Mariupol yaanguka, ushindi wa kwanza mkubwa wa Urusi

Muda mfupi uliopita Urusi imesema jiji la bandari na viwanda la Mariupol limeingia mikononi mwao kikamilifu baada ya kusafisha mabaki ya askari wa Ukraine waliokataa kujisalimisha waliokuwa wamejichimbia kwenye kiwanda kikubwa cha kufua chuma.

Askari hao pamoja na kuishiwa chakula na silaha walikuwa na uzalendo mkubwa na nchi yao na kwa kutiwa moyo na viongozi wao waliendelea kuleta upinzani mkali kwa jeshi la Urusi mpaka pale waliporushiwa makombora mazito mfululizo yaliyowafikia walipojificha na kukigeuza kiwanda hicho kuwa majivu kama ilivyothibitishwa na Reuters.

Mafanikio hayo makubwa ya Urusi yameitikisa Ukraine yote na kupelekea nchi hiyo kutoa tangazo la kusitisha kusafirisha kwenda nje ya nchi nafaka na vyakula vyote. Maelfu ya tani ya nafaka yalikuwa yamekwama kwenye bandari ya Mariupol hivyo kauifanya Ukraine kujaribu kusafirisha nafaka kibiashara kupitia kaskazini ya nchi hiyo kabla ya kutolewa tangazo la katazo hilo.

Jiji zuri la Kyiv nalo linaendelea kuwaka moto.

View attachment 2190254
For the Great Mother Russia
 
Hiyo Moriopol Russia wamekuwa wakitangaza mara kadhaa upo chini yao lakini Ukraine wanakataa
Kama umesikiliza vilio vya raisi Zelensky sasa utakubaliana na Urusi kuwa Mariupol ipo chini yao.Anachobembeleza Zelensky ni kuwa hao askari wake waliobaki wasiuliwe.Anatishia ikiwa watauliwa basi mazungumzo na Urusi itakuwa basi. Hoja zake hazina maana kama hajawaamrisha wajisalimishe.Na atakachokifanya Mrusi kwao basi asilaumiwe.
 
Maneno ya Meya wa Mariupol baada ya mji kuanguka"Nasikia warusi wanajisifia kukamata mji wa Mariupol,wameuwa watu zaidi ya elfu 10 na kubomoa asilimia 95 ya majengo yote.sasa hapo kuna mji gani wa kuchukua,mji usiokuwa na watu wala majengo"

Haya ni maneno ya mkosaji
Nyie warusi kwa kutunga habari hamjambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno ya Meya wa Mariupol baada ya mji kuanguka"Nasikia warusi wanajisifia kukamata mji wa Mariupol,wameuwa watu zaidi ya elfu 10 na kubomoa asilimia 95 ya majengo yote.sasa hapo kuna mji gani wa kuchukua,mji usiokuwa na watu wala majengo"

Haya ni maneno ya mkosaji
Ni utamaduni wa kisoviet kuharibu miji

Bado kievu hua wakiondoka wanaacha Ghost city muwakumbuke vizuri ni Russian War culture...
 
Back
Top Bottom