JUMUIYA ya Marastafarian Tanzania, (Taramo), imeandaa Tamasha la kumbukumbu ya muasisi wa muziki wa Reggae ulimwenguni, Nesta Robert, maarufu kama Bob Marley litakalofanyika ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam, leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ras Bumijah alisema, tamasha hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuenzi mchango wa muasisi huyo, aliyechangia pia kulinda mila na utamaduni wa marastararian ulimwenguni kote.
Alisema, kutokana na mchango wake huo, Jumuiya imekuwa ikifanya kumbukumbu kila mwaka na safari hii wamealika wasanii na wanamuziki wengi kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.
Ras Bumijah, aliwataja baadhi ya wasanii na wanamuziki watakaopamba leo kuwa ni washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro, Chibwa na Dabo, Ras Mizizi, Man Kifimbo na yeye mwenyewe.
"Tumewaalika Dabo na Chibwa kuja, kutokana na kuutendea haki muziki huu ulioasisiwa na Bob Marley, ambaye Jumamosi hii tunamkumbuka. Wataitumia nafasi hii kuwashukuru wale wote waliofanikisha ushindi wao na wataimba live kwa ajili ya mashabiki na wapenzi wa miondoko ya reggae," alisema Ras Bumijah.
Aliongeza kuwa, pamoja na wasanii hao kutoa burudani, pia kutakuwa na burudani nyingine ya vikundi mbalimbali vinavyopiga muziki wa reggae asili, sambamba na uuzaji wa mavazi ya asili ya kiafrika kama njia ya kumuenzi Hayati Bob Marley.
Chanzo:Tanzania Daima

Wazungu ni akina nani?Sina hakika na hilo la Bob kuwa muasisi wa muziki wa Reggae labda ningeshauri watu wasome vizuri historia ya The Wailers, kusema Bob ndiyo muasisi(peke yake) siyo kweli labda kusema 'mmoja wa waasisi wa Reggae', Tanzania Daima wangetumia neno 'mmoja wa waasisi wa muziki wa Reggae' maana Bob peke yake siyo mwasisi kama wazungu wanavyotaka tuamini, uasisi wa Reggae ni wa kundi na unapotaja uasisi wa Reggae usiache kuwataja kina Peter Tosh na Buny Wailer pia
africa unite
How good and how pleasant it would be before God an'man yea-eah..Coz we are moving right out of babylon. And we are going to our father's land