Mashabiki Yanga wamsindikiza Manji polisi

Choga Cosmasy

Member
Feb 8, 2017
18
32
Na
Cosmasy Choga

Siku moja baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutaja orodha ya watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya akiwemo mwenyekiti wa yanga Yusuph Manji mashabiki wa club hiyo tayari wameaza kuwasili kituo cha polisi kujua hatima ya kiongozi wao.

Watuhumiwa hao waliombwa kufika kituoni hapo kesho ijumaa lakini muda mfupi tu baada ya tamko hilo bwana yusuph manji alihitisha kikao na wandishi wa habari na kusema yeye ataenda leo kuripoti na sio ijumaa.

Baadhi ya mashabiki wa yanga baada ya kusikia hivyo tayari wamekwisha fika eneo hilo la polisi kutaka kujua yatakayo jili juu ya mwenyekiti wao.

Manji amekuwa akiisaidia club ya yanga katika kuhakikisha inafanya vyema kwenye mashindano pia ndio kiongozi wa juu wa timu.

Wachezaji wanena

Wachezaji wa yanga nao wameshituka kusikia hivyo na kila mchezaji akisema ya moyoni mwake juu ya boss wao

Mwenyekiti amekuwa akituasa kutotumia madawa ya kulevya kama tunataka kufanikiwa kisoka

Una maoni gani katika hili?
1486628554228.jpg
 
Tatizo kubwa la Watanzania mnataka mtu hasa mwenye hadhi kijamii adhalilike mkiwaza kwamba akidhalilika basi itakua sawa na wewe...haiwezekani milele...ni kwasabbu ya mawazo hayo potofu tumegeuka nchi ya majungu..fitina chuki na kutaftana kuanzia ngazi ya familia mpaka maofisni mpaka kwenye kila kitu..roho mbaya ya wivu inatuua..
 
.
Kibaya zaidi kuna baadhi ya viongozi washagundua huu udhaifu wa watanzania, wakishindwa ku -deliver au kutimiza ahadi zao hawaoni aibu kuwadhalilisha wenye majina/fanikiwa kiuchumi ili wawafurahishe masikini wengi waliowazunguka.
 
Back
Top Bottom