Marando na watuhumiwa wa ufisadi

Marando na watuhumiwa wa ufisadi

Role ya Marando ni kubwa sana hasa upande wa kotini kwa maslahi ya wapinzani wote nchini. Siku zote amekuwa akisema hakubaliani na aina ya watu wanaoletwa kotini kwa tuhuma za ufisadi kwakuwa ni dagaa tu, mapapa hayaletwi. Hivi karibuni aliulizwa swali hilo kwenye mdahalo na akina Nape akaeleza hivyo hivyo. Kwa maneno rahisi ni kuwa washitakiwa wa ufisadi wanabambikwa kesi. Fikiria kubambikwa kesi na machungu yake? Ulishawahi kufuatilia au hata kuiskia kesi ya Mahalu? Umeshaskia mashahidi wanaotakiwa Mahakamani kumtetea mshitakiwa? Dogo, TAFAKARI!

Kwa sasa anatetea vidagaa unataka kuniambia akipata nafasi ya kutetea visamaki ataacha? Pili km watuhumiwa wanababikiwa kesi unataka kutuambia Chadema wanawaongea watu?
 
Comrade Ngwendu, ni kweli kabisa hawa Pro-CDM-JF,uelewa wao ni mdogo sana kama huo mfano wa mgonjwa na Wakili.
Tatizo hawataki kujifunza na kukubali mawazo kutoka kwa watu wengine wao ni CDM tu mpaka imewapa upofu na akili zimedumaa kabisa tena zimefunikwa na blanketi jeusi,
hawa Pro-CDM-JF ni pumba sana mpaka wanatia huruma

JF Hate Preacher .... akili yako kama avatar zako

View attachment 36600

hivi ulifikiria uozo gani ukatumia hii avatar .... stigma
 
Kwa sasa anatetea vidagaa unataka kuniambia akipata nafasi ya kutetea visamaki ataacha? Pili km watuhumiwa wanababikiwa kesi unataka kutuambia Chadema wanawaongea watu?
Hujaeleweka, fafanua kidogo.
 
Hao walioshtakiwa ni watuhumiwa wadogowadogo ambapo kama hawatawakilishwa na wakili mzuri na anayesimamia haki (marandu) ccm watawabebesha mzigo wote hao watuhumiwa vidagaa huku wakiwaacha watuhumiwa halisi wakishirikiana kutafuna mapesa na viongozi wa ccm. TATIZO NI UELEWA WA WATANZANIA TULIO WENGI
 
Wale ni watuhumiwa bado hawajahukumiwa. Ana haki ya kuwatetea, kwani nao ni sehemu ya jamii ya Watanzania.

Kwa hiyo Leo Chadema wakiamua kwenda mahakamani kumshtaki ROSTAM kwa wizi wa kagoda uliochangia kikwete kuingia madarakani 2005 itakawa ni sawa mjumbe wa kamati kuu ya cdm MARANDO kumtetea rostam?
 
Hivi ndugu zangu,

Marando alishaacha kazi yake pale TISS???? Au majukumu yake CHADEMA ni sehemu ya kazi yake ya TISS!!!
 
Kwa hiyo Leo Chadema wakiamua kwenda mahakamani kumshtaki ROSTAM kwa wizi wa kagoda uliochangia kikwete kuingia madarakani 2005 itakawa ni sawa mjumbe wa kamati kuu ya cdm MARANDO kumtetea rostam?

Rostam ni fisadi papa hawez tetewa
 
huu ni ukweli mchungu kwetu wana cdm,Marando na kuwatetea mafisadi ni somo gumu sana kwa wananchi wa kawaida.dawa ya hili ni kuangalia namna ya kuliweka sawa hili na si kutetea tu kama vipofu,Tukumbuke Marando ni bosi cdm
 
...... kazi ya wakili ni kumtetea mhalifu na sio kuhukumu yupi ni mhalifu na yupi si mhalifu .... ......

LAT,

Mimi nalidhani wakili kazi yake ni kumtetea 'mtuhumiwa'!?

Hoja ya 2015 (ID ya member) sio kwamba ni tatizo kisheria kwa Marando kutetea watuhumiwa wa ufisadi lakini anaona inaweza kuleta mkanganyiko (hasa kwa watu wa kawaida, me and you excluded!) na kushindwa kutofautisha role ya marando kama wakili na hapohapo kama mwanasiasa/mwanaharakati/mwanachama wa chama kinachojipambanua kuwa against ufisadi. Mleta hoja anaona mkanganyiko huu unaweza kuiathiri CDM (au Marando kama mwanasiasa).

Binafsi pia hili linanipa shida (pamoja na kwamba sioni tatizo la kisheria). Kwa mfano masuala kama ya EPA/Kagoda, Meremeta na mengine yamekuwa yakipigiwa kelele na CDM mara kwa mara na kuishurutisha serikali kuchukuwa hatua (kuchunguza na kuwashitaki watuhumiwa) na kuna watu kadhaa ambao CDM (including Marando) imekuwa ikiwataja kwa majina (viz, List of Shame).

Sasa let say watuhumiwa hawa itokee wapelekwe mahakamani halafu Marando kama wakili achukue assignment ya kuwatetea....kwangu mimi kimantiki nitaona kuna tatizo (nitatilia shaka credibilty ya Marando kama wakili au kama mwanasiasa). Inawezekanje kwenye jukwaa la siasa umtaje/umtuhumu mtu kuwa fisadi halafu wewe huyohuyo uende mahakani kumtetea kwamba sio fisadi? Kama hili linawezekana, by implication nalo linakuwa ufisadi....ni kama vile unatoa shutuma za uongo juu ya mtu ili baadae upate kazi ya kumtetea!

Kama kweli tunaipenda CDM, nadhani ni vema tukawa wakweli na kuwashauri ipasavyo (hata kama itawauma) ili kama chama kizidi kuimarika. Wakati mwinge sio rahisi kwa wanasiasa kuona conflicting interests walizonazo. Hivyo pamoja na kuwa ni haki ya Marando kufanya afanyacho na pia ni haki ya watuhumiwa kupata fair representation kwenye vyombo vya kisheria, lakini bado anaweza kuchuja ili kuepuka/kupunguza conflict of interest.
 
Wana JF

Kwanza na-declare interest mm ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA, Hili swala la Marando kuwa wakili wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi km vile manji na mahalu litakuja kuwa na madhara makubwa sana hapo badae ktk harakati za chama za kuchua dola natambua kabisa ile ni professional yake na ni vigumu aache kazi aliyoisomea kwa muda mrefu, lakini kabla ya kuchua kazi lazima mtu ufanya client assessment.

Kwa kuwa ameamua kuwa ktk siasa na kufanikiwa kuwa mjumbe wa cc ya cdm ni wakati wake muafaka wa kuhakikisha kimoja kati ya professional yake na siasa hakuna kinacholeta madhara kwa kingine. Kwa hiyo moja ya criteria ya kutumika kwake kum-accept client iwe ni asiwe mtuhumiwa wa ufisadi. Nionavyo mm professional yake kwa sasa inaleta madhara ktk siasa si kwake tu bali kwa Chadema kwa ujumla coz ni vigumu sana mtu kupinga ufisadi majukwaani na kuukubali mahakamani na watu wote wakaamua kukuamini ww ni mpiganaji wa kweli wa ufisadi.

Swala kubwa la sisi wana-chadema tunalotakiwa kulielewa ni kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawawezi kutofautisha professional na siasa kiasi kwamba point tutakayoitumia kuuelezea uma ya kuwa hii ni siasa na hii ni professional haitaweza kuzaa matunda yeyote. Marando na uongozi wa juu ulitazame hili kwa mapana na marefu ili nguvu iliyokwisha tumika kukifikisha chama hapa isije kupotea kirahisi kisa mtu mmoja ambae ana uwezo wa kuchua kesi zingine na kuendelea na maisha.

Tujiulize swali dogo kwa mfano leo ROSTAM amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa KAGODA na marando akafanya km anavyofanya kwa wale wa EPA itakuwa sahihi? Au kuwatetea wa EPA itakuwa halali na kumtetea Rostam itakuwa haramu wakati wote ni mafisadi?

Nawasilisha
Abracadabra!
 
LAT,
Mimi nalidhani wakili kazi yake ni kumtetea 'mtuhumiwa'!?

Hoja ya 2015 (ID ya member) sio kwamba ni tatizo kisheria kwa Marando kutetea watuhumiwa wa ufisadi lakini anaona inaweza kuleta mkanganyiko (hasa kwa watu wa kawaida, me and you excluded!) na kushindwa kutofautisha role ya marando kama wakili na hapohapo kama mwanasiasa/mwanaharakati/mwanachama wa chama kinachojipambanua kuwa against ufisadi. Mleta hoja anaona mkanganyiko huu unaweza kuiathiri CDM (au Marando kama mwanasiasa).

Binafsi pia hili linanipa shida (pamoja na kwamba sioni tatizo la kisheria). Kwa mfano masuala kama ya EPA/Kagoda, Meremeta na mengine yamekuwa yakipigiwa kelele na CDM mara kwa mara na kuishurutisha serikali kuchukuwa hatua (kuchunguza na kuwashitaki watuhumiwa) na kuna watu kadhaa ambao CDM (including Marando) imekuwa ikiwataja kwa majina (viz, List of Shame).

Sasa let say watuhumiwa hawa itokee wapelekwe mahakamani halafu Marando kama wakili achukue assignment ya kuwatetea....kwangu mimi kimantiki nitaona kuna tatizo (nitatilia shaka credibilty ya Marando kama wakili au kama mwanasiasa). Inawezekanje kwenye jukwaa la siasa umtaje/umtuhumu mtu kuwa fisadi halafu wewe huyohuyo uende mahakani kumtetea kwamba sio fisadi? Kama hili linawezekana, by implication nalo linakuwa ufisadi....ni kama vile unatoa shutuma za uongo juu ya mtu ili baadae upate kazi ya kumtetea!

Kama kweli tunaipenda CDM, nadhani ni vema tukawa wakweli na kuwashauri ipasavyo (hata kama itawauma) ili kama chama kizidi kuimarika. Wakati mwinge sio rahisi kwa wanasiasa kuona conflicting interests walizonazo. Hivyo pamoja na kuwa ni haki ya Marando kufanya afanyacho na pia ni haki ya watuhumiwa kupara fair representation kwenye vyombo vya kisheria, lakini bado anaweza kuchuja ili kuepuka/kupunguza conflict of interest.

mkuu ... i stand to be corrected ' ..... i meant "watuhumiwa"

mind you ... marando anapractice proessional carrier yake legally ..... yes tunatambua shutuma za ufisadi .... je hakuna uwezekano kwamba marando is after his daily bread as an attorney? kwani kuwatetea ni subject lazima washinde ...
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Uwe unasoma na kuelewa na sio kupost tu, nimesema naelewa anachokifanya marando ni kazi yake kwa kuwa ni mwanasheria lakini nikatahadharisha ya kuwa ameshachanganya na siasa na vilevile si wananchi wengi wenye uwezo wa kutenganisha hivi vitu viwili, Kuna umuhimu gani wa kuanza kuwaelewesha watu eti ile ni professional yake acha awatete na tusitumie huo muda kueneza zaidi somo hili la ufisadi kwa watz coz sio watz wote wameshaelewa madhara mazima ya ufisadi

Unayosema mkuu ni ukweli mtupu lazima atenganishe Hayo mambo kama maslahi ya chama au kutetea hao anaowatetea
 
marando yupo kazini bt serikali inatakiwa ipeleke wanasheria wazuri kuproval kama kweli watuhumiwa ni waarifu kweli ili washindane na wakina marando tatizo serikali inapeleka wanasheria weupe katika sheria ushahidi hautoshi na nk,

but ili swala la marando tunanatakiwa tuliangalie kwa jicho la tatu mfano hivi marando akipewa pesa na watuhumiwa wa ufisadi then akaenda kutoa ile pesa kuchangia chama hapo si tutakuwa tumepokea pesa ya mafisadi wakati sisi cdm tunapinga ufisadi?

kwa sababu katika hali ya kawaidi hailete picha nzuri dr slaa ameibua tuhuma za ufisadi kwa bwana jitu pater then marando anadai jitu hana hatia.

tufikie wakati tuwe wanachama wa tanzania na sio wanachama wa vyama vya siasa katika kupigania matakwa ya tanzania
 
LAT,

Mimi nalidhani wakili kazi yake ni kumtetea 'mtuhumiwa'!?

Hoja ya 2015 (ID ya member) sio kwamba ni tatizo kisheria kwa Marando kutetea watuhumiwa wa ufisadi lakini anaona inaweza kuleta mkanganyiko (hasa kwa watu wa kawaida, me and you excluded!) na kushindwa kutofautisha role ya marando kama wakili na hapohapo kama mwanasiasa/mwanaharakati/mwanachama wa chama kinachojipambanua kuwa against ufisadi. Mleta hoja anaona mkanganyiko huu unaweza kuiathiri CDM (au Marando kama mwanasiasa).

Binafsi pia hili linanipa shida (pamoja na kwamba sioni tatizo la kisheria). Kwa mfano masuala kama ya EPA/Kagoda, Meremeta na mengine yamekuwa yakipigiwa kelele na CDM mara kwa mara na kuishurutisha serikali kuchukuwa hatua (kuchunguza na kuwashitaki watuhumiwa) na kuna watu kadhaa ambao CDM (including Marando) imekuwa ikiwataja kwa majina (viz, List of Shame).

Sasa let say watuhumiwa hawa itokee wapelekwe mahakamani halafu Marando kama wakili achukue assignment ya kuwatetea....kwangu mimi kimantiki nitaona kuna tatizo (nitatilia shaka credibilty ya Marando kama wakili au kama mwanasiasa). Inawezekanje kwenye jukwaa la siasa umtaje/umtuhumu mtu kuwa fisadi halafu wewe huyohuyo uende mahakani kumtetea kwamba sio fisadi? Kama hili linawezekana, by implication nalo linakuwa ufisadi....ni kama vile unatoa shutuma za uongo juu ya mtu ili baadae upate kazi ya kumtetea!

Kama kweli tunaipenda CDM, nadhani ni vema tukawa wakweli na kuwashauri ipasavyo (hata kama itawauma) ili kama chama kizidi kuimarika. Wakati mwinge sio rahisi kwa wanasiasa kuona conflicting interests walizonazo. Hivyo pamoja na kuwa ni haki ya Marando kufanya afanyacho na pia ni haki ya watuhumiwa kupata fair representation kwenye vyombo vya kisheria, lakini bado anaweza kuchuja ili kuepuka/kupunguza conflict of interest.

Kweli kabisa mkuu,

Labda kama Marando anafanya assignment nyingine ambayo watu wengi hatuwezi kuiona kwa macho ya kawaida!!
 
Marando bado yuko serikalini nyie anazuga tu profesheni yake hakuna kustaafu ye na mtikila damu damu!
 
....mind you ... marando anapractice proessional carrier yake legally ..... yes tunatambua shutuma za ufisadi .... je hakuna uwezekano kwamba marando is after his daily bread as an attorney? kwani kuwatetea ni subject lazima washinde ...

Ndio hapa suala la conflicting interest linapokuja. Sasa kama anawatetea bila kujali kama wanashinda (kupata haki) ama la ilimuradi mkono umeenda kinywani bado atafaa kuitwa wakili? Haki ya mtuhumiwa tunaiweka wapi?
 
Sijui kwa nini watu hawaoni tatizo kaka role hii ya Marando,

Hata kama unatafuta mkate wako wa kila siku, ni halali kuutafuta nyumbani kwa shetani....na especially kama wewe ni mhubiri unayeshinda majukwaani ukimchana chana huyo shetani???
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mleta mada hajui anachosema kabisaaa kwani akiwa mwanasheria si ni kazi yake kutetea watu au umehujui kazi yake pole badilisha mada kwani umechemka.

Chadema ni chama makini hakitaki kwenda Ikulu kwa kupigiwa kura na watu wasioelewa nini wanafanya kama ilivyozoea CCM. Kama mpiga kura hajui kutofautisha kati ya Kazi za chadema kama chama cha siasa na kazi za kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Marando basi wapiga kura bado hawajaelimika.

Marando kama mwananchi mwema anapinga ufisadi kwasababu hapendi watu fulani kuonewa kwa rasilimali zao kuliwa na watu wachache kwa njia za wizi.

Pia Marando kama Mwanasheria (professional) atakuwa wa ajabu kama atakataa kumsimamia mtu katika kesi ili atendewe haki. Sidhani kama Chadema ikiingia madarakani itafanya kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi na kuwasweka jela kwa vifungo bila kuwapa nafasi ya kujitetea na kufanya haki itendeke.
 
Back
Top Bottom