barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,375
- 29,732
Habari zenu!
Kama kichwa cha habari kinavyosema, ila sio kwa wote ila ni asilimia kadhaa, hawa ndugu zetu yaani masekretari na mareceptionist WANAWAKE wengi wana roho ya korosho kwa wale wanaopeleka barua za maombi ya kazi katika makampuni na maofisi.
Hawa wadada maana sio wamama, hupokea barua za hawa vijana wanaoenda omba kazi na kutoa maneno kuwa zimefika. Wengine kwa jinsi anavyokuongelesha tu utajua barua yako ndo imefika mwisho. Wafanyacho ni hawazipeleki kwa wahusika wenye kuzipitia na kufanya maamuzi. Eidha atairarua baada ya wewe kuondoka na kuiweka ktk dustbin au ataondoka nayo kwenda kwake na kuiangamiza huko.
Nasema haya sababu imewahi nitokea na baada ya kufuatilia kwa bosi muhusika ilidhibitika kuwa secretari hakufikisha barua.
Wiki ilopita imemtokea mwenzangu HIVYO naona ni katabia ka hovyo sana kwa hawa madada zetu.
Tafadharini, acheni KUWABANIA wenzenu, maisha ni kutafuta sio kubaniana, huwezi jua bahati ya mwenzio imelalia wapi.
BADILIKENI, ACHENI HIYO TABIA YA KURUDISHANA NYUMA.