Marehemu wengi hurejea baadhi ya sehemu walizofia?

Marehemu wengi hurejea baadhi ya sehemu walizofia?

Ndotoni....but alikuja straight...akaniuliza hapa ndo nyumbani kwako?
nikamjibu ndio...akasema basi nimekuja tu kukuaga
tukapeana mkono akaondoka...
Nimekusoma vema, ila hata Mimi nikiwa mdogo kati ya miaka 8-10 kuna vitu vilikuwa vinatokea nikiota usiku jambo kesho lzm litokee, mfano wakati mmoja tulimwangiza baba flani atuletee viatu nje ya nchi,akaa kama wiki2. usiku nimeota nimeletewa viatu, kweli asubuhi yake nililetewa viatu. wakati mwingine tena nilikuwa nimelala katika mkeka usiku nikaota nampiga nyoka fimbo na kumuua. kulipo kucha asubuhi kweli nilimkuta nyoka pembeni yangu katika mkeka amekufa, Sikujua alifikaje pale
 
Interesting
unapaswa ku pay attention na kila unachoota
 
Ni kitu cha kushangaza kidogo kustaajabisha na pengine inaweza kuwawia vigumu wengine kuamini! Lakini baadhi ya marehemu huwa na hulka kwa sababu zozote zile hurudi mahali walipofia ama kuugua hadi kufa
Hawaji moja kwa moja, huwaoni moja kwa moja kwakuwa wao si mwili tena wao ni roho...utahisi tu hali tofauti utahisi uwepo wake harufu yake ama hata kumuona sura isiyo kamili

Hali hizi hutokea kwenye mazingira ya utulivu pasipo na vurugu za watu wengi na muda mwingi huwa ni nyakati za usiku
Wengine hurudi kusalimia, wengine hurudi kukumbukia mateso waliyopitia wengine hurudi kukamilisha mambo anuwai wasiyoyakamilisha....
Ni wazi sasa kuwa kifo si mwisho wa uhai bali mi mwanzo wa kuingia kwenye hatua nyingine ya maisha isiyo juu na kubwa zaidi kuliko haya maisha tunayoishiView attachment 456023
Unatumia sayansi gani kuthibitisha haya??
 
ni images ndani ya bongo zetu na memories ndo zinafanya uone kama aliyekufa amerudi sawa na ile theory inayosema Sisi wanadamu huwa hatuna mwisho, tumekuja duniani kwaajili ya kukamilisha mambo ya system iliyopo. Hakuna nafsi yeyote inayokufa au kupotea. Lazima mzunguko ukamilike kwamba unapokuja (Unapozaliawa) duniani baada ya kufa unakwenda kwenye ulimwengu mwingine. Meditation pekee ndio inayo saidia kujitambua kuwa wewe hapa duniani ni nani na umekuja kwa ajili gani.Kabla ya kuzaliwa sisi tulitoka kwe nyeye source ya souls ambayo nguvu zake zinapatikana kutokana na meditation baada ya kuvuta cosmic energy. Na mtu anaposhindwa kuelewa lengo lake kuu la hapa duniani atakufa na baadae atarudi duniani kama kiumbe tofauti.
 
Baada ya kifo roho huwa na uwezo mkubwa zaidi wa utambuzi

Nna dada yangu alifariki nikiwa shule na kwa bahati mbaya sikuweza kuhudhuria msiba wake. Niliporudi nyumbani kuna siku nikamuota, alikuja huku akiwa na furaha na aliponiona alitaka kunikumbatia. Mimi nikamkwepa nikamwambia wewe mbona ulishakufa kitambo sasa umefuata nini huku? Alinijibu hivi ,'ni kweli nimekufa ila huko niliko nakukumbuka sana ndo maana nimekuja kukusalimia'. Akaendelea kusema, kama unaniogopa basi ntajiziba usoni na kanga then nipe mkono tusalimiane. Kweli akajiziba usoni na kanga nikampa mkono tukasalimiana then akapotea nikastuka usingizini. Ukapita kama mwaka hivi akaja tena, akaniambia maneno yaleyale kuwa huko aliko ananikumbuka sana ndo maana huja kunisalimu na akaniambia kila nikija ntakua najifunika usoni tunasalimiana kwa kupeana mikono then anaondoka. Kweli tulipeana mikono then akaondoka nikastuka usingizini. Nilimsimulia hii kitu mama angu, alikasirika sana akasema akuache kabisa asikufatefate na kweli hajaja tena kwa style ile ila huwa namuota endapo kuna jambo muhimu sana nimemfanyia mmoja wa ndugu zake ndo huja kama kutoa shukrani. Hii hali inanitisha mno
 
Biblia. Mhubiri 9:5
[5]kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Kwa muktadha wa Maandiko ni sahihi lakini pia kuna tafsiri nyingi kwenye hilo na pia kuna miktadha mingine ya reincarnation nk
 
Dah!...mimi leo nimemuota nduguyangu aliyefariki miaka miwili iliyopita nikimlisha chakula huku ndugu yangu ambaye nimzima tukimzika akiwa amefariki ambapo hawa nimtu na mdogowake
Hunitokea Mara nyingi sana naota nazungumza na watu waliokufa pia wakati mwingine huota nacheza na wadudu hatari sana kwa binadamu! Mshana hii husababishwa na nini? Au dalili za nini!! Nifumbue kidgo mn huwa napuuzia tuu
 
Ndotoni....but alikuja straight...akaniuliza hapa ndo nyumbani kwako?
nikamjibu ndio...akasema basi nimekuja tu kukuaga
tukapeana mkono akaondoka...
Mkuu siku nynge usirudie iyo tabia ya kupeana mkono na wafu ukiwa ndotoni huwa wanasema unaweza ukajikuta unaenda nae....au ukaskia unaitwa usiku na mtu haonekan hurusiw kuitika
 
Hunitokea Mara nyingi sana naota nazungumza na watu waliokufa pia wakati mwingine huota nacheza na wadudu hatari sana kwa binadamu! Mshana hii husababishwa na nini? Au dalili za nini!! Nifumbue kidgo mn huwa napuuzia tuu
Mh hili la kuota marehemu na maumbo ama viumbe vya kutisha huwa ama lina uhusiano na nguvu za giza ama kisayansi tatizo la ubongo
 
Back
Top Bottom