Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Usiulize karafuu Pemba, Lakini Rais Magufuli ni kivuli halisi cha Marehemu Karume kwa sifa na vitendo:-
1. Wote ni wachapa kazi na hawaagizi. Mzee Karume kila siku saa moja asubuhi yuko Michenzani kusimamia ujenzi wa nyumba za maendeleo kwa vitendo. Athari ya historia alioiacha kwa mji wa Zanzibar ni kielelezo kisichosahaulika.
2.Wote hawapendi kufuja pesa za umma kwa kusafiri. Mzee Karume hakuwahi kusafiri nje ya nchi zaidi ya Tanzania uhai wake wote akiwa Rais wa Zanzibar na Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania
3. Wote wanawapenda na kuwatetea wanyonge
4.Wote wanachukia siasa zisio na kikomo.Mzee Karume alipiga marufuku vyama vya siasa na marufuku yakufanyika uchaguzi kwa kipindi cha miaka 50!
5. Wote ni wapenzi wa Young Africans: Mzee Karume alitoa Tshs 2,000,000 sawa na US$ 287,715 kwa wakati huo kugharamia ujenzi wa Klabu ya Yanga Jangwani
6.Wote wanapenda " surprises" kwa wananchi wao,JPM ameikita nchi kuhamia Dodoma; Mzee Karume alileta Kituo cha TV cha kwanza ch rangi barani Afrika
7. Wote wanachukizwa na kuwa na Taifa ombaomba. Mzee Karume mpaka amekufa Zanzibar ilikuwa haidaiwi hata senti moja na Taifa lolote duniani.
8.Karume ni mwanamapinduzi; JPM ni mwana mabadiliko