bei rahisi.

Slaa alikuwa anasema aina ya magari yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya na Mikoa thamani yake ni sawa sawa na gari moja kujenga Zahanati Nne vijijini. Wanachi waliambiwa kwamba magari hayo yatauzwa na fedha itakayopatikana itatumika kuwekeza kwenye Elimu.

Baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA hawatumii VX au V8 kwa matumizi ya kichama na yao binafsi, au thamani ya magari hayo imeshuka baada ya wao kuanza kuyatumia?

UKIKEREKA SEMA UPENDAVYO!!

Kwa hiyo wewe kilichokuuma ni kuwaona wabunge wa Chadema wanatumia ma v8 ama vx ?
 
Yaani mpaka nakuhurumia jinsi unavyotoa 'hoja'.
Iko hivi:-
Mshahara, posho, viinua mgongo, etc. ni malipo ya kazi ya Ubunge. Hivyo ni kama malipo yoyote ya mishahara ya wafanyakazi wowote wengine.
Hivyo, mpokeaji mshahara ana uhuru wa kutumia mshahara wake vyovyote anavyopenda (bila ya kujali pesa za kulipa mshahara zinatoka wapi), yaani kununua fenicha, kununua gari, kulipia marejesho ya mkopo, etc.
Kwa hiyo, unachosema wewe ni kwamba wabunge hawana uhuru wa kutumia mishahara yao wapendavyo !!! Yaani wakitumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo, inakuwa issue !!!
Jiulize, wafanyakazi wa serikali huwa wanakopa?? Hivi wakikopa, wanaruhusiwa kutumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo ??
Kwa wewe, ungesema wasitumie mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo maana, hiyo mishahara yao ni pesa zetu za kodi !!!

Mbona ueleweki ulichoandika mkuu, nadhani ungejikita zaidi kwenye kubold tu mkuu wangu ndicho unachofahmu.
 
Mkuu Acha hadithi za sungura.

Sungura(CDM) alisema, mkiniingiza shamba la zabibu( mkinipa Nchi), nikakula zabibu mbichi tu Kama Nina njaa(CDM hatanunua mashangingi).
Leo tu CDM wanakula zabibu za jana( mashangingi yaliyozeeka), wakipata nchi we fikiria mwenyewe itakuwaje,watakula zabibu za jana au za Leo leo?

hesabu yako imekaaje mimi navyo elewa siku kabla ya jana ni juzi,halafu nashukuru kwa utabiri wako kwamba umetambuwa kuwa wataongoza nchi.... watakuweje ..jibu subiri uone kwani kwa sasa kila mtu ananunuwa kivyake hana masharti yeyote hata akitaka kuwa na helkopta kama ndesa ni juu yake mafuta na spea dereva anakolipaki kila kitu atajuwa mwenyewe....
subiri uone wacha umbea kwa sasa hawajashika nchi

wewe ni bogas kabisa ni sawa na masaburi unashindwa hata kutofautisha kitu kinachonunuliwa na kodi za watanzania wavuja jasho na zinazo2miwa na CDM au kodi inalipwa kwa CDM ckuiz?kama ni kweli 2tasema wana2mia vibaya mali ya uma lakini km c hivyo hebu nenda kafikiri vizuri.
 
hesabu yako imekaaje mimi navyo elewa siku kabla ya jana ni juzi,halafu nashukuru kwa utabiri wako kwamba umetambuwa kuwa wataongoza nchi.... watakuweje ..jibu subiri uone kwani kwa sasa kila mtu ananunuwa kivyake hana masharti yeyote hata akitaka kuwa na helkopta kama ndesa ni juu yake mafuta na spea dereva anakolipaki kila kitu atajuwa mwenyewe....
subiri uone wacha umbea kwa sasa hawajashika nchi
Another lumpen ploetariat, mtu ambaye hajui kwamba serikali inaendeshwa na taratibu zilizowekwa na kuwa gazetted.
Huamki leo na kusema lile lilomo moyoni bila kufuata taratibu.
Na hilo ndio weakness kubwa ya CDM.
Mtupatie sera zenu za kiuchumi, elimu,biashara na itikadi yake ili tuweze kuwaelewa.
Sera ya kupunguza matumizi ya serikali ni muafaka , lakini imetayarishwaje?
 
Back
Top Bottom