Nchi ni watu ndiyo, lakini si kwa muktadha ambao unaouelezea. Kwa muktadha ni kwamba: Nchi ni eneo la nchi kavu lililokusanya jamii ya watu wanaoishi na lenye mipaka yake, na hujulikana kama Taifa.
Raia mmoja mmoja anafanya jumla ya Taifa(nchi) kwa maana yeye ni sehemu ya nchi. Lakini haimaanishi ukimuona raia wa nchi fulani basi yeye ni nchi, yeye ni muwakilishi (balozi)
Tafsiri ya kusema nchi ni raia ina maana haiwezekani kukawa na nchi bila kuwepo watu, na watu ndiyo wanaobeba nembo ya kuitwa Taifa ikiwa ni pamoja lenye mipaka yake ya ardhi.
mbalaka said:
"Mkuu nchi ni watu, Nyerere aliingiza nchi vitani, sio kwamba Amini alikanyaga Ardhi ya Tanzania, bali Aliua watanzania wakagera."
Isikilize Speech ya Nyerere alipotangaza vita na Amini wa Uganda alisema; "Amini ametufanyia kitendo cha jeuri, cha fedheha na cha kuvunja sheria za kimataifa. Amevamia nchi yetu! Amekalia eneo la nchi yetu na amelitangaza kwamba sasa ni eneo la Uganda!...."
Na kazi kuu ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi. Hiyo ndiyo kazi kuu, mahali popote Duniani hiyo ndiyo kazi kuu ya Jeshi.
Nchi ni nini sasa?
Alichokifanya Amerika ni kumvamia na kumshambulia na kumua muwakilishi wa kijeshi mwenye hadhi ya juu kwa Taifa la Iran akiwa nje ya mipaka yake ya nchi, ambaye ni raia wa Iran, ni mmoja wa muwakilishi wa Taifa. Kwa sababu tu US ana utofauti nao wa kisiasa na Taifa la Iran.
Ni kitendo cha hatari! Ni kitendo cha uvunjifu wa sheria ya kimataifa, na ni kitendo cha uvunjifu wa sheria za nchi yenyewe ya Marekani. Bunge la US limelaani hicho kitendo! Pentagon mapema wakajivua gamba, kwamba ni amri ya rais na siyo matashi yao.
Athari yake ni kubwa! Kwa sababu viongozi wa kisiasa wakisafiri kwenda nchi nyengine itakuwa ni mchezo wa kuwindana kwa sababu tu ya utofauti wa kisiasa. Ndiyo maana US amewataka raia wake wakimbie huko Iraq mapema.
Kwa hiyo, Iran haiwezi ikatangaza vita ya kuvamia mipaka ya ardhi ya Amerika! Vita watakayoitangaza ni wao watalipiza kisasi. Hii ni hatari! Watalipiza kisasi kwa kiongozi yupi wa Marekani mwenye hadhi ya juu? Time will tell. Kwa sababu ni mchezo wa kuviziana huu.