Taarifa ya BBC Swahili ya leo (kama inavyoonekana pichani) imeandika habari za ki uchunguzi juu ya meli ambazo Trump amesema zinakwenda Korea kaskazini kushambulia na dunia ikatambua vita imeiva haswa ukizingatia ilisheheni makomando, madege pamoja na mabomu mazito ya masafa marefu na mafupi
meli hiyo haikwenda huko bali ilikuwa ni vitisho tu.
Tujikumbushe; America ilishambulia sehemu tofauti duniani ili kumuathiri Kim kisaikolojia apate hofu na kukubali mazungumzo, hali itakayopelekea kuondolewa uwezo wa silaha za Nyuklia na kuangamiza vinu vyake.
Moja ya tisho kubwa ni Amerika kupiga bomu lake la kisasa kabisa na lenye jina la 'mama wa mabomu yote duniani' ambalo alipiga nchi nyingine kwa sababu nyingine lakini wachunguzi wa mambo walisema ile ni salam kwa Kim
Pia Us alishambulia Syria pamoja na Somalia na kote huko aliangamiza roho za watu.
Kitendo cha Kim kuimarika kijeshi haswa kwa silaha za nyuklia kinaiumiza kichwa sana Marekani kwa kile kinachoitwa kutishia usalama wake, ila Trump jambo hilo linamuumiza zaidi
Pamoja na vitisho vyote Kim hakutishika kabisa na ndiyo kwanza amejipanga kivita na kusema atazidi kuyajaribu makombora yake mapya kila wiki
Hakuna vita tena na vitisho havikufanya kazi na sasa Amerika anaelekea kwengine
Kikwazo zaidi ni kwa kuwa Us hazijui vema silaha za North Korea kuhusu uwezo wake na hata namna ambavyo atazikabili, wanachojua ni kile Kim atakachokisema mwenyewe pale anapozindua kombora, zaidi ya hapo hawana taarifa zozote za kiuchunguzi japokuwa wanahisi anayo mabomu elfu moja ya yenye uwezo wa kufika bara lolote duniani ambayo yanaweza kufika moja kwa moja Marekani na kushambulia
Ndugu zangu, Us hapigani na nchi asiyoijua vema silaha zake na ndio maana anaremba tangu majuzi kuhofia usalama wake
Wangemkabili Kim miaka mingi iliyopita lakini sasa ameshapiga hatua wamechelewa, kitendo cha kuufyata ni ushindi na furaha kwa bwana mdogo