Adam Malima afikishwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka la 'Kumzuia askari kufanya kazi yake'

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mwanasiasa Adam Malima afikishwa Mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashtaka, ni baada ya sakata la malumbano na askari jana.


tmp_1432-IMG_20170516_143235-813247330.jpg

Kujua kisa kizima, soma => Masaki: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu
--------

OB/RB/7306/2017 KOSA; KUMZUIA ASKARI KUFANYA KAZI YAKE
MTUH: ADAM KIGOMA MALIMA

Mlalamikaji ni askari H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa kampuni ya PBEL inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo eneo la Double Tree Hotel Masaki alizuiliwa kutekeleza wajibu wake na aliyekuwa waziri wa zamani wa kilimo huku akishirikiana na wanachi kuwazuia askari hao.

Askari huyo aliamua kupiga risasi sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa. Hata hivyo mtuhumiwa pamoja na dereva wake walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Oysterbay.

=====

UPDATES:

Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi.
Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alitenda kosa.

Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

Kombakono ameongeza kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.
Watuhumiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wako nje kwa dhamana.mahakama imemtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini dhamana ya milioni 5. Aidha Mahakama imemtaka kila mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka ofisi yoyote inayotambulika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.Wakili Kibatala ameieleza mahakama kuwa, tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo atawasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake.

Amedai kuwa, katika shtaka hilo maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.
 
OB/RB/7306/2017 KOSA; KUMZUIA ASKARI KUFANYA KAZI YAKE
MTUH: ADAM KIGOMA MALIMA

Mlalamikaji ni askari H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa kampuni ya Pbel inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo eneo la double tree hotel masaki alizuiliwa kutekeleza wajibu wake na aliyekuwa waziri wa zamani wa kilimo huku akishirikiana na wanachi kuwazuia askari hao (.) askari huyo aliamua kupiga risasi sita hewan ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa (.) hata hivyo mtuhumiwa pamoja na dereva wake na kufikishwa kituo cha polisi Oysterbay (.)
 
Dah Tangu jana naona ile clip nimejikuta nimepata ganzi aiseeee ,Yaan nikiwafikiria hawa askari wa barabarani na usumbufu wao ,Dah yaan kumiliki gari binafsi kwa nchii hii ni kosa la jinai ,
maana hawa askar wamekuwa kero na waonevu sana kwa wenye magari ,mkulu asipoliangalia hili na akasikia vilio vya watu kuna kazi kubwa mbeleni
 
Halafu waje na kwa madereva wanaokaidi kupisha gari za wagonjwa au kufuata nyuma ya misafara.
Wasisahau madereva wanaoongea na simu wakiwa wanaendesha magari
Wasiwaache pia madereva wanaokojoa kwenye chupa na kuzitupa barabarani hasa wanaume
Bila kuwasahau polisi wa usalama barabarani wasimamie kikamilifu ukaguzi wa magari kama yanafaa kuwepo barabarani na sio kukimbilia kukusanya hela kw makosa ya kulazimisha ili fungu likamilke.
 
HATIMAYE Pascal Mnaku, mlinzi wa kampuni ya Ultimate Security aliyepambana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) jijini Dar es Salaam, amefukuzwa kazi na muajiri wake huyo.

Mnaku alijikuta kwenye mpambano mkali na waziri huyo baada ya kumtaka asogee pembeni ya mashine hiyo ya Standard Chartered ili kupisha wateja wengine baada ya Ngeleja kuonekana akitumia muda mwingi kuongea na simu akiwa ndani ya chumba cha mashine hiyo.

Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka Ultimate na kuthibitishwa na Mnaku, uamuzi wa kumfukuza kazi ulitolewa mara baada ya kikao cha nidhamu cha kampuni hiyo kilichofanyika jana kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi jioni kwenye ofisi za Ultimate. "Ni kweli nimefukuzwa kazi na hivi ninavyoongea na wewe ndio nimetoka katika kikao cha nidhamu na uamuzi uliofikiwa ndio huo,"alisema mlinzi huyo ambaye hakutetereka wakati Waziri Ngeleja alipohoji kama anamfahamu ni nani wakati akitakiwa kutoka kwenye ATM. "Na hii ni kutokana na kitendo changu cha kumtaka Waziri Ngeleja awapishe wateja wengine kwenye ATM," alilalamika Mnaku.

Jana jioni Mnaku aliliambia Mwananchi kuwa anatakiwa aende kuchukua barua yake ya kutimuliwa kazini Januari 30. Hata hivyo, mara baada ya gazeti hili kuripoti sakata hilo, Ngeleja alikiri kutokea kwa mtafaruku huo na kujitetea kuwa Mnaku ndiye aliyekuwa chanzo cha mtafaruku huo uliotokea kwenye mashine ya fedha iliyo kwenye jengo la Harbour View (zamani JMall). Mwananchi iliripoti kuwa waziri huyo alikaribia kuzichapa na mlinzi huyo kwenye baada ya kuombwa asogee pembeni kupisha wateja wengine.
 
Mwanasiasa Adam Malima afikishwa Mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashtaka, ni baada ya sakata la malumbano na askari jana.

Kujua kisa kizima soma Masaki: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu
---
OB/RB/7306/2017 KOSA; KUMZUIA ASKARI KUFANYA KAZI YAKE
MTUH: ADAM KIGOMA MALIMA

MLALAMIKAJI NI ASKARI H.7818 PC ABDUL AKIWA KAZIN NA MAAFISA WA KAMPUNI YA PBEL INAYOJIHUSISHA NA KUKAMATA WATU WANAOPAKI MAGARI HOVYO ENEO LA DOUBLE TREE HOTEL MASAKI ALIZUILIWA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE NA ALIYEKUWA WAZIRI WA ZAMANI WA KILIMO HUKU AKISHIRIKIANA NA WANACHI KUWAZUIA ASKARI HAO (.) ASKARI HUYO ALIAMUA KUPIGA RISASI SITA HEWAN ILI KUWATULIZA WATU WALIOKUWA WANAZOMEA WAKIONGOZWA NA MTUHUMIWA (.) HATA HIVYO MTUHUMIWA PAMOJA NA DEREVA WAKE NA KUFIKISHWA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY (.)
Is there a necessity to file such a case?
 
Back
Top Bottom