Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,344
- 6,865
Sijakosea. Unachokisema vwewe ndiyo KILE AMBACHO nimeandikaSio shida. Kwanza Makanyaga Kakosea kidogo John Adams hana udugu na Andrew Jackson.
John Adam rais wa 2 ni Baba wa John Quincy Adams rais wa 6.
William Harrison rais wa 9 ni Babu wa Benjamin Harrison rais wa 23.
Theodore Roosevelt rais wa 26 ana udugu na FDR (Franklin Delano Roosevelt) rais wa 32. Hata First Lady wa FDR, Eleanor Roosevelt ni mpwa wa Theodore Roosevelt. Hivyo walioana ndugu.
JFK, Rais wa 35, mdogo wake RFK (Alikuwa AG wakati wa uongozi wa kaka yake na baadae Senetor) ilikuwa agombee mwaka 1968 ila aliuawa na Sirhan Sirhan. Ted Kennedy ( alikuwa Senator kwa muda mrefu) mdogo wao mwingine akataka kugombea mwaka 1980. Mwanae Ted anayeitwa Patrick Joseph Kennedy aliwahi kuwa US Rep. Nadhani mnamjua Robert F. Kennedy Jr. mtoto wa RFK aliyeuawa 1968 alitaka kugombea mwaka huu.
George H. W. Bush rais wa 41 ni Baba wa George W. Bush rais wa 43. Mdogo wake George W. Bush, Jeb Bush (alikuwa Governor), alitaka kugombea mwaka 2016.