Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu askari aliyefyatua risasi hewani mbele ya Waziri wa zamani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278

'Kamishna Sirro asema mzozo kati ya Polisi na Adam Malima ulisababishwa na kuegesha gari vibaya na alipotakiwa kulipeleka 'yard' alikataa.

Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu askari aliyefyatua risasi hewani mbele ya Waziri wa zamani Adam Malima, "Waziri alikataa kutoa gari"

"Kukosekana maelewano ndio kilichofanya askari kutumia nguvu ya ziada na kufyatua risasi tatu ili kuwatuliza wananchi"

Kamishna Sirro: Polisi alifyatua risasi hewani kuwatawanya watu na kufanikisha ukamataji wa mtuhumiwa. Ile ni mbinu ya kufanikisha ukamataji

Kamanda Sirro ametoa kauli muda mfupi uliopita wakati akiongea na waandishi wa habari leo.

Majibu haya yametokana na Mjala unaoendelea Mtandaoni kuhusu Adam Malima kutishiwa kwa Bunduki. Zaidi soma=>Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu
 
Japo askari hakufanya poa lakini acha liwe onyo kwa viongozi wengine wanaojiona wapo juu ya sheria
uoga huo unapoondoka vipi kwa wananchi wakawaida wasio na kinga,sidhani kama ni busara kupelekana kwa style hii haya mambo haya chelewi kujirudi kunamtu atakataa kufedheheshwa na historia tukaibadili ndani ya muda mfupi,tukumbuke hakuna aliye juu ya sheria hata ukivaa mkanda na crown na ukaap na kuapizwa lazima tujali sheria
 
'Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu askari aliyefyatua risasi hewani mbele ya Waziri wa zamani Adam Malima, "Waziri alikataa kutoa gari"

Huu ni ujinga of the top order kwa mtu kama Kamanda Sirro, kama kweli amesema hivi. Kwa hiyo mtu akikataa kutoa gari askari ajibu kwa kupiga risasi hewani? Kwa nini wasimkamate?

Hivi hawa askari huwa wanaathiriwa kichwani kwa kukaa sana kwenye ile harufu mbaya ya kwenye vituo vyetu vya polisi? Naomba wanasayansi mfanye uchunguzi kujua ile harufu mbaya ina composition gani na athari gani za kiakili kwa mtu aliyekuwa exposed kwa muda mrefu. Tunaweza kuwa tunashangaa matendo ya polisi wetu na viongozi wao kumbe kuna chanzo cha kisayansi sio kisiasa.
 
Sasa kukataa kutoa gari ndio urushe risasi hovyo? Niishauri tu serikali, wakimaliza uhakiki wa vyeti waanze na uhakiki wa ubongo pia hasa kwa viongozi viongozi.

Ingawa sipendi sana mtu akisema unanijua mimi nani, kuna mpumbavu mmoja kuna siku aliniuliza nikamwambia ndio wewe ni DG wa usalama, unasemaje sasa. Sitakagi ujinga mimi.
 
Sasa ulitegemea siro amtetee malima!
Ingeingia kwenye rekodi za maajabu ya dunia

You are missing the point. Suala ni haki kutendeka na sio unamtetea nani. Kiuhalisia pale hapakuwa na usahihi wa matumizi ya silaha. Hakuna hayo mazingira. Ukiangalia kwa makini hata yule askari mwingine hakukubaliana na mwenzake na ndio maana alikuwa akim restrain mara kwa mara. Huwezi kuwa na jeshi lenye nidhami bila kusimamia mifumo ya utendaji wake wa kazi kwa weledi.
 
Maskini Tanganyika unaelekea wapi,naona kama unapotea Tanganyika,rudi rudi!!Ulifunga ndoa na amani leo unafunga amani na vitu vyenye ncha kali!!Na watu wasio na huruma
 
Back
Top Bottom