TANZIA Mtanzania auliwa kwa kupigwa risasi Marekani, anaitwa RODGERS KYARUZI, alipata maluweluwe

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,881
109,191
275688443_501466041422299_7856642314917741392_n.jpg
Poleni sana wafiwa, Poleni sana Watanzania popote mlipo, Poleni sana Tanzania Diaspora wa USA. sote tunyayue sauti kulaani kitendo hiki.

USA wanajulikana kwa ubaguzi wao kwa watu weusi, huyu Mtanzania mwenzetu na yeye yamemkumba? Au kauliwa na mweusi mwenzake?

The Georgia Bureau of Investigation has identified a man who was shot and killed Wednesday afternoon after struggling for an Atlanta police officer's gun at a restaurant in Buckhead.

The shooting happened around 2:45 p.m. at the Lenox Village business complex, located in the 2700 block of Lenox Road.

Soma zaidi: https://www.fox5atlanta.com/news/gb...over-atlanta-officers-gun-buckhead-restaurant

Habari inajieleza yenyewe lakini haijakamilika kwa kina, sema mtangazaji anaongea Kiswahili kibovu, hana sauti yenye haiba ya utangazaji. Mwenye maelezo zaidi atie nyama.

Poleni tena wafiwa





===========================

261112674_472109371202841_5800194197544028872_n.jpg

MAMLAKA ZAELEZEA TUKIO LA RODGERS KYARUZI KUULIWA KWA RISASI

Ofisi ya Upelelezi ya Georgia (GBI) imemtaja mtu ambaye amepoteza maisha kwa kupigwa risasi na askari baada ya kutokea purukushani Mei 4, 2022 kuwa anaitwa Rogers Kyaruzi.

Rogers Kyaruzi amekuwa akitajwa mara nyingi mitandaoni kuwa ni Mtanzania, alikuwa ameshabadili uraia na kuwa raia wa Marekani.

GBI wanasema tukio hilo lilitoka nje ya Mgahawa wa Buckhead, saa 8:45 mchana, ambapo askari Lawrence Holland aliyekuwa akilinda usalama karibu na maeneo hayo alimkuta Kyaruzi akidaiwa alikuwa akifanya vurugu.

Alipojaribu kumtuliza ilishindikana na Kyaruzi akawa anataka kuchukua silaha ya askari huyo, ambapo katika kujilinda akafyatua risasi iliyompata Kyaruzi.

Kyaruzi aliyekuwa na umri wa miaka 30 alikuwa Mkazi wa Lithonia, alipelekwa Atlanta Medical Center ambapo ndipo mauti yalipomkuta akiwa hospitalini hapo.

GBI wamesema kuwa uchunguzi unaendelea kiwemo kupitia video iliyorekodiwa na kamera ya askari huyo kupitia vifaa maalum wanavyovaa askari.

Takwimu zinaonesha askari huyo anakuwa wa 45 kuhusika katika tukio la kurusha risasi ambalo linalofanyiwa uchunguzi na GBI tangu kuanza kwa mwaka 2022.

DADA WA KYARUZI AZUNGUMZA
Myra Yorke ambaye ni dada wa Kyaruzi anasema: “Nilishtushwa sana na taarifa hiyo, sijui nini kimetokea, tunasubiri uchunguzi.

“Kaka yangu alihamia hapakutoka Tanzania akiwa mdogo, alikuja Marekani kuishi katika ndoto yake, alikuwa mcheshi na mtu ambaye anapenda utani.”


KIONGOZI WA WATANZANIA AELEZEA HISTORIA YA KYARUZI
Mtu mmoja ambaye amejitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Watanzania waliopo Georgia, Marekani amesimulia kuhusu anavyomfahamu marehemu na kufafanua kilichotokea:

“Rogers Kyaruzi ni mzaliwa wa Tanzania, alikuja hapa akiwa na umri wa miaka 12, baadaye mama yake aliolewa na Mghana ambaye ni Profesa.

“Kyaruzi alihitimu masomo yake hadi ngazi ya chuo, maisha yao hayakuwa mabaya katika familia.

“Kyaruzi ni mmoja wa Watanzania ambao wamekuja muda mrefu na hawapo karibu sana na Watanzania wengine kama kina sisi ambao tumekuja hivi karibuni, hiyo ni kwa kuwa maisha yao yamebadilika na kuwa kama Wamarekani, hata uzungumzaji wao unabadilika.

“Mimi sikuwa namjua kwa ukaribu, lakini ni Mtanzania kabisa hata kama alikuwa ameshachukua uraia wa Marekani, mama yake yuko hapa na ni mwanajumuiya mwenzetu (Watanzania).


CHANZO CHA KIFO
“Kyaruzi alikuwa na rafiki yake wa karibu sana ambaye alifariki mwaka jana (2021).

“Siku ya tukio (Mei 4, 2022), Kyaruzi alipofika eneo la tukio akaingia kwenye mgahawa baada ya kutoka wakati anaingia kwenye gari inadaiwa akawa anamuona rafiki yake huyo ambaye alishafariki, akitoka ndani ya gari hamuoni.

“Akampigia simu mama yake kuomba msaada kumwambia anahisi anaona kama kuna maluweluwe yanamtokea, mama mtu akamwambia kuwa yuko mbali muda huo na akampigia simu mke wa Kyaruzi ili aende eneo la tukio.

“Baada ya hapo Kyaruzi akawa anapiga kelele akiomba msaada kwa watu wanaopita, ikaonekana kama anafanya vurugu, alipotokea askari akajaribu kumtuliza lakini ikawa ngumu na inaonekana kuna vitu ambavyo walitofautiana.

“Kumbuka kuwa Kyazuri alikuwa ni mpiganaji wa mieleka, hapo ikatokea mshikemshike, akamkamata askari chini na kumuweka chini kwa dakika kadhaa, lakini ghafla askari akampindua na kumuweka chini kisha katika kujilinda akafyatua risasi ambayo ndiyo iliyomuua mwenzetu.

“Hata nilipozungumza na mama yake baadaye akakiri kupigiwa simu na mwanaye na kusema mwanaye hakuwa sawa kichwani, hata video za tukio lenyewe nilizoona zinaonesha alikuwa akipiga magoti kama anayeomba msaada, yaani ni kama alikuwa amechanganyikiwa hivi.”

275058366_128545939694490_8035306087913477908_n.jpg

Source: Ajc & Fox5atlanta
 
USA wanajulikana kwa ubaguzi wao kwa watu weusi, huyu Mtanzania mwenzetu na yeye yamemkumba? Au kauliwa na mweusi mwenzake?

The Georgia Bureau of Investigation has identified a man who was shot and killed Wednesday afternoon after struggling for an Atlanta police officer's gun at a restaurant in Buckhead.

FF hiyo paragrafu ya pili inaeleza kuwa kauawa na polisi baada ya huyo ndugu yetu kutaka kunyang'anya bastola ya polisi...

Hivyo naona wakamdhibiti kwa kumchapa risasi na akafia hospitalini...
 
Atlanta ni mji wa kihuni sana na rappers wengi na producers wao wanazaliwa uko. Ila mtu akipigwa risasi na askari huwa naamini kuna chanzo na yeye kachangia, askari atoke from nowhere apige mtu risasi kisa ubaguzi? Siamini sana katika hilo.

Kesi nyingi kama hizo unakuta ubaguzi unachangia kiasi kidogo
 
Wataandamana huko marekani? Au kwakua siyo mmarekani mweusi basi watapotezea . Ushauri wa bure vijana bora kuishi kwenu hata kama ni masikini kuliko kukimbilia miji ya watu matokeo yake ndio hivyo unauliwa na hawana time .
 
Back
Top Bottom