kantalambaz
JF-Expert Member
- Dec 24, 2017
- 1,878
- 887
Kwani hao siyo viongozi?Tangu marekani itoe taarifa yao yameshakatika masaa zaidi ya 24 bila kusikia kikohozi wala chafya ya kiongozi yeyote wa kiserikali akiongelea jambo lolote lile. Kwa kifupi mpaka muda huu hakuna aliyeonekana akijaribu hata ile kujifanya anajikuna.
Nchi ni kama imepigwa ganzi, ndugu watanzania wenzetu wamekufa huko Moshi kwenye ajali ya Mafuta hatujasikia kauli ya viongozi hadi hivi sasa zaidi ya Kamanda Hamduni na mkuu wa Wilaya Moshi.
Je, tuamini serikali imejichimbia ikifanya rehersal ya kuja na majibu? Au Our Numero Uno amestushwa na taarifa hizo kufahamika na dunia au alikua hazifahamu na sasa yupo kupata briefing!!
Vipi viongozi ambao hata hawasikiki wakiendelea kuyaongelea maeneo yao kama tulivyozoeshwa?
Sent using Jamii Forums mobile app
hao hao wameiweka Libya kwenye machafuko na leo Libya wanatamani yule gwiji Gadafi afufuke nasi tunataka kuwasujudu wamarekani amini ipo siku tutalia na kuwatolea maneno machafu hao wamarekani kwa kusema kuwa tungejua
