Marehemu achaguliwa uongozi wa tawi CCM!

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Nimeona kwenye gazeti la sema usikike la tar 28, ukurasa wa kwanza. Limeandikwa, "Vituko uchaguzi wa ccm: Mwanachama aliyekufa na kusahaulika achaguliwa mwenyekiti wa ccm Dar". Nimebaki najiuliza, swala la kukosa wanachama wa kugombea uongozi wa shina (mabalozi) limefikia hapa!? Kweli ccm imekwisha vibaya!
 
Hilo ni gazeti la usheshi au la habari?
 
hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaha...mbavu zanguu
 
wamekosa wawakilishi mpaka wanaweka marehemu! Teh teh teh

Hilo ndilo swali nimejiuliza nikakosa jibu! Nashangaa hao marehemu watakisaidia nini chama! Au ndio na wao wanaelekea kaburini aliko!
 
Hawa magamba walikosa wagombea maeneo mengi hivyo wakaamua kuwaweka viongozi wa matawi na mashina kwa mtindo wa AUTOMATIC. Sishangai kuskia kuna marehemu kati yao kwani hata chama kinakaribia kufa, lakini wako wengi waliopewa uongozi wa matawo na mashina huku wao hawajui kitu
 
Magamba kweli wamekwama sasa,wanachagua hadi mizimu iwaongoze !? Duuu...uh ! 2015 nafikiri watamsimamisha Hayati Mwl.Nyerere agombee urais maana ndo anaheshimika hadi leo kwa watu wa vyama vyote.
 
Halafu kuna watu watasema eti ccm ni chama makini kwa vp wanajua wao,shame on them,nachukia mimi halafu chama tawala eti?
 
Nimeona kwenye gazeti la sema usikike la tar 28, ukurasa wa kwanza. Limeandikwa, "Vituko uchaguzi wa ccm: Mwanachama aliyekufa na kusahaulika achaguliwa mwenyekiti wa ccm Dar". Nimebaki najiuliza, swala la kukosa wanachama wa kugombea uongozi wa shina (mabalozi) limefikia hapa!? Kweli ccm imekwisha vibaya!
Mtu mzima na akili zako unashabikia kitu kisicho na mbele wala nyuma.
Filipo hebu rudi kwa wenzio chekechea ukaandike makorokocho unayoyaelewa vizuri zaidi.
 
si vibaya wakiongozana kule kuzimuni.
 
Kama kun mwana-ukoo yeyote yule na huyo marehemu basi akapewe urithi hicho kiti cha CCM maana ni ngekewa kwa ukoo wao kuongoza hata baada ya kwenda ahera.

Nimeona kwenye gazeti la sema usikike la tar 28, ukurasa wa kwanza. Limeandikwa, "Vituko uchaguzi wa ccm: Mwanachama aliyekufa na kusahaulika achaguliwa mwenyekiti wa ccm Dar".

Nimebaki najiuliza, swala la kukosa wanachama wa kugombea uongozi wa shina (mabalozi) limefikia hapa!? Kweli ccm imekwisha vibaya!
 
Mtu mzima na akili zako unashabikia kitu kisicho na mbele wala nyuma.
Filipo hebu rudi kwa wenzio chekechea ukaandike makorokocho unayoyaelewa vizuri zaidi.

Mkuu, sina sababu wala tabia ya "kurudi nyuma!". Unaweza kulisoma hilo gazeti ujiridhishe.
 
Mimi wala sishangai. Mtaa wetu Kariakoo umepewa mjumbe wa shina anayeishi Tandika. Sishangai.
 
Back
Top Bottom