Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,936
Haji Landa Mkazi wa kijiji cha Ihanja, Wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Mazingira ya kifo chake ni kwamba ilikuwa muda wa usiku Jana Alhamisi baada ya kupata mlo wa usiku na familia, marehemu alitoa nje kupunga upepo lakini wakati akilisogelea geti walitokea watu wakampiga risasi na kutokomea kusikojulikana
Jambo la kusikitisha mpaka naandika haya leo ijumaa saa 19:50 mwili bado upo eneo la tukio pamoja na taarifa kuwa ishatolewa kwa jeshi la polisi mkoa wa Singida.
Ndugu wa marehemu washafanya mipango yote ya msiba na mazishi lakini wanashindwa kuendelea na mipango mingine kwasababu nature ya kifo chake ni mpaka ruhusu ya Jeshi la Polisi.
Maoni Yangu;
Hii ni aibu kubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo. Nina uhakika huu ni uzembe wa hali ya juu na inabidi wakuu wa Jeshi Singida wawajibishwe. Haiwezekani mwili ulalel eneo la tukio kwa masaa 24. Mbona viongozi wa kisiasa mnawakamata na kuwasafirisha umbali mrefu. Imekuwaje mnashindwa kwenda kuchunguza mwili uliopigwa risasi. Shenzi kabisa.