Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 925
- 1,954
Mia Love, mbunge wa kwanza mwanamke mweusi wa chama cha Republican nchini Marekani amefariki akiwa na umri wa miaka 49 huko Utah, imetangaza familia yake.
Taarifa hiyo imesema, aliaga dunia kwa amani siku ya Jumapili, akiwa amezungukwa na familia nyumbani kwake huko Saratoga Springs.
Love, mtoto wa wahamiaji kutoka Haiti, alikuwa mbunge wa jimbo la Utah katika Bunge la Marekani.
Binti yake Abigale alisema mapema mwezi huu kwamba Love alikuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya ubongo.
Maisha ya kisiasa ya Mia Love yalianza rasmi mwaka 2003 aliposhinda kiti katika baraza la jiji la Saratoga Springs, na baadaye akawa meya akiwa na umri wa miaka 34.
Mwaka 2014, alichaguliwa kuwa mbunge katika Bunge la Marekani na kuweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi wa chama cha Republican kuchukua nafasi hiyo, na alihudumu kwa mihula miwili.