PostGE2025 Maridhiano ya Kitaifa: Ni baina ya nani na nani?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,974
Reaction score
9,376
Nataka kuelewa kuhusu haya maridhiano ya Kitaifa yanayozungumzwa sana.

Maaridhiano haya ni baina ya nani na nani? Kama ni ya Kitaifa swali langu "Kwani kuna mgogoro au kutoelewana baina ya nani na nani?"

Serikali haielewani na Wananchi?, ni baina ya Dola na Wananchi? ni Vyama vya siasa? Au tunataka kuridhiana juu ya kitu gani na kwa nini? Wadau wa maridhiano haya wanatokana na tatizo gani?

Maana tumewahi kuona maridhiano baina ya CCM na Chadema na wakawekeana masharti. Pia majuzi tu kulikuwa na maridhiano ya Serikali ya Zanzibar wanajua wao hoja na madai yalokuwepo.

Hata maridhiano baina ya Marekani na Iran ni kwa sababu kuna vita baina yao ili kupata suluhu wanawekeana masharti.

Sisi Tanzania tunataka maridhiano ya Kitaifa kufuatia nini na kwa matumaini gani? Kuna jambo au mgogoro gani unaohitaji maridhiano baina ya wahusika? Mimi sielewi naomba kuelimishwa.

Maasalaam
 
Kuna watu na chama chako cha Chadema baada ya kuona mambo hayaendi ndio wanazua mambo eti kuwepo maridhiano. CCM imepigiwa kura nikiwemo mimi na watu zaidi ya asilimia tisini ya wapiga kura. Unasemaje watu wanataka maridhiano nchi haiendi?

Leo ukitangaza Watanzania wanaotaka maridhiano waende mfano uwanja wa CCM Kirumba, hawatazidi watano! Halafu eti mtu anasema nchi inahitaji maridhiano! Pumbavu!!
 
Wewe unaishi Tanzania hujui hata kilichotokea October 29 ukuona hata kuskia kwa watu kwenye redio za nje au Rais siku anazindua Bunge anasimamisha Bunge kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu ulikua una Umri gani? Wakati tume zinaindwa ulikua bado mdogo?
 
Kuna watu na chama chako cha Chadema baada ya kuona mambo hayaendi ndio wanazua mambo eti kuwepo maridhiano. CCM imepigiwa kura nikiwemo mimi na watu zaidi ya asilimia tisini ya wapiga kura. Unasemaje watu wanataka maridhiano nchi haiendi?

Leo ukitangaza Watanzania wanaotaka maridhiano waende mfano uwanja wa CCM Kirumba, hawatazidi watano! Halafu eti mtu anasema nchi inahitaji maridhiano! Pumbavu!!
Hujanitendea haki, mimi nauliza swali kama wewe unalo jibu hayo matusi ya nini sasa?

Nambie maridhaino wanayozungumzia viongozi mpaka rais Samia ni maridhiano ya nani na nani na kwa lengo gani?
 
Nataka kuelewa kuhusu haya maridhiano ya Kitaifa yanayozungumzwa sana.

Maaridhiano haya ni baina ya nani na nani? Kama ni ya Kitaifa swali langu "Kwani kuna mgogoro au kutoelewana baina ya nani na nani?"

Serikali haielewani na Wananchi?, ni baina ya Dola na Wananchi? ni Vyama vya siasa? Au tunataka kuridhiana juu ya kitu gani na kwa nini? Wadau wa maridhiano haya wanatokana na tatizo gani?

Maana tumewahi kuona maridhiano baina ya CCM na Chadema na wakawekeana masharti. Pia majuzi tu kulikuwa na maridhiano ya Serikali ya Zanzibar wanajua wao hoja na madai yalokuwepo.

Hata maridhiano baina ya Marekani na Iran ni kwa sababu kuna vita baina yao ili kupata suluhu wanawekeana masharti.

Sisi Tanzania tunataka maridhiano ya Kitaifa kufuatia nini na kwa matumaini gani? Kuna jambo au mgogoro gani unaohitaji maridhiano baina ya wahusika? Mimi sielewi naomba kuelimishwa.

Maasalaam

Gentleman,
maridhiano ya hiyari ya kitaifa miongoni mwa waTanzania wote, yanalenga kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote. Full stop.🐒
 
Bado sijaelewa mkuu, Kama Maridhiano ya Kitaifa yatahusu Katiba Mpya na wadau ni sisi sote unadhani litawezeshwa vipi yaani?

Najaribu kufikiri kama hojanni Katiba Mpya tunaanzia maridhiano baina ya nani na nani maana Serikali haiwezi wafikia wananchi wote
 
Nimekusoma lakini wanasema kuwa huo muswada unaandikwa kwa mujibu wa pande mbili, hizo pande ni zipi?

Kilitokea nini mpaka imefikia hizo pande mbili hazielewani?

Kifupi, nijuze hizo pande mbili kama unazijua pengine naweza hisi kilitokea nini mpaka tumefikia hatia hii
 
Bado sijaelewakuu, Kama Maridhiano ya Kitaifa yatahusu Katiba Mpya na wadau ni sisi sote unadhani litawezeshwa vipi yaani?
Najaribu kufikiri kama hojanni Katiba Mpya tunaanzia maridhiano baina ya nani na nani maana Serikali haiwezi wafikia wananchi wote
my friends, ladies and gentlemen,

kuna baadhi ya wadau wa Jf wamepumbazwa au kupitoshwa na dhana potofu ya kwamba, eti maridhiano ya hiyari ya kitaifa miongoni mwa waTanzania, eti sijui yanalenga kutibu sijui nini huko wanajua wao wenyewe kadiri wanavyopotoshana,

but ukweli ni huu,
na chukua hii na uishi nayo,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote yanalenga kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote na si vinginevyo. Maelezo zaidi au tofauti na hayo itakua ni porojo tu gentleman 🐒
 
Maridhiano ni hali ya kufikia makubaliano, maelewano, au suluhu kati ya pande mbili au zaidi zilizokuwa na mivutano, tofauti za kimaoni, au migogoro. Kwa Kiingereza, neno hili hutafsiriwa kama reconciliation au compromise.
Hizo pande mbili ni zipi? Na kulitokea nini? Sijui kama mnanielewa!
 
my friends, ladies and gentlemen,

kuna baadhi ya wadau wa Jf wamepumbazwa au kupitoshwa na dhana potofu ya kwamba, eti maridhiano ya hiyari ya kitaifa miongoni mwa waTanzania, eti sijui yanalenga kutibu sijui nini huko wanajua wao wenyewe kadiri wanavyopotoshana,

but ukweli ni huu,
na chukua hii na uishi nayo,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote yanalenga kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote na si vinginevyo. Maelezo zaidi au tofauti na hayo itakua ni porojo tu gentleman 🐒
Tutaridhiana mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kutoelewana pande mbili yaani wanaopinga na wanaotaka Katiba Mpya?

Hizi pande mbili ndio zinanipa shida Je, ni watu, ni chama, ni taasisi maana kila anaye zungumza anasema tunataka Katiba Mpya. Kina nani wasoitaka mpaka tufanye nao maridhiano?
 
Gentleman,
maridhiano ya hiyari ya kitaifa miongoni mwa waTanzania wote, yanalenga kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote. Full stop.🐒
Hujajibu swali chawa mjinga.

Maridhiano ya hiyari kati ya nani na nani?
Akina nani wanaridhiana? Zanzibar wameridhiana CCM na CCM B or sorry na ACT wazalendo. Huo uimara wa msingi kwani umetetereka?
 
narudia tena,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote yanalenga kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote na si vinginevyo. Full stop 🐒
 
Kwa hiyo maridhiano yanahusiana na mauaji ya October 29? Yatawahusu kina nani haswa!

..maridhiano huko awali kabla ya uchaguzi yalihusu mazungumzo yatakayopelekea makubaliano ya jinsi ya kuandika Katiba Mpya.

..Sasa hapo katikati Ccm wamechezea amani ya nchi na kupelekea mauaji ya watu 518 wakiwemo WATOTO.

..Kuna tukio kule Mwanza vijana wa soka academy waliuwawa kinyama bila makosa yoyote. Sio kwamba walikuwa barabarani, bali walifuatwa ktk eneo walipokuwa.

..Kutokana na haya mauaji Ccm inataka kutumia maridhiano kujisafisha. Sasa hivi wanasema mchakato wa Katiba lazima utanguliwe na maridhiano.

..Pia Ccm wameunda Tume ya uchunguzi ambayo itawafuatilia waliohusika kuandaa maandamano. Waliofanya mauaji hawatabugudhiwa.

..Baada ya kuwabaini walioandaa maandamano hao sasa ndio watatumika kama chambo kwamba wamesamehewa kupitia maridhiano, na hivyo suala la mauaji ya OCT 29 litakuwa limefungwa rasmi.
 
Back
Top Bottom