Mary Mramba aficha shilingi 700,000,000 chumbani kwake!

Haya bana wenye hela zao, je ana uhusiano na aliyesema kuwa ndege ya mkulu wa kaya lazima inunuliwe hata wabongo wale nyasi enzi za Mr. Ben?
 
Shughuli zote zilizojaa mjini kweli milioni 700 zinafugwa ndani?!
 
Kiingereza sahihi ungeuliza hivi "Did this happen in Tanzania?" Ama sivyo ungeuliza kwa kiswahili tu. Wenyewe husema titi la mama ni tamu hata kama ni la mbwa!

Hii kitu ni tatizo la kitaifa mkuu. Hata naibu waziri wa elimu analijua hilo!

Naibu Waziri wa Elimu halijui, mwenye kulijua hilo tatizo ni Waziri wa Elimu!
 
Kama unabisha tafutata ile hotuba ya Mh Mulugo aliyoitoa huko kwenye kongamano afrika kusini. Labda hukunielewa nilimaanisha nini.
 
kwenye miti hakuna wajenzi hela zote hizo si angekuwa kaporomosha mijengo yaa kufa mtu?
 
Haiwezekani milioni mia saba kuhifadhi kabatini labda kama hilo kabati lina ukubwa wa chumba, au zote zilikuewa mpya toka BOT
 
Weee Tshs 700 trillion is Tz budget for 5 yrs.... RUDI SHULE UPESI....

U don't know where we are heading.....

TZ budget 2012/13 = 15 trillion

700 divide by 15 = 46.67 yrs

Almost 47 yrs kwa current budget...

Hapo kwenye nyekundu: Hiyo figure inatakiwa kuwa 700,000 na si 700, Soma vizuri heading ya thread!
 
mie kwa akili yangu fupi sana naona hizi hela ni feki, mihela yote hiyo waweka kwa chumba, au alitaka zizae zingine?
hopeless.
 
UTATA umegubika kuhusiana na kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni shilingi milioni 700,000,000 zilizofichwa na Mary Mramba katika kabati nyumbani kwake Stakishari eneo la Sabasaba, Ilala jijini Dar es Salaam. Fumuafumua ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu sakata la fedha hizo ambazo zilifichwa kati ya Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu, imegundua kwamba ziliibwa na watu kadhaa wakiwemo ndugu zake.

Imegundulika pia kuwa Mary alitoa taarifa Kituo cha Polisi Stakishari Septemba mwaka huu na kufunguliwa jalada la kesi STK/RB/16109/2012 na jalada la upelelezi STK/IR/12865/2012 akimtuhumu mtoto wa kaka yake aitwaye Digna Mark na wenzake kuhusiana na kesi ya kughushi hati ya nyumba na wizi huo.

Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kwamba mara baada ya Mary kugundua mwezi Januari kuwa fedha hizo zilikuwa zimeibwa, hakutaka kupeleka suala hilo polisi kwa sababu anazozijua yeye bali alifanya kikao na wanandugu akiwemo Digna na kubaini tayari magari matano na nyumba mbili zilizokuwa zinamilikiwa na mtu huyo ni vitu vilivyokuwa vimenunuliwa kwa fedha hizo.

Alichokifanya Mary ni kumpigia magoti Digna arejeshee hayo magari na nyumba hizo kwani hakutaka suala hilo alifikishe polisi. Pia inasemekana hata ndugu zake wengine walitoroka na zaidi ya shilingi milioni 400 kati ya fedha zilizoibwa. Imegundulika kuwa Digna aliiba shilingi milioni 300 na zingine ziliibwa na ndugu zake na kutoweka nazo. Mlalamikaji hakuwashitaki watu hao bali alikaa kimya ikidaiwa kwamba angeshitaki angeulizwa alikozitoa fedha hizo nyingi.

Imebainika kwamba wanandugu hao waliamua kuiba fedha hizo wakiamini Mary asingeweza kuwashitaki kutokana na kwamba wanajua jinsi fedha hizo zilivyopatikana hivyo alihofia kuwa siri ingevuja. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mary aliamua mambo hayo yaishe kwa siri ndani ya familia badala ya kupelekwa polisi ambapo yaliisha kwa upande wa Digna kwani aliamua kurejesha mali alizonunua na fedha hizo alizochukua ambazo ni shilingi milioni 300.

Hata hivyo, Mary alilazimika Septemba mwaka huu kwenda polisi baada ya kusikia kwamba Digna ameenda huko kutoa taarifa kwamba hati ya nyumba yake ilikuwa imepotea. Fumuafumua imegundua kuwa maelezo yaliyotolewa na Mary huko polisi juu ya fedha hizo ni kuwa alitumiwa na ndugu yake aitwaye Philipo Sindana aishiye nchini Italia kwa ajili ya kununua nyumba, kitendo kinachopingwa na Digna ingawa hajawa tayari kuelezea ukweli kwa sasa.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo liko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iandaliwe hati ya mashtaka. Wakati jalada hilo halijarudi, polisi imeelezwa kwamba askari wa kituo hicho cha Stakishari walikuwa wakilaumiana kwamba maelezo yalioandikwa hayakutosheleza na kuna kitu kinafichwa. Fumuafumua imebaini kwamba jalada hilo limesharudishwa toka kwa mwanasheria na kumweleza mkuu wa upelelezi Wilaya ya Ukonga, Idd Kiogomo kwamba hamna kesi ya kumshtaki Digna juu ya wizi ama kughushi bali ni kutoa taarifa za uongo za kupotelewa kwa hati ya nyumba.

Mkuu huyo wa upelelezi ameagizwa kutoa taarifa ya kina juu ya shitaka la wizi kwani maelezo ya Mary yanaonyesha kwamba wizi ulifanyika Januari hivyo iweje atoe taarifa hizo Septemba. Kiogomo ametakiwa kuchunguza na kutoa maelezo juu ya upatikanaji wa fedha hizo nyingi na kwa nini zilihifadhiwa ndani. Vilevile Mary aeleze ni mahakama gani ilimpa kibali cha kutaifisha nyumba na magari ya Digna.

Itaendelea wiki ijayo ikiwa na maelezo ya Mary, mumewe na jeshi la polisi.

jinsi ulivyotoa habari hii yaonesha wewe ni mhusika No.1, mrudishie Maria fedha yake.
 
Yeah mkuu, true kabisa. Hii ni bajeti ya Tanzania kwa miaka kama mitano hivi

kama ni 700 trilion ni bajeti ya tanzania kwa miaka 46 hapa hakuna cha kusema daraja/barabara/uwanja wa ndege n.k haukujengwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha. ni FULLY funded ni utekelezaji tuuu....
 
...dah!...kumbe watanzania tunalishwa nyasi bila sababu ya msingi!...mmm!...hii mijitu ya CCM imeisha tufanya watanzania kama ng'ombe...mambo mengine ya nchi hii ni hafadhali usiyajue,nasijikia hasira sana kiasi kwamba nikimwona kijana amevaa nguo za njano na kijani naweza hata kumpiga na kitu kizito au chenye ncha kali,potelea mbali "LIWALO NA LIWE"...
 
Kiingereza sahihi ungeuliza hivi "Did this happen in Tanzania?" Ama sivyo ungeuliza kwa kiswahili tu. Wenyewe husema titi la mama ni tamu hata kama ni la mbwa!

Au angeweza kuuliza hivi " Is this happening in Tanzania ?''

Naona Watanzania tulio wengi Kiswahili hatukijui..Kiingereza ndiyo hicho baya zaidi tunapuuza na vilugha vyetu...Tutakuwa watu wakuchekwa ktk ulimwengu huu..
 
UTATA umegubika kuhusiana na kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni shilingi milioni 700,000,000 zilizofichwa na Mary Mramba katika kabati nyumbani kwake Stakishari eneo la Sabasaba, Ilala jijini Dar es Salaam. Fumuafumua ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu sakata la fedha hizo ambazo zilifichwa kati ya Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu, imegundua kwamba ziliibwa na watu kadhaa wakiwemo ndugu zake.

Imegundulika pia kuwa Mary alitoa taarifa Kituo cha Polisi Stakishari Septemba mwaka huu na kufunguliwa jalada la kesi STK/RB/16109/2012 na jalada la upelelezi STK/IR/12865/2012 akimtuhumu mtoto wa kaka yake aitwaye Digna Mark na wenzake kuhusiana na kesi ya kughushi hati ya nyumba na wizi huo.

Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kwamba mara baada ya Mary kugundua mwezi Januari kuwa fedha hizo zilikuwa zimeibwa, hakutaka kupeleka suala hilo polisi kwa sababu anazozijua yeye bali alifanya kikao na wanandugu akiwemo Digna na kubaini tayari magari matano na nyumba mbili zilizokuwa zinamilikiwa na mtu huyo ni vitu vilivyokuwa vimenunuliwa kwa fedha hizo.

Alichokifanya Mary ni kumpigia magoti Digna arejeshee hayo magari na nyumba hizo kwani hakutaka suala hilo alifikishe polisi. Pia inasemekana hata ndugu zake wengine walitoroka na zaidi ya shilingi milioni 400 kati ya fedha zilizoibwa. Imegundulika kuwa Digna aliiba shilingi milioni 300 na zingine ziliibwa na ndugu zake na kutoweka nazo. Mlalamikaji hakuwashitaki watu hao bali alikaa kimya ikidaiwa kwamba angeshitaki angeulizwa alikozitoa fedha hizo nyingi.

Imebainika kwamba wanandugu hao waliamua kuiba fedha hizo wakiamini Mary asingeweza kuwashitaki kutokana na kwamba wanajua jinsi fedha hizo zilivyopatikana hivyo alihofia kuwa siri ingevuja. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mary aliamua mambo hayo yaishe kwa siri ndani ya familia badala ya kupelekwa polisi ambapo yaliisha kwa upande wa Digna kwani aliamua kurejesha mali alizonunua na fedha hizo alizochukua ambazo ni shilingi milioni 300.

Hata hivyo, Mary alilazimika Septemba mwaka huu kwenda polisi baada ya kusikia kwamba Digna ameenda huko kutoa taarifa kwamba hati ya nyumba yake ilikuwa imepotea. Fumuafumua imegundua kuwa maelezo yaliyotolewa na Mary huko polisi juu ya fedha hizo ni kuwa alitumiwa na ndugu yake aitwaye Philipo Sindana aishiye nchini Italia kwa ajili ya kununua nyumba, kitendo kinachopingwa na Digna ingawa hajawa tayari kuelezea ukweli kwa sasa.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo liko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iandaliwe hati ya mashtaka. Wakati jalada hilo halijarudi, polisi imeelezwa kwamba askari wa kituo hicho cha Stakishari walikuwa wakilaumiana kwamba maelezo yalioandikwa hayakutosheleza na kuna kitu kinafichwa. Fumuafumua imebaini kwamba jalada hilo limesharudishwa toka kwa mwanasheria na kumweleza mkuu wa upelelezi Wilaya ya Ukonga, Idd Kiogomo kwamba hamna kesi ya kumshtaki Digna juu ya wizi ama kughushi bali ni kutoa taarifa za uongo za kupotelewa kwa hati ya nyumba.

Mkuu huyo wa upelelezi ameagizwa kutoa taarifa ya kina juu ya shitaka la wizi kwani maelezo ya Mary yanaonyesha kwamba wizi ulifanyika Januari hivyo iweje atoe taarifa hizo Septemba. Kiogomo ametakiwa kuchunguza na kutoa maelezo juu ya upatikanaji wa fedha hizo nyingi na kwa nini zilihifadhiwa ndani. Vilevile Mary aeleze ni mahakama gani ilimpa kibali cha kutaifisha nyumba na magari ya Digna.

Itaendelea wiki ijayo ikiwa na maelezo ya Mary, mumewe na jeshi la polisi.

Huyo MARY MRAMBA ndio Nani?
Na DIGNA aliiba pesa wapi? kwenye story inasema kuna Mlalamikaji anayedai ameibiwa..
 
tunasubiri sehemu ya pili mambo yote ni hapo,hiyo habari ya mil.700 itajulikana tu na huo ujanja aliotumia mary kudai zimetumwa kutoka Italy kila kitu kitajulikana wakubwa,lakini kama mary kweli anauhusiano na Basil Pesambili Mramba yule mzee wa pale mkuu aliyewambia watanzania kwamba "mtakula majani" lazima ndege ya rais inunuliwe,watu wasihangaike yule mzee ukimuona utadhani hana akili yule ni nyoka ana vijisenti vingi amewekeza kwenye mahotel karibu kila kona ya hii dunia anzia pale Mo-town mji wa wagumu,nenda A-town,hashikiki yule ni nomaaaaaaa ile mbaya hata kale ka kesi kake kalikotungwa ili wazungu watupe misaada,atakatungua tu hapa ni suala la muda.
 
safi sana...wao hizo hela wamezipata wapi kama sio uwizi...na wao wameibiwa vile vile...what goes around comes around
 
eeh Mungu mbona si tunahangaika wakati wengine wanafaidi?
 
Back
Top Bottom