Marekani - Makampuni makubwa yafilisika yafunga store 54 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani - Makampuni makubwa yafilisika yafunga store 54

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Candid Scope, Dec 30, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Florida hit hardest by Sears store closings
  • Florida to lose 11 Sears or Kmart stores; Ohio, Michigan and Georgia will lose 6
  Florida will be hit the hardest by the closing of Sears and Kmart stores, losing 11, according to a preliminary list of 79 planned closures released Thursday. Ohio, Michigan and Georgia are not far behind with six store closures planned in their states. Tennessee, North Carolina and Minnesota are set to lose four stores each.

  A spokeswoman for Sears Holding Corp. said each store employs between 40 and 80 people.
  None of the closures announced so far are in Sears' home state of Illinois. The 125-year-old retailer said on Tuesday it would close up to 120 stores to raise cash.


  The projected closings represent only about 3 percent of Sears Holdings' U.S. stores. Sears and Kmart merged in 2005. The company now has about 3,560 stores in the U.S. That's up from 3,500 immediately after the merger.


  Here is the list of closures announced so far http://www.searsmedia.com/tools/122711_close.pdf :

  — Alabama (3): Sears in Mobile; Kmart in Auburn and Gadsden.
  — California (3): Sears in El Monte and San Diego (2).
  — Colorado (3): Sears in Longmont; Kmart in Broomfield and Glenwood Springs.
  — Florida (11): Sears in Crystal River, Deland, Port St. Lucie, Stuart, West Palm Beach; Kmart in Callaway, Fernandina Beach, New Smyrna Beach, Orange City, Pompano Beach and St. Augustine.
  — Georgia (6): Sears in Macon; Kmart in Atlanta, Buford, Columbus, Douglasville and Jonesboro.
  — Idaho (1): Sears in Lewiston.
  — Indiana (3): Sears in Anderson; Kmart in Indianapolis and St. John.
  — Iowa (2): Kmart in Cedar Rapids and Davenport.
  — Kansas (1): Sears in Lawrence.
  — Kentucky (3): Sears in Middleboro; Kmart in Hazard and Winchester.
  — Maryland (1): Sears in Ellicott City.
  — Michigan (6): Sears in Adrian, Brighton, Chesterfield Township, Harper Woods, Monroe and Washington Township.
  — Minnesota (4): Kmart in Duluth, New Hope, White Bear Lake and Willmar.
  — Mississippi (3): Sears in Columbus, Jackson and McComb.
  — Missouri (2): Sears in Lee's Summit and St. Louis.
  — New Hampshire (2): Sears in Keene and Nashua.
  — North Carolina (4): Sears in High Point, Morehead City, Rocky Mount and Statesville.
  — Ohio (6): Kmart in Chagrin Falls, Columbus, Medina, Springfield and Toledo (2).
  — Oregon (1): Sears in Roseburg.
  — Pennsylvania (2): Sears in Pottstown and Upper Darby.
  — South Carolina (1): Sears in Sumter.
  — Tennessee (4): Sears in Antioch, Cleveland, Oak Ridge; Kmart in Hendersonville.
  — Virginia (3): Sears in Norfolk; Kmart in Midlothian and Richmond.
  — Washington (2): Sears in Walla Walla; Kmart in Lacey.
  — Wisconsin (2): Sears in West Baraboo; Kmart in Rice Lake.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  tatizo ni nanai?Obama?
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uchumi wa dunia bado haujasetirika, madhara ya kuyumba uchumi duniani yatachukua muda mrefu sana.
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Bila shaka Cameron & Obama wakikiri mbele ya huyu MUNGU aliyehai kwmb wana makosa na utawala wao hakika uchumi itaimarika mara moja.

  Eti NDOA ya mtu mmoja! NA WALAANIWE!
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  hawa waZungu ni wajanja sana,

  - ulaya pamoja na marekani wanatumia zile mbinu za wakati wa vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia
  - hawa watawala wakisha ona mambo kwenye nchi zao ni magumu watu hawana ajira, makampuni ya filisika wao wanacho kifanya ni kuanzisha kitu kingine ili wananchi wahamishe mawazo yao kutoka kwenye kulia hali mbaya ya uchumu wahamie kwenye maada zingine

  - waliona mabo yamkekuwa magumu wakavamia libya, hapo ni ili wanachi wabaki kujadili vita na maswara ya uchumu yawekwe pembeni

  - sasa hivi hali inavyo endelea wanataka kuipiga irani au sylia hayo yote wao wanataka kujiokoa na wanachi wao

  hawa wako tiyali kutengeneza tukio kubwa sana ambalo litabadili muelekeo wa mazungumzo ya wanachi wao

  ni wajanja sana, wanaweza hata tafuta magaidi walipue majengo yao ili wanachi wabadili mazungumzo
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Jaribu kunyoosha zaidi maana duh umezungumza mambo wengine hayaamini sana.
   
 7. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo Obama, haya mambo yalianza kuonekana toka mwishoni mwa uraisi wa Clinton.

  Utamaduni wakununua na kutupa uliokuwepo marekani kwa takriban miaka 40 kwa sasa unatoweka. Kwahiyo makampuni yaliyotajirika kwa kufyatua bidhaa sasa hivi yanafilisika kwa kutopata faida.

  Watu wengi wamekuwa masikini kwa kukosa kazi kwasababu kazi za viwandani zimepungua kwahiyo watu hawana pesa za ziada za matumizi. Mishahara pia haijaongezeka kihivyo kulinganisha na gharama za maisha ya sasa kwahiyo kile kidogo wanachopata wanakitumia katika vitu muhimu tuu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Ni kweli hali ya maisha ya taifa la Marekani ni ngumu kwa wananchi walio wengi, na dalili ni kufungwa kwa biashara nyingi kutokana na kujiendesha kwa hasara kufikia kiwango cha kufilisika. Hata viwanda vya uzalishaji kwa sasa vimepunguza sana wafanyakazi kutokana na kupunguza shift za kazini kutoka 24 hr hadi 16 hr na nyingine zimefikia hatua ya 8 hr tu.

  Hali hii imetokana na hali ya nguvu za uchumi duniani kuanza kuhamia bara la Asia kwa kasi, hivyo nchi za ulaya na marekani kuwa katika wakati mgumu wa kiuchumi. Watatoa visingizio vingi lakini ukweli ndio huo. Ukiona sasa mataifa ya bara la Asia uchumi unakua kwa kasi sana wakati bara la Ulaya na Marekani wanalalamikia hali nguvu ya uchumi, historia inajieleza, ndivyo roman empire ilivyofilisika na nchi nyingine za ulaya kujiimarisha. Ndivyo ilivyo Ulaya na Marekani uchumi wake unapolegalega ndipo mwanya wa nchi za bara la Asia zinapojiimarisha kujenga nguvu za uchumi duniani.

  Marekani sasa si nchi ya uzalishaji, bali ni nchi ambayo ni soko la bidhaa za bara la Asia, hali kadhalika bara la Ulaya. Idadi kubwa ya magari yatumikayo nchi ya Marekani hata bara la Ulaya ni yale ya Kijapani. Bidhaa nyingi za Marekani ni zile za kutoka China na Korea, pia kutoka visiwa vya Indonesia. Sasa nchi inapotegemea bidhaa za kutoka nje kujenga uchumi wake ni dalili wazi nguvu za uchumi zinazidi kutetereka. Pamoja na maelekezo ya ubora wa bidhaa zinazoingiwa Marekani, bado soko la bidhaa za ndani ni dogo kutokana na gharama za uzalishaji ukilinganisha na gharama za uzalishaji kutoka Bara la Asia. Kama magari ya kijapani ni imara zaidi kuliko magari ya kimarekani ambayo yakishachoka unaweza kupata ugonjwa wa moyo within 6-9 years wakati ya kijapani yanadunda hadi miaka 15 bila usumbufu wa pekee.

  Wanaoona mbali katika hilo wameshaanza kutafuta upenyo mataifa mengine kama Asia na Afrika kutokana na hali ya uchumi wa Ulaya na Marekani kusuasua na kutoleta matumaini ya kuhuishwa. Ndio maana tunaona wimbi la wawekezaji Barani Afrika, si ombi letu bali ni msukumo kutoka kwao, na hata tusipoenda kuwaomba kwa hali ya sasa watakuja tu, kinachotakiwa ni kuweka mikakati ya hao wawekezaji kukuza uchumi wa nchi zetu badala ya kuiba rasilimali na kutoroka nazo.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Marekani lilitokana zaidi na uroho wa viongozi wa makampuni yao. Walitaka wazalishe bidhaa kwa gharama ndogo sana huko China na Mexico, halafu waziuze kwa faida kubwa sana Marekani. Wakasahu kuwa kwa kufanya hivyo walikuwa wanaua soko lao hilo kwa vile wanunuzi watakuwa hawana kazi ya kuwapa kipato. China ilichangamkia sana tenda hiyo mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kwa kuanzisha makampuni ambayo yalikuwa ni kopi ya yale ya merakani yaliyojijihamishia huko China. Michoro ya biadhaa zote zilizohamishwa kwenda kutengenezewa China ilipatikana na hivyo wachina wakaaza kutengeza bidhaa hizo hizo tena kwa bei ya chini zaidi kwa vile maCEO wao halipwi mamilini ya wale wa Marekani. Uroho na ubinfasi ndivyo vinavyoiponza Marekani. Na kwa bahati mbaya wamarekani wengi leo hawataki kusoma masomo magumu ya engineering na science kwa kiwango cha juu kama wanavyofanya wenzao wachina na wahindi. Kwa hiyo miaka michache ijayo, hata ile brain power ya wamarekani katika fani muhimu za sayansi na engineering zitatoweka.
   
 10. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Nawashukuru sana wote bwana candid scope na kichuguu huo ndio ukweli ulivyo, je SWALI VIONGOZI NA MATAIFA yetu ya Africa na hasa sisi watanzania wanajipangaje kwa hili ? HAWAJAIONA HIYO FURSA ? ?
   
 11. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Freemason
   
 12. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Haswa, hii wenyewe wanaaita Reaganomics, na hii ndiyo iliyoleta matatizo ya leo. Yaani ni uroho tuu wa republicans wanasahau kuwa ukimkamua ng'ombe sana maziwa bila kumlisha vizuri atakufa na wote mtakosa.

  Yaani wao sana sana wanakimbilia kusoma sociology wakitegeme ndiyo italisha inchi. Siyo kudharau taaluma za watu, lakini taaluma nyingine ni muhimu pale unapokuwa umeshiba. Sasa kama nchi haizalishi unafikiri social worker atasaidia nini?

  Vijana wengi wakimarekani hawapendi kabisa hisabati na sayansi ukiwaambia mimi nimetoka Africa nimekuja kufanya Engineering wanakwambia, "you're so smart, I wanna have your baby". Msingi wa maendeleo ya nchi ni innovation na hii inatokana na science and research lakini hawa generation y wa huku hawataki kabisa kusikia mambo ya kuumiza kichwa.

  Wanafunzi wengi wanao major kwenye engineering marekani ni wageni na kati ya hao asilimia kubwa ni waasia. Mi nakumbuka miaka ile wakati nafanya CE niliwahi kumuuliza mdada wa kijapani, "kwanini mnakuja huku? Kwani nchi yenu ni tajiri na inavyuo vizuri. Nikamwambi sisi kuna baadhi ya taaluma hatuwezi kuzipata nyumbani ndo maana tunakuja huku".Akaniambia, "ni kwasababu ya ushindani, akaendelea kusema Marekani ni washindani wetu wakubwa kibiashara kwahiyo nilazima tuwasome vizuri ili tuwajue, kiutamaduni na kielimu".
   
Loading...