Mashabiki na wanachama wengi wa Chama cha Mapinduzi hawajui kujenga hoja, wamebaki tu kutukana Watu

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,682
3,065
Wasalaam,

Nimekuwa mfuatiliaji wa mambo ya siasa kwa muda mrefu sasa .

Lakini siku za hivi karibuni baada ya Mh Magufuli kuingia madarakani wana CCM wengi wameacha kujadili vitu na watu kwa hoja sasa ni kushambulia tu watu ama kwa kuwatishia kuwaua au kuwaangamiza wanavyojua.

Mathalani mnaweza kuwambia uwepo Mdahalo wa wagombee Urais watakwambia kwa kazi alifonya Magufuli hatakiwi kufanya mdahalo,ukimtupia tena swali basi asifanye campaign kwa vile kazi yake inaonekana anakosa hoja.

Kiukweli wana CCM wanaboa sana wanabaki kujivua kombati zao na ukivuli wa kuwa karibu na UT NA PT zaidi hawana jipya ni matusi tu.

Zamani ukutane na akina Mwakyembe,Selelii,Ole Sendeka wanapanga hoja wanapangua hoja .

Ila muda kuanzia mwenyekiti ,katibu Mwenezi wanapayukapayuka tu .

Muulize Mwenyekiti maswali majibu yake ni ya kudhalilisha tu akina mama na wanawake.

CCM mjirekebishe jingeni hoja jibuni hoja.

Kizazi hiki cha Leo sio cha 48 watu wamesoma watu wameelimika.

Mnaeda kudidimia kwa sababu nguvu za dola zitakuja kushindwa na nguvu za umma siku moja na mtafutikana Milele.

Msifikiri upinzani ni vyama upinzani ni wananchi
 
kiukweli wana ccm wana hoja na wanajua kuzipangilia ukiangalia kazi iliyofanyika na serikali ya awamu zote5 ni wazi kuwa ccm ndio imetufikisha hapa tulipo na kiukweli tumepiga hatua kubwa sana katika kila awamu katika kila nyanja, ila inawezekana wewe ulikutana na mwana CCM asie jua kupanga na kuelezea hoja mmoja ukaamua kujumuisha wote, ila amini nakueleza ukweli unao moyoni mwako wagombea wa vyama pinzani walio teuliwa kugombea uraisi awamu hii wote hawatoshi kuwa maraisi isopokuwa mh john pombe magufuli
 
Ukitaka kujua wamefikia pabaya, huko kwa waziri mkuu wagombea wa upinzani hasa cdm na ACT wametekwa na kupigwa vibaya sana ili apite bila kupingwa. Polisi wako kimya maana wanajua kinachoendelea.
Mmezoea kutafuta visingizio mbalimbali ili mkishindwa muwakamate wajinga kwa maneno ya uongo ili muandamane sasa hiyo nafasi haipo aiseh
 
Hata Arusha mgombea ubunge wa CCM katekwa na kupigwa polisi pia wako kimya
 
CCM ni kama ugonjwa wa busha ktk mwili wa mwanaume, ambapo vazi pekee la kusitiri nyeti zake ni msuli ama kanzu, yaani kubebwa kwa hila ama mbeleko ya vyombo vya dola.
 
Mmezoea kutafuta visingizio mbalimbali ili mkishindwa muwakamate wajinga kwa maneno ya uongo ili muandamane sasa hiyo nafasi haipo aiseh

Sent from my SM-A320FL using JamiiForums mobile app

Hatukosei tunachosema boss. Hizi tabia za chama kilichoko madarakani kufanya unyama kisha kukimbia hadharani kupoteza ukweli, ni mbinu zilizokuwa zinafanyika huko ulaya mashariki. Mbinu hizo zimeigwa na viongozi wengi wa kiafrika madictator, na sasa ziko rasmi hapa nchini. Tabia hizi hufikia kikomo tu iwapo wananchi wataondokana na woga na kuamua kuchukua hatua, na kisha jeshi liwe upande wa wananchi na sio upande wa matumbo yao. Uzuri haya yanayotokea sasa tunatunza rekodi, muda ukifika tutasoma file la kila mmoja.
 
Mimi hata sijibizani nao maana wakikujua watakutafutia msala na kwakuwa mwenyekiti wao ni mbaguzi anaweza kunifukuza kazi. Hawachelewi kukukomoa hao nzi wa chooni. Wakimbie kama alivyokimbia Yusuf Manji
 
CCM ni kama ugonjwa wa busha ktk mwili wa mwanaume, ambapo vazi pekee la kusitiri nyeti zake ni msuli ama kanzu, yaani kubebwa kwa hila ama mbeleko ya vyombo vya dola.
Ukiondoa vyombo vya dola CCM ni chama kikubwa sana hapa mchini huenda ata babayako ni mwanachama wa CCM uwezi kukiondoa kwa maneno ya kihuni huni au kwa mambo yasio na maana, zaidi itapendeza ukiendelea kutoa mchango wako mzuri kwa viongozi ili tusaidie kuijenga nchi kwa pamoja

Sent from my SM-A320FL using JamiiForums mobile app
 
Wasalaam
Nimekuwa mfuatiliaji wa mambo ya siasa kwa muda mrefu sasa .
Lakini siku za hivi karibuni baada ya Mh Magufuli kuingia madarakani wana CCM wengi wameacha kujadili vitu na watu kwa hoja sasa ni kushambulia tu watu ama kwa kuwatishia kuwaua au kuwaangamiza wanavyojua.
Mathalani mnaweza kuwambia uwepo Mdahalo wa wagombee Uraisi watakwambia kwa kazi alifonya Magufuli hatakiwi kufanya mdahalo,ukimtupia tena swali basi asifanye campaign kwa vile kazi yake inaonekana anakosa hoja.

Kiukweli wana CCM wanaboa sana wanabaki kujivua kombati zao na ukivuli wa kuwa karibu na UT NA PT zaidi hawana jipya ni matusi tu.

Zamani ukutane na akina Mwakyembe,Selelii,Ole Sendeka wanapanga hoja wanapangua hoja .
Ila muda kuanzia mwenyekiti ,katibu Mwenezi wanapayukapayuka tu .

Muulize Mwenyekiti maswali majibu yake ni ya kudhalilisha tu akina mama na wanawake.

CCM mjirekebishe jingeni hoja jibuni hoja.
Kizazi hiki cha Leo sio cha 48 watu wamesoma watu wameelimika.
Mnaeda kudidimia kwa sababu nguvu za dola zitakuja kushindwa na nguvu za umma siku moja na mtafutikana Milele.
Msifikiri upinzani ni vyama upinzani ni wananchi
Kada yeyote ukimtoa nje ya
Sgr
Stigla
Madaraja
Mandege ya bombadia

Huwa hawana kingine cha kusema.
 
Hatukosei tunachosema boss. Hizi tabia za chama kilichoko madarakani kufanya unyama kisha kukimbia hadharani kupoteza ukweli, ni mbinu zilizokuwa zinafanyika huko ulaya mashariki. Mbinu hizo zimeigwa na viongozi wengi wa kiafrika madictator, na sasa ziko rasmi hapa nchini. Tabia hizi hufikia kikomo tu iwapo wananchi wataondokana na woga na kuamua kuchukua hatua, na kisha jeshi liwe upande wa wananchi na sio upande wa matumbo yao. Uzuri haya yanayotokea sasa tunatunza rekodi, muda ukifika tutasoma file la kila mmoja.
Wachaaah kwaiyo jeshi liwe upande wa wananchi mala ngapi au wanajeshi ni akina nani si ni hao tunaishi nao mitaani na wengine ni ndugu zetu sasa unasemaje wawe upande wa wananchi ikiwa wao wenyewe ni wananchi, acheni maneno ya porojo ya kupotosha umma jamani

Sent from my SM-A320FL using JamiiForums mobile app
 
Kada yeyote ukimtoa nje ya
Sgr
Stigla
Madaraja
Mandege ya bombadia

Huwa hawana kingine cha kusema.
Vipo vingi sana kaka
Wafanyabiashara ndogo wako free
Elimu ni bure utoi ada
Mgao wa umeme hakuna
Hospitali na zahanati zimejaa kila kona
Barabara za mijini zimewekwa bora kama unaishi dar nadhani unajionea
Adabu makazini
Kifupi kafanya mengi sana kaka acha unafiki

Back
Top Bottom