Bahati mbaya sana Dunia inapambaa na kitu wasichokijua, kwani stage ya kwanza kupambana na kitu chochote kwanza ni kukijua kuanzia mienendo yake na wao ni kina nani kutofautisha na wengine, cha kushangaza mpaka leo DUNIANI hakuna tafasiri moja inayoelezea Gaidi ni nani zipo zaidi ya tafasiri 15 ambazo zinaelezea gaidi ni nani lakini wataalamu wa maswala ya matukio ya mashambulizi ya kustukiza na yenye kuleta hofu wameshindwa kukubaliana maana sahihi ya UGAIDI na GAIDI ni nani na wanaposhindana ni vigezo vipi vinatumika kumuita mtu gaidi? au ni vigezo gani vinatumika kumtoa mtu kuitwa gaidi? mfano wapigania Uhuru wote (freedom fighter) walikuwa wanaitwa magaidi mfano Mandela lakini kwa waafrica tulikuwa tunamwona kama mpigania uhuru na haki za waafrica weusi nchini South Africa lakini makaburu na wazungu walikuwa wanamuona ni Gaidi na aliwekwa mpaka kwenye list ya Magaidi Duniani amekuja kufutwa kwenye list tena mmoja wa viongozi wakuu Duniani Margaret Thatcher aliwai kumuita Mandela na ANC kuwa ni “typical terrorist" haya kuna nchi duniani zinavamia nchi zingine na kufanya mauaji ya kinyama mfano Israel wanavyofanya kwa watoto wa kiparestna je hule ni nini?
Leo kundi la (ISIS) inasemekana wanapata ufadhiri kutoka US sasa unajiuliza hawa magaidi na hawa wapinga ugaidi wana mpango gani tena? nadhani ni wakati sahihi ktk kupambana na ugaidi na magaidi duniani siku wapambana na ugaidi wakiwa serious kupambana na ugaidi tutapata tafasiri moja ya ugaidi ni nini na gaidi ni nani na wote tutajua tunapambana na nani na nina uhakika ugaidi utakuwa history kama ilivyokuwa ucominist