Marekani yaruhusu Ukraine kupewa Ndege Vita

Marekani yaruhusu Ukraine kupewa Ndege Vita

Mie napenda Ukraine apewe siraha nzito nzito kwa kiwango kile kile anachotumia Russia, ikiwezekana hata Meli vita na nyambizi apewe. Haiwezekani upambane na mtu mwenye bomu huku wewe unatumia fimbo. Ili litafanya uwanja ubalance
 
Atamwadhibu kwa lipi...hzo f16 50 au kuna lingine..??...yaani ktk hii vita Wazungu nimewaona nao ni kama ngozi nyeusi tu ktk kufikiri wanachotuzidi Mungu aliwapendelea maarifa yakaanzia kwao...lakini ni bure kabisa nao...!!!...hv kwa nguvu ya Jeshi la Urusi.. hzo f16 zitasaidia nn..?.. hata wangepewa 100...nn kitaenda kubadilika..??...yaani mpaka hapa hakuna namna yoyote ya wao kushinda hii vita...ni kupoteza roho za askari tu buree yaani...!!!...na kwa jinsi Russia anavyopata wakati mgumu wa kudeal na issues kama hz ndio huko mbeleni itakuwa ngumu sana kusuluhisha huu ugomvi....!!! ngoja tuona akili za mzungu wa West na East...nani atakaeshinda hii vita..!!!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Sasa hili nalo Neno.
Taifa la Urusi lipo tiari KUPAMBANA na US plus Nato direct. Hapa zitumike f16, f22, f35 na helcopiter zote na nyambizi zote, Meri Vita, makombora yote na mabomu, siraha za sumu n.k Sijuhi nuklia.
Sasa hizo F16 ndio nini? Wakati Uturuki wanazo na zimekwisha fanyiwa upembufu wa kinifu zinasubiriwa tu ziingie angani ama mafichoni zidunguliwe hata kabla hazijapaa. Ni Wajinga wa kwanza.
 
Hakuna cha uvamizi wala nini siju, mabeberu ndio walikuwa wameweka mikakati kabambe kwa kutaka kuitumia Ukraine militaty and some NATO troops ili kushambulia by all means kusini mashariki mwa Ukraine, Crimea, Sevaspotol possibly na Russian Federation - baadae waje kupenyeza magaigi ili waweze kuanzisha masula ya ugaidi kama walivyo fanya nchini Syria.

Mabeberu wana fund na ku-arm Ukraine military/magaidi for a good reason namely her vast Natural resources za Urusi ndio zinafanya nchi za magharibi watake Urusi isambaratike - ni wivu tu na wala si kitu kingine - Uzuri Urusi inazielewa sana njama zote za magharibi na haitaruhusu hata njama moja kutekelezeka, mabeberu wataishia kwenye ngonjera na maazimio yao basi - lakini kujitia kupigana vita ya ana kwa ana na Urusi - ujasiri huo mabeberu hawana kabisa.
Siku wakidhubutu nahisi Mataifa Kama UINGEREZA, UJERUMANI, Poland, UFARANSA zitafutika hata kabla ya masaa 24
 
Mpaka sasa hawaulizi hao rafiki kwanini wampe siraha za kupiga ardhi yake mwenyewe, kwa lugha nyingine anakubari kushirikiana na Urusi kuharibu miundo mbinu zake mwenyewe. Kwa hali hiyo ushindi atatoa wapi?. Yaani hapo ni sawa na Mandonga awe anarusha ngumi anajipiga harafu ategemee kudhinda

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Kichwa kigumu sana wewe, hapo nikwamba mrusi kaingia ndani yanchi ya Ukraine amejichukulia maeneo kwaio hawa nato wanamsaidia kupambana nahuyo mvamiz wampige asepe, sasa unataka wapewe missile zakupiga Moscow huko zanin wakati adui yupo ndan kwao
 
Rais wa Marekani, Joseph Biden akiwa Japan kwenye mkutano wa G7 amesema ametoa ruhusa na atashirikiana na nchi zingine kuwafundisha Marubani wa Ukraine matumizi ya ndege vita aina ya F16.

Hapo jana Pentagon ilisema kuwa wanajeshi wa Ukraine walioenda kwa ajili ya mapitio juu ya uwezo wa kuongoza ndege hizo wanaweza fanikiwa kwa miezi 4 ambayo ni tofauti na miezi 18 kwa wanajeshi wengine.

Hivyo basi baada ya tamko na ruhusa hiyo, nchi za Netherlands, Norway watatoa ndege na mafunzo kwa wanajeshi anga wa Ukraine.
Inakadiriwa Ukraine watapewa ndege 50
Wanaongopa wanajeshi wa UKRAIN wakati kuna wanajeshi wao ndio wanapigana na hata hizo ndege kwa mda mfupi huo itakua wanajeshi wa Nato ndio wanaziendesha
 
Atamwadhibu kwa lipi...hzo f16 50 au kuna lingine..??...yaani ktk hii vita Wazungu nimewaona nao ni kama ngozi nyeusi tu ktk kufikiri wanachotuzidi Mungu aliwapendelea maarifa yakaanzia kwao...lakini ni bure kabisa nao...!!!...hv kwa nguvu ya Jeshi la Urusi.. hzo f16 zitasaidia nn..?.. hata wangepewa 100...nn kitaenda kubadilika..??...yaani mpaka hapa hakuna namna yoyote ya wao kushinda hii vita...ni kupoteza roho za askari tu buree yaani...!!!...na kwa jinsi Russia anavyopata wakati mgumu wa kudeal na issues kama hz ndio huko mbeleni itakuwa ngumu sana kusuluhisha huu ugomvi....!!! ngoja tuona akili za mzungu wa West na East...nani atakaeshinda hii vita..!!!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Yani hizo ndege 50 zikipigwa zikiisha Nato watakua uchi, hakuna namna watakimbilia kwenye vikwazo maana cjui watatuma silaha gani tena zaidi maana wanatoa silaha zingine wanaweka akiba kwa usalama wao kama patroit ishapigwa mfumo gani tena watajidai nao kwa usalama wao
 
toka mwanzo nato wamekuwepo ukraine, wanajeshi wa ukraine walishapotea, saizi ule ni uwanja kati ya nato na russia,.....

acha waendelee, atakayechoka atanyoosha mikono juu
Ata jeshi la Tanzania ingeingia vita na Russia wasingeweza kumalizwa kama unavyodai kwa upande wa Ukraine.
Labda kama hujui maana ya vita, kwanza elewa hakuna nchi inakuwa na wanajeshi wake wote ndani ya nchi...wengine wanakuwa nje ya nchi au nje ya mfumo wa jeshi.
Mengine ni stories zenu za kujifurahisha tu.
 
Russia amekuwa na mkakati wa kujitanua kwa kutwaa maeneo ya Ukraine ili yawe yake lakini hilo halitawezekana kabisa kwani hakutakuwa na amani kwenye maeneo hayo kama wanavyofikiri.
Sio mkakati hiyo ni vita kati ya magharibi na Urusi kwahiyo UKRAIN kaamua kutoa eneo lake ndio litumike kupimana ubavu wababe hao ila kwa siraha za kawaida tu na ndio maana kila upande unamkumbisha mwenzake isitumie siraha za nyuklia . kwahiyo rais wa UKRAIN katoa uwanja wacha watu wapimane ubuvu kwa technology
 
Washaamua liwalo na liwe.

Hatimaye Marekani kapata sehemu sahihi ya kumuadhibu Urusi

Syria wameshindwana
Libya haikuwezekana


Sasa wamekutana
Ndio; Uso kwa uso ; jino kwa jino; naniliu na nanihii -patachimbika. 💪 💪
 
Huwezi toa tech isiyo yako bila ruhusa ya mtengenezaji
Acha uongo wewe. Kwani aliwagawia? Si walinunua? Ikumbuke walinunua products na sio tech ya namna ya kutengeneza. Yaani uniuzie bunduki alafu nisubiri ruhusa yako kumshambulia mtu akinitisha kuniua au akinivamia?????? Hebu katafute wa kuwadanganya plz
 
Sio mkakati hiyo ni vita kati ya magharibi na Urusi kwahiyo UKRAIN kaamua kutoa eneo lake ndio litumike kupimana ubavu wababe hao ila kwa siraha za kawaida tu na ndio maana kila upande unamkumbisha mwenzake isitumie siraha za nyuklia . kwahiyo rais wa UKRAIN katoa uwanja wacha watu wapimane ubuvu kwa technology
Siraha X Silaha ✓ Labda kama unaandika kikurya.
 
Acha uongo wewe. Kwani aliwagawia? Si walinunua? Ikumbuke walinunua products na sio tech ya namna ya kutengeneza. Yaani uniuzie bunduki alafu nisubiri ruhusa yako kumshambulia mtu akinitisha kuniua au akinivamia?????? Hebu katafute wa kuwadanganya plz
Hapana mkuu, HIMARS yupo sahihi. Kinachozungumziwa ni ile technolojia ya utengenezaji siri za kiufundi. Wewe ukiwa ni mlaji tu hakuna shida llakini huruhusiwi kuunda wala kufanya biashara au kuwa mzembe kiasi. Sasa inapokuwa ni suala la silaha Manufacturer anakuuzia lakini kwa sharti la kutoku-expose siri za utengenezaji wake. Ndo mana e.g. Mrusi anaziwinda sana HIMARS ili walao apate ni Tech. gani iliyotumika kuitengeneza. NATO naye aliokota na kupeleka maabara mabaki ya kombora lililodaiwa kuwa ni Kinzhali.
Kwa maneno rahisi unasikia kwa mafano magari ya Toyota yanatengenezwa South Africa under license(i.e. yanatengenezwa kwa Kibali), Cocacola hata Tz tunatengeneza kwa kibali lakini siri yake kiufundi hatuijui.
 
Mpaka sasa hawaulizi hao rafiki kwanini wampe siraha za kupiga ardhi yake mwenyewe, kwa lugha nyingine anakubari kushirikiana na Urusi kuharibu miundo mbinu zake mwenyewe. Kwa hali hiyo ushindi atatoa wapi?. Yaani hapo ni sawa na Mandonga awe anarusha ngumi anajipiga harafu ategemee kudhinda

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Jifunze basi kuandika maneno ya kiswahili vizuri, mbona unaandika kikurya sana muraa.
 
Back
Top Bottom