Marando na watuhumiwa wa ufisadi

CCM wamefikia hapa kwa kupuuza puuza vitu walivyokuwa wanaviita havina tija kwa uhai wa chama!issue ya marando lazima tuiweke sawa mapema na wananchi wa kawaida watuelewe bila mishipa kuwatoka!
 
Comrade Ngwendu, ni kweli kabisa hawa Pro-CDM-JF,uelewa wao ni mdogo sana kama huo mfano wa mgonjwa na Wakili.
Tatizo hawataki kujifunza na kukubali mawazo kutoka kwa watu wengine wao ni CDM tu mpaka imewapa upofu na akili zimedumaa kabisa tena zimefunikwa na blanketi jeusi,
hawa Pro-CDM-JF ni pumba sana mpaka wanatia huruma
Ya kweli haya?
 
Chadema ni chama makini hakitaki kwenda Ikulu kwa kupigiwa kura na watu wasioelewa nini wanafanya kama ilivyozoea CCM. Kama mpiga kura hajui kutofautisha kati ya Kazi za chadema kama chama cha siasa na kazi za kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Marando basi wapiga kura bado hawajaelimika.

Marando kama mwananchi mwema anapinga ufisadi kwasababu hapendi watu fulani kuonewa kwa rasilimali zao kuliwa na watu wachache kwa njia za wizi.

Pia Marando kama Mwanasheria (professional) atakuwa wa ajabu kama atakataa kumsimamia mtu katika kesi ili atendewe haki. Sidhani kama Chadema ikiingia madarakani itafanya kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi na kuwasweka jela kwa vifungo bila kuwapa nafasi ya kujitetea na kufanya haki itendeke.

Napingana na wewe mkuu,

Huwezi kufanya kazi ya profession kwa kudeal na watu wenye imani tofauti na wewe. Ndiyo maana Tz ya enzi zile ilikataa kata kata kufanya biashara na makaburu bila kujali madhara ya kiuchumi ambayo tuliyapata.

Marando akifanya kazi na mafisadi lazima watamlipa pesa za kifisadi tu na hilo ni tatizo kubwa!
 
Wana JF

Kwanza na-declare interest mm ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA, Hili swala la Marando kuwa wakili wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi km vile manji na mahalu litakuja kuwa na madhara makubwa sana hapo badae ktk harakati za chama za kuchua dola natambua kabisa ile ni professional yake na ni vigumu aache kazi aliyoisomea kwa muda mrefu, lakini kabla ya kuchua kazi lazima mtu ufanya client assessment.

Kwa kuwa ameamua kuwa ktk siasa na kufanikiwa kuwa mjumbe wa cc ya cdm ni wakati wake muafaka wa kuhakikisha kimoja kati ya professional yake na siasa hakuna kinacholeta madhara kwa kingine. Kwa hiyo moja ya criteria ya kutumika kwake kum-accept client iwe ni asiwe mtuhumiwa wa ufisadi. Nionavyo mm professional yake kwa sasa inaleta madhara ktk siasa si kwake tu bali kwa Chadema kwa ujumla coz ni vigumu sana mtu kupinga ufisadi majukwaani na kuukubali mahakamani na watu wote wakaamua kukuamini ww ni mpiganaji wa kweli wa ufisadi.

Swala kubwa la sisi wana-chadema tunalotakiwa kulielewa ni kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawawezi kutofautisha professional na siasa kiasi kwamba point tutakayoitumia kuuelezea uma ya kuwa hii ni siasa na hii ni professional haitaweza kuzaa matunda yeyote. Marando na uongozi wa juu ulitazame hili kwa mapana na marefu ili nguvu iliyokwisha tumika kukifikisha chama hapa isije kupotea kirahisi kisa mtu mmoja ambae ana uwezo wa kuchua kesi zingine na kuendelea na maisha.

Tujiulize swali dogo kwa mfano leo ROSTAM amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa KAGODA na marando akafanya km anavyofanya kwa wale wa EPA itakuwa sahihi? Au kuwatetea wa EPA itakuwa halali na kumtetea Rostam itakuwa haramu wakati wote ni mafisadi?

Nawasilisha

You have a point
 
Mimi nakubaliana na suala hili. Professionalism wanaijua professionals. wakulima wetu hawawezi kutofautisha ukisimama jukwaani na kusema Ufisadi mwiko kesho unasimama mahakamani kumtetea Rostam na kusema siyo fisadi wakati wewe jana ulimtaja kuwa ni fisadi!

Anaweza kuchukua kesi nyingine kwa sababu halazimishwi.

Declaration: Mimi ni Kiongozi katika Chadema ngazi ya wilaya lakini suala hili linanipa kizunguzungu! Linahitaji kufanyiwa kazi
Quality
 
Pole sana ndugu yangu halafu ukizingatia wewe ni kiongozi wa CHADEMA...Mimi ni mtanzania wa kawaida tu ila napenda kuyaona mambo katika uhalisia!!

Katika hili suala Marando lazima achague upande mmoja ...ama kuwatetea Watanzania wanaoibiwa au mafisadi wanawaibia. Hata kama majukwaa ni tofauti...hawazi kuwatetea wote!!

Na swali gumu ni hili hapa...Hivi hao wateja wake wakishinda kesi atarudi kwenye jukwaa la CHADEMA kuwasafisha???
 
Kwani hujui kila goti kwa mungu litapigwa kama anatetea usahihi atafanikiwa kama atawafanya wasiwe na hatia wakati wana hatia ole wake
 
wewe jamaa .... hivi ukiwa kama daktari halau mwizi akaletwa hospitalini ameumizwa vibaya je hautamtibu kwasababu ni mwizi ?
Uwezi kumtetea Marando kwenye ili suala la kuwatetea Mafisadi, kila unapojenga hoja zako naona unazidi kujivua nguo tu!
Kaa kimya kijana Leave well alone! You wont improve matters by going on tinkering, teh teh teh
 
Mm nikiwa ndo nilienzisha thread hii nimesoma maoni ya wengi na kugundua wachangiaji waliowengi hawafurahishwi na hili swala, japo kuna wachache bado wanaona ni sahihi kwa marando kuendelea na kuwatetea, Sasa basi hatuwezi kuishia kulaumu tu humu JF wakati chama tulichohangaika kukijenga hata km si kiasi kikubwa kinapotea kirahisi kwa vitu vinavyowezekana kurekebishika, Nimeamua naindike barua kwenda kwa katibu mkuu kumuelezea si tu watu hawafurahishwi na hili swala bali vuongozi wetu km wa kijiji, kata na tarafa hawawezi kuwajibu watu ni namna gani mjumbe wa kamati anawatetea mafisadi na kuwapinga, Draft ya hyo barua nitaiweka kesho then tutajadili kwa pamoja namna gani tuiboreshe. Kuna baadhi ya wana jf humu wanajifanya wao peke yao ndo wanaipenda chadema, km kweli mtu unakipenda chama basi uoneshe kukikosoa pale panapohitajika ni sio kushabikia vitu tu
 
LAT,
Mimi nalidhani wakili kazi yake ni kumtetea 'mtuhumiwa'!?
Hoja ya 2015 (ID ya member) sio kwamba ni tatizo kisheria kwa Marando kutetea watuhumiwa wa ufisadi lakini anaona inaweza kuleta mkanganyiko (hasa kwa watu wa kawaida, me and you excluded!) na kushindwa kutofautisha role ya marando kama wakili na hapohapo kama mwanasiasa/mwanaharakati/mwanachama wa chama kinachojipambanua kuwa against ufisadi. Mleta hoja anaona mkanganyiko huu unaweza kuiathiri CDM (au Marando kama mwanasiasa).
Binafsi pia hili linanipa shida (pamoja na kwamba sioni tatizo la kisheria). Kwa mfano masuala kama ya EPA/Kagoda, Meremeta na mengine yamekuwa yakipigiwa kelele na CDM mara kwa mara na kuishurutisha serikali kuchukuwa hatua (kuchunguza na kuwashitaki watuhumiwa) na kuna watu kadhaa ambao CDM (including Marando) imekuwa ikiwataja kwa majina (viz, List of Shame).
Sasa let say watuhumiwa hawa itokee wapelekwe mahakamani halafu Marando kama wakili achukue assignment ya kuwatetea....kwangu mimi kimantiki nitaona kuna tatizo (nitatilia shaka credibilty ya Marando kama wakili au kama mwanasiasa). Inawezekanje kwenye jukwaa la siasa umtaje/umtuhumu mtu kuwa fisadi halafu wewe huyohuyo uende mahakani kumtetea kwamba sio fisadi? Kama hili linawezekana, by implication nalo linakuwa ufisadi....ni kama vile unatoa shutuma za uongo juu ya mtu ili baadae upate kazi ya kumtetea!
Kama kweli tunaipenda CDM, nadhani ni vema tukawa wakweli na kuwashauri ipasavyo (hata kama itawauma) ili kama chama kizidi kuimarika. Wakati mwinge sio rahisi kwa wanasiasa kuona conflicting interests walizonazo. Hivyo pamoja na kuwa ni haki ya Marando kufanya afanyacho na pia ni haki ya watuhumiwa kupata fair representation kwenye vyombo vya kisheria, lakini bado anaweza kuchuja ili kuepuka/kupunguza conflict of interest.
Comrade SMU, Great Thinkers
 
  • Thanks
Reactions: SMU
2015 lazima nikupongeze kwa kutufundisha kitu hapa,malalamiko bila hatua ndio vinatuangamiza.bravo mkuu kwa kuchukua hatua mwenyewe!
 
2015 lazima nikupongeze kwa kutufundisha kitu hapa,malalamiko bila hatua ndio vinatuangamiza.bravo mkuu kwa kuchukua hatua mwenyewe!

Barua nitaiweka hapa muione kabla sijaipeleka, mm sina ugomvi na marando ila swala hili limeniumiza kwa muda mrefu yeye achane na hizo kesi aendelee na kesi za kawaida km hyo itamshinda basi atuachie chama, kitendo cha mtu kukipenda chama pekee ni swala zuri na kukipenda kwa kukijenga ni zuri zaidi, kwa ambae atataka tushirikiane ktk hili anicheki au anitumie mawazo yake mwanajamii33@yahoo.com
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sijui ni kwa nn wanajf tumekuwa wagumu kumuelewa mtoa hoja,na zaidi amejitahidi kuelewesha vizuri.Ni ukweli uliowazi kwamba tuliowengi humu ni ama mashabiki,wafuasi ama wapenzi wa CDM,hilo si tatizo hata kidogo.Shida niionayo ni pale fikra zetu,mawazo yetu na utashi wetu unapofungwa na mapenzi au ushabiki dhidi ya CDM.Tusipokuwa makini tutajikuta tunakizamisha chama wenyewe.Rai yangu kwa viongozi na wana CDM kwa ujumla jambo hili tusilifanyie ushabiki,tutafute njia nzuri ya kukiokoa chama juu ya hili.
 
wewe jamaa .... hivi ukiwa kama daktari halafu mwizi akaletwa hospitalini ameumizwa vibaya je hautamtibu kwasababu ni mwizi ?

Ni kweli, pia aelewe kuwa wale ni watuhumiwa si haki kuwabagua kwa utuhumiwa wao
hadi pale haki itakapojibainisha.
 
Barua nitaiweka hapa muione kabla sijaipeleka, mm sina ugomvi na marando ila swala hili limeniumiza kwa muda mrefu yeye achane na hizo kesi aendelee na kesi za kawaida km hyo itamshinda basi atuachie chama, kitendo cha mtu kukipenda chama pekee ni swala zuri na kukipenda kwa kukijenga ni zuri zaidi, kwa ambae atataka tushirikiane ktk hili anicheki au anitumie mawazo yake mwanajamii33@yahoo.com

Ni wazo zuri kabisa na niko tayari kuchangia mawazo yangu...na pia kuweka sahihi yangu kama mtanzania na siyo mwanachama. Kama ni ya wanachama tu, basi mie nitawapa mawazo yangu.

Lazima watu wajifunze kuchora mistari ili kutenganisha mapenzi yao na maslahi yao na madhara yake kwa maslahi ya umma. Katika hili Marando anahitaji kuvua magwanda ya CHADEMA au kukaa mbali na mafisadi.

Baada ya hapa itabidi tumwombe na naibu katibu mkuu ajibu tuhuma za Barrick Gold mines na misaada yao jimboni kwake!
 
Ni kweli, pia aelewe kuwa wale ni watuhumiwa si haki kuwabagua kwa utuhumiwa wao
hadi pale haki itakapojibainisha.

Hana haki ya kuwabagua watuhumiwa wowote ila kama mtu anayehubiri kila siku kwamba hapendi na anachukia ufisadi basi anatakiwa kuangalia aina ya watuhumiwa wa kuwatetea.. Hana moral authority ya kuongelea ufisadi kama anakaa kwenye bench la utetezi wa mafisadi!!

Ni hoja rahisi tu, naamini hata yeye Marando anaielewa...labda kama ni task kutoka kwa wakubwa wake wa TISS!!!!
 
Sijui ni kwa nn wanajf tumekuwa wagumu kumuelewa mtoa hoja,na zaidi amejitahidi kuelewesha vizuri.Ni ukweli uliowazi kwamba tuliowengi humu ni ama mashabiki,wafuasi ama wapenzi wa CDM,hilo si tatizo hata kidogo.Shida niionayo ni pale fikra zetu,mawazo yetu na utashi wetu unapofungwa na mapenzi au ushabiki dhidi ya CDM.Tusipokuwa makini tutajikuta tunakizamisha chama wenyewe.Rai yangu kwa viongozi na wana CDM kwa ujumla jambo hili tusilifanyie ushabiki,tutafute njia nzuri ya kukiokoa chama juu ya hili.

Kumbuka Marando ni wakili, anaongozwa na maadili ya uwakili na si itikadi za kichama,
anapaswa kumtetea yeyote hata kama mtu huyo kamuua mwanaye, kwani kwa kufanya
hivyo haki itabainika. Kuwa kada wa CDM hakumaanishi asisimame upande wa mtu fulani, kama
mna chuki zenu binafsi dhidi ya watu fulani hilo halihusiani na maadili ya uwakili wa Marando.
 
Hana haki ya kuwabagua watuhumiwa wowote ila kama mtu anayehubiri kila siku kwamba hapendi na anachukia ufisadi basi anatakiwa kuangalia aina ya watuhumiwa wa kuwatetea.. Hana moral authority ya kuongelea ufisadi kama anakaa kwenye bench la utetezi wa mafisadi!!

Ni hoja rahisi tu, naamini hata yeye Marando anaielewa...labda kama ni task kutoka kwa wakubwa wake wa TISS!!!!

Ni kweli lakini maadili ya uwakili yanasemaje? Tusipende kuhukumu pasipo kujua tunachokihukumu.
 
CDM wanastahili kujua kwamba ni wachache wanao weza kutofautisha hoja hizo mbili, magamba wataifanya hii kuwa ajenda yao na kipropaganda kwa wenzetu wenye uelewa mdogo wataikubali na kudharau injili mpya ambayo imeanza kupokelewa
 
Kumbuka Marando ni wakili, anaongozwa na maadili ya uwakili na si itikadi za kichama,
anapaswa kumtetea yeyote hata kama mtu huyo kamuua mwanaye, kwani kwa kufanya
hivyo haki itabainika. Kuwa kada wa CDM hakumaanishi asisimame upande wa mtu fulani, kama
mna chuki zenu binafsi dhidi ya watu fulani hilo halihusiani na maadili ya uwakili wa Marando.

Nakubaliana na wewe, lakini je ni wananchi wangapi wenye kulijua hili? kumbuka mpaka leo ccm mtaji wake mkubwa ni ujinga wa watz walio wengi, km hadi leo hawajaona madhara ya ccm unadhani ni lini watagundua marando anaongozwa na maadili ya uwakili? pia sisi km wanachama hatuweza kuwa busy kuhakikisha marando mmoja maadili yake ya uwakili hayaharibiki wakati huo huo chama chenye watu wengi ndo kiharibike,
Hii hoja ni vyema mkaitazama kwa undani kwa kuzingatia idadi kubwa ya uelewa mdogo waliyonayo wananchi wengi.
 
Back
Top Bottom