Mary Chitanda azidi kuaibika

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,415
Ndg wana JF,
Huyu mama ajulikanaye kwa jina la Mary Chitanda (Kiswahili Kitanda) naona anazidi kuwa katika wakati mgumu kutokana na matamshi yake ya utata. Ikumbukwe kuwa mama huyu ndiye hasa chanzo cha mgogoro wa nafasi ya Umeya Ausha mjini.
Wiki iliyopita aliwabwatukia maaskofu kwa kile alichokiita kuwa maaskofu wavue majoho ili wapambane kwenye siasa. Hii ilikuwa baada ya maskofu kukemea mauaji ya Arusha yaliyofanywa na polisi wakati wa maandamano ya amani ya chadema; vilevile maaskofu walidai kuwa hawamtambui meya huyo ambaye alichaguliwa kinyume na taratibu.
Lakini kuonesha kuwa hata viongozi wa juu wa ccm hawako pamoja na mama huyo, jumapili iliyopita Waziri Steven Wasira ambaye alikuwa anamwakilisha Rais katika sherehe za kumsimika Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mwanza aliwataka Maaskofu na viongozi wa dini kuikemea serikali pindi wanapoona inafanya maovu.
Vile vile juzi wakati waziri huyo alipokuwa anahojiwa na kituo cha TV cha TBC1 aliendelea kusisitiza kuwa kwa kukemea maovu ya serikali sio siasa hivyo alishikilia msimamo wake kuwa viongozi wa dini waendelee kuikosoa serikali pale wanapoona inakwenda kinyume na maadili.
Swali langu:
Huyu Mary Kitanda ni nani hasa hata apinge kauli ya Rais (iliyotolewa kwa niaba yake na Waziri Wasira). Anapata wapi kiburi cha kubwabwaja na kutishia amani ya nchi. Kikwete unamuona au humuoni huyu mama.

Quote:
Ukicheka na nyani shambani utayavuna mabua.
 
Naombeni picha yake tu...mengine niachieni mimi, najua janja ya kumfanyia!
 
Kumbe ni kitanda, yaani wanamlalia lalia ndiyo maana akili zake zimekaa kitandani tandani tuuu.PASHKUNA MKUBWA HUYU.
 
eti unamuuliza rais! huyuhuyu jk? mangapi hayaoni iweje hilo, we tuombe mungu 2015 ifike salama.
 
ni limbukeni wa kisiasa. Anatumia kiburi cha hawala yake makamba; mwisho wake uko ukingozi; do not worry!
 
Ndg wana JF,
Huyu mama ajulikanaye kwa jina la Mary Chitanda (Kiswahili Kitanda) naona anazidi kuwa katika wakati mgumu kutokana na matamshi yake ya utata. Ikumbukwe kuwa mama huyu ndiye hasa chanzo cha mgogoro wa nafasi ya Umeya Ausha mjini.
Wiki iliyopita aliwabwatukia maaskofu kwa kile alichokiita kuwa maaskofu wavue majoho ili wapambane kwenye siasa. Hii ilikuwa baada ya maskofu kukemea mauaji ya Arusha yaliyofanywa na polisi wakati wa maandamano ya amani ya chadema; vilevile maaskofu walidai kuwa hawamtambui meya huyo ambaye alichaguliwa kinyume na taratibu.
Lakini kuonesha kuwa hata viongozi wa juu wa ccm hawako pamoja na mama huyo, jumapili iliyopita Waziri Steven Wasira ambaye alikuwa anamwakilisha Rais katika sherehe za kumsimika Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mwanza aliwataka Maaskofu na viongozi wa dini kuikemea serikali pindi wanapoona inafanya maovu.
Vile vile juzi wakati waziri huyo alipokuwa anahojiwa na kituo cha TV cha TBC1 aliendelea kusisitiza kuwa kwa kukemea maovu ya serikali sio siasa hivyo alishikilia msimamo wake kuwa viongozi wa dini waendelee kuikosoa serikali pale wanapoona inakwenda kinyume na maadili.
Swali langu:
Huyu Mary Kitanda ni nani hasa hata apinge kauli ya Rais (iliyotolewa kwa niaba yake na Waziri Wasira). Anapata wapi kiburi cha kubwabwaja na kutishia amani ya nchi. Kikwete unamuona au humuoni huyu mama.

Quote:
Ukicheka na nyani shambani utayavuna mabua.

Kwenye list ya ngao wa Mhs Chenge mbona na yeye yumo?????????
Maslahi Ndg MASLAHI anatetea maslahi, njaa saana huyu!!!!!!!!!!!!
 
Nimechek kwenye mtandao wa bunge mtandao wenyewe ovyo tu, nimehangaika sana kupata picha ya huyu malaya bila mafanikio; lakini j4 ya wiki hii alionekana kwenye itv akibwabwaja kama kawaida yake, so kama kuna mtu ana access na itv anaweza akapata hata video yake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom