Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,738
- 15,211
Kesi iliyofunguliwa na jopo la Wanasheria wazalendo kule Mbeya kupinga mkataba wa bandari kila mtanzania ana hamu ya kufahamu nini kitaendelea mahakamani katika kesi hiyo, lakini cha kushangaza media za hapa bongo zimekaa kimya kabisa na kinafiki, si redio wala gazeti linaloripoti kuhusu kesi hiyo.
Mikutano ya Chadema na Sauti ya wazalendo licha ya kwamba waandishi wa magazeti na redio wanakuwepo kwenye mkutano lakini hawaruhusiwi kuandika chochote kuhusu mikutano hiyo! Je hapo utajisifu kwamba kuna uhuru wa vyombo vya habari Tanzania?
Nape Nauye kazi yako ya kuuwa vyombo vya habari imeonekana endelea hivyo hivyo kuhubiri mdomoni kuna uhuru wakati kivitendo ni tofauti kabisa.