Masaa 24 yameshapita

Masaa 24 yameshapita

Heeeyyy

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Suala la Saddam ni suala la kisiasa zaidi alikuwa anatishia maslahi yao mapana ya kiuchumi na watu waote wanajuwa ilikuwa ni hali ya kutafuta idhini ya kimataifa na mbaya zaidi Saddam alikuwa anawatisha kuwa anazo silaha kwa kukataa kuruhusu wakaguzi kwa kudhani itamsaidia ila hilo sio suala la Makonda hawana maslahi naye na zaidi siku nyingi wanasema fanyeni uchunguzi kimyaa haiwezekani matukio kibao eti asishikwe mtu hata mmoja inaweza kuwa sio yeye lakini lazima majibu yapatikane ni nani huyo anafanya upuuzi huu. kumbuka kuna watu kibao wamepotea au kutekwa wakati fulani lakini kweli hakuna mtu hata kushukiwa?? hapa wamemtaja mtu mmoja hawajasema nchi sasa usiniambia Mkuu wa mkoa anatishia maslahi yao. hapana kuna mambo hayasemwi na ni lazima yasemwe. Serikali ina mtandao mkubwa ukitishia maslahi ya nchi utajulikana kabla ya matukio.
Saddam Hussein aliruhusu wakaguzi wakimataifa,jaribu kua na kumbukumbu nzuri,Wakati wa vita vya Iraq na Iran (Vita ya Ghuba ya Uajemi) kwa zaidi ya miaka 8 Saddam alipata support ya US,Nchi kama US inaangalia maslahi yake,Mbona Rwanda waliuana Wahutu na Watusi lakini hawakuingilia? Hata US kuna watu hupigwa risasi mchana kweupe na kuna kesi kibao za Polisi weupe kuwapiga black,Siasa ni zaidi unavyoijua mkuu,haya mambo hua yana siri kubwa iliyofichika.
 
Tangu marekani itoe taarifa yao yameshakatika masaa zaidi ya 24 bila kusikia kikohozi wala chafya ya kiongozi yeyote wa kiserikali akiongelea jambo lolote lile. Kwa kifupi mpaka muda huu hakuna aliyeonekana akijaribu hata ile kujifanya anajikuna.

Nchi ni kama imepigwa ganzi, ndugu watanzania wenzetu wamekufa huko Moshi kwenye ajali ya Mafuta hatujasikia kauli ya viongozi hadi hivi sasa zaidi ya Kamanda Hamduni na mkuu wa Wilaya Moshi.

Je, tuamini serikali imejichimbia ikifanya rehersal ya kuja na majibu? Au Our Numero Uno amestushwa na taarifa hizo kufahamika na dunia au alikua hazifahamu na sasa yupo kupata briefing!!

Vipi viongozi ambao hata hawasikiki wakiendelea kuyaongelea maeneo yao kama tulivyozoeshwa?
EMBU TUACHENI KIDOGO TUNAOMBOLEZA VIFO VYA WACHAGA WENZETU ATI HAMNA HATA ROHO YA HURUMA NA UBINADAMU
 
Hii ngumu kumeza huko JIWE lile komwe lake linawaka moto.
Hapa ndio ataona umuhimu wa wanadiplomasia wenye nchi yao.
 
Saddam Hussein aliruhusu wakaguzi wakimataifa,jaribu kua na kumbukumbu nzuri,Wakati wa vita vya Iraq na Iran (Vita ya Ghuba ya Uajemi) kwa zaidi ya miaka 8 Saddam alipata support ya US,Nchi kama US inaangalia maslahi yake,Mbona Rwanda waliuana Wahutu na Watusi lakini hawakuingilia? Hata US kuna watu hupigwa risasi mchana kweupe na kuna kesi kibao za Polisi weupe kuwapiga black,Siasa ni zaidi unavyoijua mkuu,haya mambo hua yana siri kubwa iliyofichika.
Yes kuna kesi kibao kwa maana kuna watu wameshtakiwa. Lini hapa umesikia matukio yote yaliyotokea kuna mtu kakamatwa au kuna kesi.
 
Hapo kuna mambo mawili yaliobakia, either serikali yetu itutoe kafara raia million zaidi ya 50 (tushughulikiwe nchi nzima) au atolewe kafara mmoja aliezua hili balaa lote (DAB).

Viongozi wetu nchi hii wana matatizo, sisi raia sio kwamba tunaunga mkono ushoga, hapana, tunauchukia ushoga toka moyoni kutokana na imani na maadili yetu. ila huyu DAB alijisahau sana akawa anaji MWAMBAFY kupita kiasi. Ameonea watu wengi sana.

Kuna wapo aliowapa kashfa za kuuza madawa ya kulevya kwenye TV waliharibiwa biashara zao/kazi/maisha/heshima na wengine walifunga biashara zao zote nchini (Hakuna hata mmoja aliethibitishwa mbele ya mahakama wala kufungwa jela kwa kashfa hio - Ishu hii ilikua na nini nyuma ya pazia?).

Kufungia na kuwaonea wafanya biashara wa sehemu za starehe, kiongozi wa serikali badala ahamasishe biashara ili mzunguko wa hela uwepo na ajira, anapangia watu "MUDA" wa kuanza biashara (kama vile anawasaidia kulipa kodi au ana share katika hizo biashara). Amefungia matumizi na biashara ya "SHISHA" kitu ambacho dunia nzima inaruhusu, na ni kitu kilichokua na ajira/mzunguko wa hela mkubwa sana katika sehemu za starehe na hoteli za kitalii (Kwa kigezo cha kijinga eti wanatumia kuvutia madawa ya kulevya - Mbona hajazuia matumizi na kuuzwa kwa "RIZLA" au "SIGARA" kwenye maduka na supermarket??? Rizla na Sigara tunatumia kusokotea na kuchanganya skadi kupunguza ukali. . . . . Leo watalii wanakuja nchini kwaajili ya mapumziko wanakutana na masharti ya muda wa kuanza starehe???? Unawalipia gharama za kuja nchini kwenye mapumziko mpaka uwapangie muda wa kufanya starehe???

Sakata la wanaume kutelekeza watoto, lilianza kwa siku mbili tu na kisha kufa, na asilimia kubwa lilitumika kuchafua watu na si kusaidia watu.

Kutoa kejeli kwa wananchi wa Dar Es Salaam, asiokua na ajira wala elimu atarudi kijijini. Kupitisha msako nyumba hadi nyumba kupima tezi dume (Aliwaza budget/gharama za kufanya hili? Hela ingetoka hazina au bungeni?)

#Watu walimkumbusha kuna maisha baada ya uongozi, sasa yamefika, ajionee huku mtaani watu walivyoweka beef nae.
Mkuu mbona ile ya kufukuza mashoga umeiluka...acha kukimbia kivuli chako watu wote wanafahamu makonda kapigwa ban baada ya kuyafurusha mashoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba Niipongeze serikali kwa kimya hiki.. Hili sio jambo la kukurupuka tena... Hata kidogo... Kuna mlolongo wa matukio yatafuata baada ya hili... Hivyo linahitaji muda wa kutosha weledi na hekima kwenye kulitolea tamko

Jr
Ni kweli mkuu ila nafikiri cha kufanya ni kwa serikali kwanza kushukuru kwamba marekani wametusaidia kuliona tatizo ambalo muda wote hatujaliona,pili iombe msamaha kwa marekani na kujutia kosa hilo n kukili kutorudia tena. Tatu iombe ushauri wa nini cha kufanya ili tuendelee kuonekana vizuri mbeya ya jamii ya kimataifa,nne serikali imkamate makonda na kumkabidhi kwa serikali ya marekani ili imshughulikie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ni kama imepigwa ganzi, ndugu watanzania wenzetu wamekufa huko Moshi kwenye ajali ya Mafuta
Hizi ajali za mafuta zimekuwa aibu kwa taifa letu.
Mara mafuta yaliyomwagika kwenye ajali ya gari yameuwa watu.
Mnasahau kisa hiki unasikia kuna mtumishi wa Mungu kaona malori ya mafuta haya anguki kamwaga kwa makusudi mafuta yake ya upako watu wauwane!

CC: Mshana Jr
 
Wamarekani wamesema wanazo taarifa za kutosha kuwa BASHITE ndio kiongozi wa watekaji na wapotezaji watu sasa unategeme nani aongee hapo
wanaogopa kuongea..maana wao ndio victims wakuu...makonda ni mbwa tu wamfuga mbwa ukiona ana bweka ujue ametumwa...ama anataka kumfurahisha mfugaji wake
 
Hizi ajali za mafuta zimekuwa aibu kwa taifa letu.
Mara mafuta yaliyomwagika kwenye ajali ya gari yameuwa watu.
Mnasahau kisa hiki unasikia kuna mtumishi wa Mungu kaona malori ya mafuta haya anguki kamwaga kwa makusudi mafuta yake ya upako watu wauwane!

CC: Mshana Jr
😃😃😃inasikitisha ..inachekesha pia
 
Uyo mwamposa wa kazi gani achangii chochote serikalini hakatwi kodi sasa anatuulia ndugu zetu wa kazi gani mpuuzi mmoja tu apigwe bani aende uko nigeria kwa wenzie hatuna shida nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi ya mauaji si ndogo mkuu, hasa ukibaini mtu uliyemtuma keshabainika na 'vyombo vya dola'

Anyway tuwaombee marehemu wetu na wafiwa. Tamko la Rais pia linahitaji juu ya yote. Hapa ndio kipimo Cha busara ya kiongozi kinatakiwa kitamalaki.
Kabisa, kaka mkubwa anapokemea jambo fulani, unatakiwa upime kila kauli itakayokutoka vinginevyo ni bora utumie busara ya kukaa kimya kulinda diplomasia na economic sanctions,
 
Hapo kuna mambo mawili yaliobakia, either serikali yetu itutoe kafara raia million zaidi ya 50 (tushughulikiwe nchi nzima) au atolewe kafara mmoja aliezua hili balaa lote (DAB).

Viongozi wetu nchi hii wana matatizo, sisi raia sio kwamba tunaunga mkono ushoga, hapana, tunauchukia ushoga toka moyoni kutokana na imani na maadili yetu. ila huyu DAB alijisahau sana akawa anaji MWAMBAFY kupita kiasi. Ameonea watu wengi sana.

Kuna wapo aliowapa kashfa za kuuza madawa ya kulevya kwenye TV waliharibiwa biashara zao/kazi/maisha/heshima na wengine walifunga biashara zao zote nchini (Hakuna hata mmoja aliethibitishwa mbele ya mahakama wala kufungwa jela kwa kashfa hio - Ishu hii ilikua na nini nyuma ya pazia?).

Kufungia na kuwaonea wafanya biashara wa sehemu za starehe, kiongozi wa serikali badala ahamasishe biashara ili mzunguko wa hela uwepo na ajira, anapangia watu "MUDA" wa kuanza biashara (kama vile anawasaidia kulipa kodi au ana share katika hizo biashara). Amefungia matumizi na biashara ya "SHISHA" kitu ambacho dunia nzima inaruhusu, na ni kitu kilichokua na ajira/mzunguko wa hela mkubwa sana katika sehemu za starehe na hoteli za kitalii (Kwa kigezo cha kijinga eti wanatumia kuvutia madawa ya kulevya - Mbona hajazuia matumizi na kuuzwa kwa "RIZLA" au "SIGARA" kwenye maduka na supermarket??? Rizla na Sigara tunatumia kusokotea na kuchanganya skadi kupunguza ukali. . . . . Leo watalii wanakuja nchini kwaajili ya mapumziko wanakutana na masharti ya muda wa kuanza starehe???? Unawalipia gharama za kuja nchini kwenye mapumziko mpaka uwapangie muda wa kufanya starehe???

Sakata la wanaume kutelekeza watoto, lilianza kwa siku mbili tu na kisha kufa, na asilimia kubwa lilitumika kuchafua watu na si kusaidia watu.

Kutoa kejeli kwa wananchi wa Dar Es Salaam, asiokua na ajira wala elimu atarudi kijijini. Kupitisha msako nyumba hadi nyumba kupima tezi dume (Aliwaza budget/gharama za kufanya hili? Hela ingetoka hazina au bungeni?)

#Watu walimkumbusha kuna maisha baada ya uongozi, sasa yamefika, ajionee huku mtaani watu walivyoweka beef nae.
Mbona hukutaja kuwa kadhibiti panyaroad, watoto zaidi ya 500 wamepata huduma ya moyo bure, uwajibikaji umeongezeka kwa kuwadhibiti ikiwemo kuwakamata wakandarasi wavivu na watumishi wabadhirifu, walemavu zaidi ya elfu moja walipata miguu ya bandia, akina mama waliopigwa mimba na kutelekezwa wamepata haki ya matunzo. Amejenga hospital kubwa ya mama na mtoto kwa msaada wa korea
 
Back
Top Bottom