Marekani ina lengo gani kwa kukashifu nchi nyingine kutoa silaha kwa Russia?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111432777212.jpg

Hivi karibuni, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Reuben Brigety aliiomba radhi serikali ya Afrika Kusini kwa kuishutumu nchi hiyo kuipatia silaha Russia. Kabla ya hapo, Marekani nayo pia ilidai kwamba China inaweza kutoa silaha kwa Russia.

Lakini halisi ni kuwa si China wala Afrika Kusini imejihusisha kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine, wala haitoi silaha kwa upande wowote. Basi je, ni kwa nini Marekani inapenda kuzikashifu nchi nyingine katika suala hili bila ya ushahidi wowote?

Kwanza, Marekani inaficha lengo lake la kujitafutia manufaa binafsi katika mgogoro huo. Katika mchakato mzima wa mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani inabeba lawama zisizoweza kukwepeka kutoka kukuza upanuzi wa NATO kuelekea upande wa mashariki na kufanya"mapinduzi ya rangi" katika maeneo ya karibu Russia, hadi kufanya uchochezi wakati mvutano kati ya Russia na Ukraine unapopungua, ambapo ilituma maafisa wa ngazi za juu kufanya ziara ghafla ili kuonyesha kuunga mkono Ukraine, na kutoa misaada ya kuchochea mgogoro. Ni wazi kuwa mgogoro huo umekuwa makabiliano kati ya Marekani na Russia, na kukashifu na kuonya nchi nyingine zisisaidie kijeshi Russia, ni kuhakikisha kuwa Marekani inaweza kudumisha nguvu yake katika mgogoro huo.

Pili, kitendo hicho kinaharibu uhusiano kati ya China, Russia na nchi za Afrika, ambazo kwa pamoja zinaunga mkono kujenga dunia iwe na usawa na haki. Mbele ya shinikizo kutoka kwa Marekani, China, Afrika Kusini, na Russia, zikiwa ni miongoni mwa nchi wanachama wa BRICS, zote zimetoa kauli ya wazi kwamba hazikubali umwamba wa Marekani. Mwezi Februari mwaka huu, nchi hizo tatu zilifanya mazoezi ya pamoja ya siku 10 ya jeshi la majini, ikimaanisha kuwa ushirikiano kati ya nchi za BRICS haukomei katika sekta ya uchumi, bali pia unahusisha jeshi. Uhusiano huu wa karibu bila shaka unachukuliwa kama changamoto na kitisho kwa Marekani. Kwa hiyo, Marekani inazipigia kelele China na Afrika Kusini kutoa silaha kwa Russia ili kujenga kutoelewana kati ya pande hizo tatu na kudhoofisha uaminifu miongoni mwao.

Tatu, hatua hiyo inatenganisha nchi za Afrika. Sote tunajua, kuhusu mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani imekuwa ikijaribu kuziteka nchi za Afrika katika kambi yake, lakini majaribio yote yameshindikana. Mitazamo ya nchi za Afrika inatofautiana, kwani nchi nyingi hazipendi kuegemea upande wowote kama Afrika Kusini, lakini nchi chache zimeamua kuunga mkono upande mmoja. Kwa hivyo, kwa kuikashifu Afrika Kusini kuizuia silaha Russia, Marekani inaweza kuiita nchi hiyo kama "msumbufu", na kuweka shinikizo kwa nchi nyingine za Afrika zenye msimamo wa kutoegemea upande wowote kujitenga au hata kuipinga Russia.

Kwa kifupi, Marekani kukashifu nchi nyingine kutoa silaha kwa Russia kunaweza tu kuonyesha nia yake mbaya. Hivi majuzi, mwakilishi maalum wa China ameanza ziara katika nchi za Ukraine, Russia na nchi nyingine ili kuwasiliana na pande zote juu ya kutatua mgogoro kati ya Russia na Ukraine. Wakati huohuo, ujumbe wa viongozi sita kutoka Afrika Kusini, DRC, Senegal, Uganda, Zambia na Misri pia unatarajiwa kwenda mjini Moscow na Kiev kujadili suluhu zinazowezekana za kumaliza mgogoro huo na marais wa nchi hizo mbili.

Inaaminika kuwa, katika mazingira ya sasa, mitazamo yenye mantiki inayotetea kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo na kupinga kuingiliwa na nje na vikwazo itatawala.
 
Marekani sio a akashifu anazionea huruma sababu mrusi stock yake ya silaha kwa sasa iko.kidogo na ciwanda vyake uzalisjaji silaha umekwama kwa kukosa baadhi ya mali ghafi sababu ya vikwazo vya kimataifa

Sasa hivi urusi anachofanya kimojawapo ni kumunua silaha kwa wale aliwauzia sio kwa pesa taslimu sababu kuna vikwazo anachofanya ni kuwa lama ulikopa silaha za shilingi bilioni moja pamoja na riba sababu kwako hazitumiki sana sababu vita huna anakuja kuomba azinunue kwa kuzichukua mfano kwa shilingi milioni mia saba na kufuta deni lako lote la bilioni moja analokudai kwa hizo milioni mia saba ila wewe umdai shilingi.milioni.mia tatu kama deni ulilomkopesha.

Mmarekani anawaonea huruma kuwa wanampa huyo mrusi silaha zao je jwao kikiinuka watakuwa wageni wa nani?
 
View attachment 2631943

Hivi karibuni, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Reuben Brigety aliiomba radhi serikali ya Afrika Kusini kwa kuishutumu nchi hiyo kuipatia silaha Russia. Kabla ya hapo, Marekani nayo pia ilidai kwamba China inaweza kutoa silaha kwa Russia.
Supa poa kumbe ameanza kuazima silaha wakati masaa sabini na mbili hayajaisha?
Hata mimi ningekuwa marekani ningekashfu, urusi alianzisha vita bila kupima athari
alijua fika NATO wangetia miguu yao ndo maana mwanzoni alipiga mikwara mizito
kwamba atakayejiingiza atakipata cha moto.
 
Back
Top Bottom