Marufuku ya nguo fupi, Mlegezo, Kiduku na mitindo kwa ujumla, Nyerere alimkataza Kawawa kusumbua wananchi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nadhani Tanzania imefikia mahali inabidi tuwe na wasiwasi na uongozi wa awamu ya tano chini ya Magufuli kwamba sasa serikali inahaha na kukosa focus na kuanza mambo mengi ambayo mengine ni usumbufu tu kwa wananchi. Imefikia Watanzania wanafuatiliwa kwa vitu vidogo vidogo vingi (micro managing) hadi sasa inakuwa kero. Hizi si dalili nzuri. Raisi yeyote yeyote mwenye staili ya namna hii ya uongozi ni kwamba yuko kwenye mwelekeio ambao utaleta matatizo huko mbele, na mara nyingi ni mwelekeo wa udikteta - micromanagement of citizens at the highest level.

Mfano ni hili la nguo fupi. Miaka ya 70, kwa wale mnaokumbuka, serikali kwa usimamizi wa Waziri Mkuu wakati huo, Rashidi Kawawa, ililivalia sana njuga suala la nguo fupi, nywele bandia nk. Hadi askari wa mgambo wakawa wanatembea mitaani kutafuta dada zetu waliovaa nguo fupi au kuwa na nywele bandia ili wakamatwe. Hata kulikuwa na baadhi ya matukio ya kina dada kuchaniwa nguo.

Hili jambo lilileta kero nyingi hadi Rais Nyerere akaingilia kati. Akamwambia Kawawa usihangaike na mambo yanayopita na wakati kama mitindo ya kuvaa au nywele. Leo watu watavaa mini-skirt na kesho utakuja mtindo wa max, pekosi halafu chupa, raizoni halafu stileto nk. Akaagiza wananchi wasibughudhiwe kwa vitu kama aina ya nguo walizovaa au sijui nywele za kubandika. Na kweli baada ya muda fulani kuvaa mini-skirt kuliisha bila serikali kuingilia, na hata nywele za bandia kutoweka.

Sasa mini skirt zimerudi kama ambavyo nywele bandia zilirudi. Si Tanzania peke yake bali dunia nzima. Kamanda wa polisi Mambosasa na timu yake wamelishupalia jambo hili. Suala la kujiuliza ni kwamba wametumwa na nani? Haya nayo ni maagizo ya Magufuli?

Mambosasa, bila hata kufikiri, anatoa kauli kwamba "kama sisi tunavaa nguo hizo wazungu wakija watajifunza nini?". Hii nimeona ni kauli ya mtu mmoja ambaye ana dalili za kutoelimika kabisa, na kwa maneno ya mitaani ni kauli ya kishamba kama imetolewa na mtu ambaye hajawahi kwenda shule kabisa (naive statement). Kwanza ni aibu kwa mtu kama Mambosasa kutoa reference kwa wageni toka nje kama "wazungu". Nashangaa mtu mwenye uwezo wa kufikiri kama huu ndio anakuwa na dhamana kubwa katika jeshi letu la polisi (nakumbuka bado kauli aliyotoa bila ushahidi kuwa Dr. Louis Shika alitumwa na Lugumi kwenda mnada wa TRA wa nyumba za Lugumi)

Kuna mambo kadhaa ningependa nimuulize Mambosasa na serikali ya Magufuli kwa ujumla. Hii Tanzania ya utalii tukianza kukamatana kwa kuvaa miniskir na staili ya nywele, wageni na watalii nao tutawakamata kwa mitindo yao ya kuvaa na nywele, au kwa sababu tunataka wao wajivunze kwetu tutawaacha?

Hii serikali sasa inaonekana imekosa focus. Imekuwa ikitapatatapa na kurukia mambo bila kufikiri.

Gazeti la Nipashe limeandika: Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku
Operesheni hiyo inaonekana kufanyika kuanzia wiki iliyopita katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam yakiwamo katikati ya jiji (Posta), Mbagala, Kariakoo, Temeke, Kinondoni na Magomeni.

Katika uchunguzi uliofanywa na Nipashe, imebainika kuwa watu wanaokamatwa ni wale walionyoa mtindo wa kuacha nywele nyingi katikati ya kichwa, maarufu kama kiduku na wanawake wavaa nguo fupi, zilizobana na zinazoonyesha maumbile.

Polisi imekuwa ikiwakamata watu hao ambao wengi ni vijana na kupelekwa vituoni kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamtwa kwa watu ambao wanakiuka maadili ya Kitanzania kwa kuvaa mavazi yasiyo na maadili, alipozungumza na Nipahe jana.

Alisema watu wanaovaa nguo fupi na zenye kuwadhalilisha wanafanya kosa la kimaadili hivyo wanawakamata na kuwachukulia hatua.

"Mtu akikutwa fukwe amevaa suti tutakushangaa," alisema Kamanda Mambosasa, "na tukikukuta upo uchi hatutakushangaa".

"Lakini hatutarajii kumkuta mtu aliyevaa nguo za fukwe akiwa kanisani. Tutamkamata tu."

Alisema wakikamata watu waliokiuka maadili ya Kitanzania huangalia kosa lililokiukwa kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuchukua hatua.

Aidha, Kamanda Mambosasa alisema askari wake wanakamata watu wananaojiuza na ambao wamekuwa wakiwauza wenzao katika maeneo mbalimbali ya nchi.

"Sisi hatuna operesheni ya kuwakamata wanaovaa nguo fupi, lakini tukikukuta umekiuka maadili ya Kitanzania tutakuwajibisha kwa sababu kama sisi tunavaa nguo hizo wazungu wanaokuja nchini watajifunza nini?"

Yursa Mohamed, mkazi wa Kimara, aliliambia Nipashe kuwa wiki iliyopita akiwa maeneo ya Posta alishuhudia polisi wakikamata watu waliovaa nguo zisizofaa.

MAUMBILE YAOAlisema watu waliokuwa wakikamatwa ni wanawake waliovaa nguo fupi, zilizobana na zinazoonyesha maumbile yao.

Alisema wanaume pia walikamatwa katika eneo hilo endapo walikuwa wamenyoa viduku, kuvaa suruali chini ya makalio na waliovaa nguo zilizochanywa chanwa.

"Polisi walikuwa wamesimama Posta," alisema. "Wakiona mwanamke aliyevaa nguo za kubana wanamuita kwa ustaarabu na akifika wanamuelekeza kupanda kwenye gari la polisi lililokuwa limepaki (limeegeshwa) pembeni. "Wanawake walikuwa wakiitwa na askari wanawake na wanaume vivyo hivyo (na askari wa kiume)."

Naye mkazi wa Tandika, Hadija Issa, aliiambia Nipashe kuwa alishuhudia askari katika maeneo hayo wakikamata watu waliovalia nguo za kudhalilisha.

"Wanapita mitaani mchana na magari yao, wakiona umevaa nguo fupi sana, zilizochanywa na wale walionyoa viduku, wanakamatwa na kupendishwa kwenye gari," alisema Hadija.

Kamatakamata kama hiyo imefanyika pia katika maeneo ya Magomeni na Kinondoni, kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe ambako uwepo wa askari uliwafanya baadhi ya wanawake kujifunga kanga ili kuepuka mkono wa sheria.

Mary Joshua, mkazi wa Ubungo, alilieleza Nipashe aliona askari wakipita na magari mtaani huku ikielezwa kuwa mbali na kutafuta wahalifu wa kawaida, walikamata watu wanaovaa nusu uchi wakati wa mchana.

"Nimesikia watu wanasema waaovaa (nusu) uchi na wanaonyoa viduku wanakamatwa mitaani na kuna watu nimeambiwa wamekamatwa ingawa mimi sijashuhudia," alisema.

======

UPDATES;

Habari hii imetolewa Ufafanuzi na Jeshi la Polisi. Zaidi soma=> Jeshi la Polisi: Hatukamati waliovaa vimini na kunyoa viduku, Mwandishi wa NIPASHE anatafuta umaarufu

Hii iko interesting. Jibu ni kwamba, Polisi hapa walichokuwa wanafanya ni damage control. Ni kwamba walikurupuka kuchukua hatua za kukamata nguo fupi na nywele kiduku bila kuwasiliana na mamlaka za juu. Sasa badala ya mamlaka za juu kuwakanusha na kutengua hatua hizi za Polisi, imefanyika katika namna tunayoita "damage control", kwamba isemwe kuwa mwandishi wa IPP alikosea. Kama Magufuli kwa mfano, angewakosoa Polisi hadharani juu ya hili, ingeharibu sana hadhi ya Mambosasa na Polisi kwa ujumla kwa wananchi (japo sidhani kama Mambosasa ana hadhi kubwa kwa wananchi). Namna Magufuli alivyoshughulika na hili ni zile mara chache ambazo huwa naona Magufuli anatumia busara badala ya nguvu. Niko willing ku-bet mshahara wangu wa mwezi huu kwamba huyu mwandishi wa IPP ameombwa asikanushe madai ya Polisi kuwa alikuwa anatafuta umaarufu na kutoa ushahidi wa chanzo cha habari yake. Na kama ingekuwa ni kweli kwamba Mwandishi wa IPP alijitungia habari kupata umaarufu, Nipashe ingekuwa imeshafungiwa miaka minne hadi sasa!
 
Mkuu hebu tulia
Wengine ndio tunapenda kuangalia hizo mini skirt kusudi tuchague vizuri,
Hebu tafadhali hili suala la nguo fupi serikali itulie tu.
Mkuu sijaipongeza serikali kwa ujinga huu na kupotezeana wakati.

upload_2018-1-17_10-33-6.png
 
Nadhani Tanzania imefikia mahali inabidi tuwe na wasiwasi na uongozi wa awamu ya tano chini ya Magufuli kwamba sasa serikali inahaha na kukosa focus katika mambo mengi ambayo mengine ni usumbufu tu kwa wananchi. Imefikia Watanzania wanafuatiliwa kwa vitu vidogo vidogo vingi (micro managing) hadi sasa inakuwa kero. Hizi si dalili nzuri. Raisi yeyote yeyote mwenye staili ya namna hii ya uongozi ni kwamba yuko kwenye mwelekeio ambao utaleta matatizo huko mbele, na mara nyingi ni mwelekeo wa udikteta - micromanagement of citizens at the highest level.

Mfano ni hili la nguo fupi. Miaka ya 70, kwa wale mnaokumbuka, serikali kwa usimamizi wa Waziri Mkuu wakati huo, Rashidi Kawawa, ililivalia sana njuga suala la nguo fupi, nywele bandia nk. Hadi askari wa mgambo wakawa wanatembea mitaani kutafuta dada zetu waliovaa nguo fupi au kuwa na nywele bandia ili wakamatwe. Hata kulikuwa na baadhi ya matukio ya kina dada kuchaniwa nguo.

Hili jambo lilileta kero nyingi hadi Rais Nyerere akaingilia kati. Akamwambia Kawawa usihangaike na mambo yanayopita na wakati kama mitindo ya kuvaa au nywele. Leo watu watavaa mini-skirt na kesho utakuja mtindo wa max, nk. Akaagiza wananchi wasibughudhiwe kwa vitu kama aina ya nguo walizovaa au sijui nywele za kubandika. Na kweli baada ya muda fulani kuvaa mini-skirt kuliisha bila serikali kuingilia, na hata nywele za bandia kutoweka.

Sasa mini skirt zimerudi kama ambavyo nywele bandia zilirudi. Si Tanzania peke yake bali dunia nzima. Kamanda wa polisi Mambosasa na timu yake wamelishupalia jambo hili. Suala la kujiuliza ni kwamba wametumwa na nani? Haya nayo ni maagizo ya Magufuli?

Mambosasa, bila hata kufikiri, anatoa kauli kwamba "kama sisi tunavaa nguo hizo wazungu wakija watajifunza nini?". Hii nimeona ni kauli ya mtu mmoja ambaye ana dalili za kutoelimika kabisa, na kwa maneno ya mitaani ni kauli ya kishamba kama imetolewa na mtu ambaye hajawahi kwenda shule kabisa (naive statement). Kwanza ni aibu kwa mtu kama Mambosasa kutoa reference kwa wageni toka nje kama "wazungu". Nashangaa mtu mwenye uwezo wa kufikiri kama huu ndio anakuwa na dhamana kubwa katika jeshi letu la polisi (nakumbuka bado kauli aliyotoa bila ushahidi kuwa Dr. Louis Shika alitumwa na Lugumi kwenda mnada wa TRA wa nyumba za Lugumi)

Kuna mambo kadhaa ningependa nimuulize Mambosasa na serikali ya Magufuli kwa ujumla. Hii Tanzania ya utalii tukianza kukamatana kwa kuvaa miniskir na staili ya nywele, wageni na watalii nao tutawakamata kwa mitindo yao ya kuvaa na nywele, au kwa sababu tunataka wao wajivunze kwetu tutawaacha?

Hii serikali sasa inaonekana imekosa focus. Imekuwa ikitapatatapa na kurukia mambo bila kufikiri.
tanzania ni nchi pekee yenye wajuaji wasicho kijua
hao ndio watanzania
 
Wee vaa tu vazi lako, nyoa upendavyo: your dress your choice hakuna wa kukubabaisha
 
Mambo ya "fent fort" tu! Mambo ya hovyo hovyo ndio wanayapa kipaumbele lakini ya msingi wananyamaza na wala hawataki yajadiliwe kwa kuyabatiza "uchochezi".

Kwangu wanazidi kuthibitisha kuwa wamefeli vibaya kwenye kuongoza nchi na/au kuleta maendeleo.
 
Mkuu hebu tulia
Wengine ndio tunapenda kuangalia hizo mini skirt kusudi tuchague vizuri,
Hebu tafadhali hili suala la nguo fupi serikali itulie tu.
Serikali ituachie vitu vyetu maana baada ya vyuma kukaza,minskirt no ni grisi ya bongo zetu jamaa!
 
Back
Top Bottom