TANZIA Marekani: Charlie Kirk afariki dunia baada ya kupigwa risasi

TANZIA Marekani: Charlie Kirk afariki dunia baada ya kupigwa risasi

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,896
Reaction score
11,791
charlie-kirk-gty-jt-250910_1757531378345_hpMain.jpg
Charlie Kirk, aliyejulikana kama mwanachama mkuu wa mrengo wa kulia na mwanzilishi mwenza wa Turning Point USA, aliuawa kwa risasi tarehe 10 Septemba 2025, katika tukio linalochukuliwa kama moja ya dalili za ongezeko la vurugu za kisiasa nchini Marekani. Tukio hilo linapelekwa kwa uchunguzi wa kina, huku halijulikani mshukiwa halisi bado hayupo mikononi mwa polisi

Angalia jinsi alivyouawa kwa risasi. Hii ni screenrecord, kwa hiyo ni heri uzoom ili uone vizuri

Charlie Kirk amefariki baada ya kupigwa risasi tarehe 10 Septemba 2025, wakati akiwa kwenye mkutano wa "American Comeback Tour" katika Utah Valley University, Orem, Utah .

Shambulio lilitokea karibu saa 12:10 jioni (MDT). Risasi ilipigwa na kutoka kwa jengo lililoko takribani mita 200 mbali na jukwaa. Charlie alipigwa shingoni na kuanguka papo hapo .

Kifo kilithibitishwa na Rais Donald Trump kupitia mtandao wake wa Truth Social, akimtaja Kirk kuwa "mkubwa, hata wa kifahari", na kuongeza kuwa ilikuwa ni hasara kubwa kwa vijana wa Marekani .
20250911_000150.jpg

FBI pamoja na ATF (Bureau of Alcohol, Tobacco, Firearms and Explosives) waliingizwa kwenye uchunguzi wa tukio hilo. Awali kuliripotiwa kuwa mtu alikamatwa, lakini baadaye ukaelezwa mtu aliyekamatwa si mshukiwa, na mshukiwa halisi bado hayupo mkononi mwa polisi .

Tukio hili limechukuliwa kama sehemu ya wimbi la vurugu za kisiasa zinazoongezeka nchini Marekani katika kipindi hiki, likichangia wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa mtu anayeonekana kama kiongozi wa kisiasa .

Charlie Kirk alikuwa mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa shirika la kisiasa la Turning Point USA, ambalo liliandaliwa kumshawishi vijana watunge siasa za mrengo wa kulia. Alikuwa na umri wa miaka 31 alipoaga dunia, na aliongoza kupitia sinema maarufu za kisiasa, vituo vya redio na podcasti .

Kwa wasiomjua Charlie Kirk tembeleeni account ya Instagram ya "Turning point USA" Utaona, video zake. Alikuwa anapenda kubishana na wanachuo kuhusu mambo ya siasa
 
RIP Charlie Kirk.

Huyo ndie alikuwa na ushawishi mkubwa kwa wafuasi wa Donald Trump khasa vijana ambao wengi walipiga kura katika uchaguzi ulopita ambao Trump alishinda.

Ni mfuasi mkubwa wa MAGA na alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa siasa kali za mlengo wa kulia.

Muuaji bado hajapatikana ingawa polisi walikuwa wakimshikilia mtu ambae wadhania (personal of interest) kuwa ndie aliepiga risasi hiyo moja ilomlenga Kirk shingoni na kumuua papo hapo lakini muuaji halisi bado asakwa.

FBI imethibitisha kuachiwa kwa mtu huyo kupitia mkurugenzi wake Kash Patel.
 
...akili kubwa huku akineemeka kwa kusambaza chuki katika jamii. Apumzike panapostahili
Sidhani kwamba jamaa alikuwa na akili kubwa ukizingatia kuwa aliacha kwenda chuo kikuu na akiwa na miaka 18 akaanzisha turning point movement (hapa niko tiyari kukosolewa).

Naamini kwa watu wa aina yake angejiongeza kwa shahada kadhaa khasa za siasa au sayansi jamii basi angeelewa madhara ya kukazania kuondoa "second amendment" ambayo yamuondolea mmarekani uwezo wa kumiliki silaha.

Second Amendment ukitaka uishi uzuri kisiasa bila kudhurika usiiguse hiyo.

Hata Barak Obama aliona hiyo (kutogusia second amendment) na akaishi kisiasa kwenye uraisi kwa miaka 10 licha ya kuwa ni mmarekani mweusi.
 
....nilikuwa najaribu kumjibu mdau aliyesema kwamba Kirk alikuwa ni akili kubwa, hakuwa na hiyo akili kubwa kama ambavyo wahafidhina wanataka kumjengea jina. Siungi mkono kilichompata, mauaji ya aina yoyote hayaleti suluhu kwenye kutofautiana kwa mitizamo.
Jamaa hakutaka tu kuiongelea 2nd amendment bali alihubiri na kutaka kupandikiza mawazo hasi dhidi ya dhahania ya 'replacement'. Na asingeishia hapo, rejea wale wawakilishi wa Minnesota
 
Unapimaje akili ya mtu mkuu kujua akili kubwa na ndogo
 
....nilikuwa najaribu kumjibu mdau aliyesema kwamba Kirk alikuwa ni akili kubwa, hakuwa na hiyo akili kubwa kama ambavyo wahafidhina wanataka kumjengea jina. Siungi mkono kilichompata, mauaji ya aina yoyote hayaleti suluhu kwenye kutofautiana kwa mitizamo.
Jamaa hakutaka tu kuiongelea 2nd amendment bali alihubiri na kutaka kupandikiza mawazo hasi dhidi ya dhahania ya 'replacement'. Na asingeishia hapo, rejea wale wawakilishi wa Minnesota
Ndo mkuu, hata mimi siungi mkono "violence" yoyote ile ila hawa jamaa wa mlengo wa kulia huwa wajitengenezea maadui bila kufahamu madhara ya kujadili masuala mazito.

Dunia yazidi kubadilika kwa kasi sana na sasa hivi ni kuwa makini na kila uongeacho.
 
.....kwa muktadha wa ishu ya leo, akili kubwa imepimwa kwa uwezo wa kuongea mambo ya kihafidhina kwa sauti kubwa na kupata ufuasi wa wanaoamini mawazo yako.
Vipimo vingine havijajumuishwa kwenye aya ya juu.
Basi hujapima akili ila umetoa maoni. So tuache kutoa maoni kwa kuwakilisha hisia mkuu. Tutoe maoni tu sio kuja na hitimisho la hoja la jumla. Maana umefika mbali sana mpaka kupima akili? Ni kati ya ipi na ipi sasa.
 
Ila inasemekana kama ni staged mana apo kwenye mkono pete imehama kutoka kidole kingine kwenye kidoke cha mwisho

Back
Top Bottom