PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 10,518
- 23,009
Kwa haya matukio ya kuambatanisha shughuli za club na maisha ya nje na binafsi ya wachezaji na watu wa ndani ya Yanga. Huu upuuzi nimeona umeletwa kwa kasi sana.
Yanga ni Club inayojengwa kwa kwa jitihada za kila mdau. Ikimbukwe Yanga siyo kikundi cha wasanii wanaotaraji kuji brand kwa maisha yao binafsi na matukio ya kiki.
Kinachoendelea hivi sasa ni udharirishaji wa Club ambayo inatarajiwa iendelee kujijenga ndani na nje ya uwanja kupitia changamoto na mafanikio yake, lakini si kupitia mahusiano ya akina Aziz K na yule demu wake, wala si kupitia mahusiano ya Manara na dem wake, imefikia mahala hata camera za club kila wakati kumfuatilia Aziz K na demu wake ambaye anaonekana kuwa hana mipaka kwenye circles zote za club, si vyumba vya wachezaji, si viwanjani.
Anachokifanya Manara ni kutaka kuiweka Club kwenye makwapa ya watu fulani, hilo halipaswi kufumbiwa macho. Kuna watu wanataka kuifanya Yanga ionekane ina gain umaarufu na mafanikio kupitia wao while wale wanaoipa mafanikio wenyewe si waongeaji. Badala ya kuongelea mambo ya Yanga wao wanaleta mambo yao kwenye mambo ya Yanga.
Mchezaji au wachezaji huinuliwa na jitihada, nidhamu, mafanikio na mashabiki wao, lakini hiki cha mtu kutoka huko alikokuwa na kutaka kumtengeneza mchezaji fulani kwa kutumia rasilimali na majukwaa ya club Kujiinua yeye na awatakao halipaswi kuachwa.
Rai yangu kwa viongozi wa Yanga
Hongereni kwa mlipoweza kuifikisha timu, ila hampaswi kukumbatia watu aina ya Manara, huyo mnavyozidi kumuweka karibu atasababisha mivurugano ndani ya Club kuanzia wachezaji hadi viongozi.
Upande wa mashabiki na sisi wanachama huku hana chake sababu katu hawezi kutugawa, kwetu tunamchukulia kama mtafutaji ambaye mungu wake kamtengenezea mlo wake upatikane Yanga, sisi hatukuwahi kumhitaji wala kuona tija yake kwetu, kazi yake ndani ya Simba aliifanya vyema, hilo hatupingi. Hatukuona shida mfanye naye kazi sababu tunawaamini na tumewapa majukumu ya kufanya na wale mnaoona kuwa watawasaidieni, lakini kwa hili la Manara ushauri wangu binafsi mngejifikiria vizuri, maana mnajenga timu lakini Manara hajui kuishi kama sehemu ya timu, anataka kuwa juu ya timu si kwa jitihada na weledi, bali kwa fitina, chuki na kila ushenzi.