Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Umaarufu wa rais wa Marekani Joe Biden umepungua kwa asilimia saba na kufikia kiwango chake cha chini baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan, kulingana na uchunguzi wa Shirika la Habari la Reuters / Ipsos.
Baada ya mahojiano yaliyofanywa na raia kadhaa wa Marekani siku ya Jumatatu, uchunguzi unaonyesha kuwa Wamarekani 46% tu ndio wanampenda rais wao, kiwango cha chini kabisa tangu Joe Biden aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu.
Umaarufu wa Joe Biden umepungua wakati Taliban iliteka mji mkuu mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kufuta miongo miwili ya uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo.
Hata hivyo hivi karibuni Joe Biden alitetea maamuzi yake na kusema kuwa hajutii maamuzi ya kuwoandoa wanajeshi wa taifa hilo nchini Afghanistan.
Joe Biden amekuwa akikosolewa ndani na nje ya chama chake cha Democratic kufuatia uamuzi wake wa haraka wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.