Mashangingi ya CHADEMA!!

Kwanza nikuulize. Hivi usingeweza kujenga hoja yako ya kuipinga hoja yangu bila ya kuandika hilo neno nililoli-bold?

Wengi wa walioipinga hoja yangu wameongea kama vile mimi sielewi nani anakusanya kodi na serikali inatumiaje kodi inayokusanya. Kiuhalisia serikali kukusanya kodi na kuigawanya kwa matumizi ya serikali ni mambo mawili tofauti. Kodi inayotumika kulipa wafanyakazi wa kufagia maofisi ya serikali ndiyo hiyo hiyo inayotumika katika kulipa posho wabunge na mawaziri wa serikali. Hakuna Kodi inayokusanywa maalum kwa ajili kuwalipa wabunge marupurupu yao.

Hoja yangu hapa ni ya kimaadili. Mtu mkweli utamtambua kwa matendo yake, ndiyo maana nasema nguruwe akiuzwa uswahilini au super market wote ni nguruwe na bado watakuwa ni haramu kwa waislamu na wasabato. Kama wao CHADEMA walisema matumizi ya mashangingi ni hasara kwa serikali basi wangeonyesha kwa vitendo kwa.

Nimetoa mfano wa baadhi ya wabunge ambao kwa hakika walikuwa hawana hata uwezo wa kununua Baiskeli lakini leo wanamiliki VX kama vyombo vyao vya usafiri. Makadirio ya kuwapa wabunge mafuta yanatokana na aina ya magari ambayo wabunge wengi wanatumia. kama wabunge wengi wa CHADEMA wangekuwa na magari mdogo yanayotumia mafuta kidogo ni pesa ngapi za walipa kodi zingeokolewa kwa wabunge hao kutumia magari ya "kawaida"?

Sisi ambao tunafika kwenye viwanja vya bunge mara kwa mara tunajua siyo tu wabunge wa CCM hata wabunge CHADEMA nao huwa hawaji na magari yao DODOMA lakini bado tu wanachukua na posho ya kuyahudumia magari yao wakiwa DODOMA.

Chadema haina serikali magari wanapewa tu na bunge.
So ku put blame on them ni ujinga.
 
Si alikopa milioni 90 kununua gari wakati alivyokuwa mbunge sasa hivi siyo mbunge ndio maana nimeuliza karudisha?

Unachohoji ni kama atamalizia kulipa mkopo au kurudisha gari? Watanzania wa namna yako ya kufikiri ndio wanafanya nchi hii iendelee kuwa maskini.
 
Bla bla nyingi za nini?
Nasisitiza CDM watoe sera za jinsi ya kuendesha serikali kwa tija inayotokana na kupunguza matumizi ya uendeshaji.

Bla bla hizi Kama hapo juu zinaonyesha kuwa ni kazi rahisi sana kulaumu tu kuliko kutengeneza mipango mbadala yenye tija na matumizi nafuu kwa serikali.
Kwa mapana Yake matumizi yasiyo na tija serikalini haitokani na mashangingi na posho tu.
CDM itabidi wafanye utafiti wa kutosha kabla ya kujikita katika petty issues.

Hiyo sera wakishaitoa wanaifanyia nini ikiwa serikali inaongozwa na CCM? Wewe unayeona magari ya serikali ni petty issues ni kwa kutokujua kwako namna yanavyotumiwa vibaya na namna yanavyoigharimu serikali kwenye service.

Kama hizo uliziona ni blah blah basi hakuna maneno utakayoambiwa zaidi ya hayo ukayaona yana maana kwako. Tatizo lako ni kuamua kuishi kwa mazoea kwa kuwa una imani kuwa kuishi kwa kufikiri ni gharama.
 
Hiyo sera wakishaitoa wanaifanyia nini ikiwa serikali inaongozwa na CCM? Wewe unayeona magari ya serikali ni petty issues ni kwa kutokujua kwako namna yanavyotumiwa vibaya na namna yanavyoigharimu serikali kwenye service.

Kama hizo uliziona ni blah blah basi hakuna maneno utakayoambiwa zaidi ya hayo ukayaona yana maana kwako. Tatizo lako ni kuamua kuishi kwa mazoea kwa kuwa una imani kuwa kuishi kwa kufikiri ni gharama.

Mkuu unakaugonjwa kanakoitwa chademaosis changiuim fever, kaugonjwa ka kutaka mabadiliko kwa gharama yoyote bila kujua unakoelekea.

Actually si vibaya kutaka mabadiliko maana ndiyo tabia ya binadamu, akini mabadiliko for its own sake inabidi uwe reckless kutaka hayo mabadiliko yasiyojulikana.
Chama chako hakijaonyesha ukomavu wa kututia moyo kuwa kinaweza kuendesha gari kubwa linaloitwa serikali ya JMT.
Kwamba gari haliendi vizuri, hilo ni muafaka , kila mtu anajua hilo, kubadili dereva? leseni yako bado haijaturidhisha.
Hatutaki kuishia mtaroni, mtaro wa kisiasa na kiuchumi.

Kama ni matumizi ya pesa basi tungeona mfano mzuri wa ile hela ya Sabodo, watu wanawapa hata wake zao tenda kwa milango ya nyuma!
Maskandali tele humu JF, wala haututaki kuzisikia zinaletwa na nyie wenyewe ndani ya chama chenu.

Pamoja na yote sioni kiongozi, nasema sioni kiongozi ndani ya chama chenu mwenye uwezo wa kutengeneza sera itakayoeleweka na wananchi wote Tanzania.
Kutoa lawama kwa sauti kali na kunyoosheana vidole, hilo hata mtu asiyeenda shule anaweza

Ukitaka kujua , leo tunafuata sera zilizo wekwa na Baba wa Taifa, hata kama zimechakachuliwa!
 
Back
Top Bottom