chikanu chikali
JF-Expert Member
- Aug 29, 2017
- 1,141
- 1,826
Kama ni kweli basi Mungu awabariki sana marekaniNimetoka kuongea na rafiki yangu anafanya ubalozi wa marekani hapa nchini ananiambia huu mwaka wa uchaguzi tuombe Mungu maana " mabeberu " wametupania hasa kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba unakuwa huru na uwazi .
Wanataka kuhakikisha vyama vyote vya siasa vinapata uwanja sawa wa kushiriki kampeni za uchaguzi na zoezi zima la upigaji kura na utangazaji wa matokeo.
Sasa nimejiuliza tuu binafsi kwa figisu figisu ambazo chama tawala CCM wamezoea kucheza kwenye uchaguzi kweli tutapona.
Nimeambiwa hata baadhi ya matamko yanayotolewa na serikali ya marekani siyo wanabahatisha ni kwamba tayari "move" imeanza ili kutafuta sababu za kuweza kutunyoosha.
Sasa lengo la mimi kuandika hapa ni kuitahadharisha serikali ya CCM chonde chonde msije mkatuingiza kwenye machafuko.