Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 559
Katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari leo jijini dodoma...Kaimu balozi wa Marekani ametoa tamko la Serikali ya Marekani juu ya Hali ilivyo kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini kwa kumpiga kijembe waziri wa mambo ya nje Prof. Kabudi kwa kusema
"Uhuru wa vyombo vya habari haupimwi kwa idadi ya machapisho yanayodai kuwa kuna Uhuru huo, bali ni kwa kutoa ripoti na Tafiti pamoja na habari za kuaminika.
Ikumbukwe kwamba wiki hii waziri kabudi alitembelewa na ujumbe wa marekani ofisini kwake na katika kuthibitisha kuwa kuna uhuru wa vyombo vya habari nchini, alitoa rundo la magazeti (Kama inavyoonekana pichani ) na kuwaonyesha akidai vyombo hivyo vina uhuru.
Swali ni je walikusanya na magazeti waliyoyafungia kwa kuandika habari nyeti za kumkosoa jiwe na serikali yake?....Je walihusisha pia magazeti yenye ripoti za kutoweka kwa waandishi kama Azory Gwanda?!