Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kanye2016

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
2,895
2,985


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya PRE SCAN AUCTION MATT waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Adam Kighoma Malima alikuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, aliwahi kuwa pia Naibu Waziri wa Fedha enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.

====

UPDATES:

Adam Malima afikishwa Mahakamani kwa Kumzuia Askari kufanya kazi yake. Habari zaidi soma=>News Alert: - Adam Malima afikishwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka la 'Kumzuia askari kufanya kazi yake'
 
Back
Top Bottom