Marafiki wanaoishi DAR... Sio kabisa

Wana JF ... hili limekaa vipi?.. Mie nimetoka Mkoani nimekuja Jijini(DAR).. kwa Mapumziko kidogo, kusalimia ndugu na marafiki zangu....
sasa jamani ugumu nimeukuta ktk ishu moja... Rafiki zangu wa Ukweli,,nimesoma nao kabisa,,,tumeishi pamoja chuoni... tumekula bata(kujirusha) pamoja wakati nipo nao chuo...!!! Maajabu nimewatafuta niwaone wamekua watu wa ma promise yasiyokua na fulfilment... Sasa mie nikajiuliza hawa vijana wanaoishi dar... wanatuchukulia vipi sie tunaotoka Mkoa... wanadhani ua tunakuja lia NJAA..kwao auuu??? Acheni ujinga bana, tunakuja na hela zetu za mavuuno ...!!!

Sisi tumefunzwa ukarimu, nakupa majina ya wafuatao ukifika dar uje tukupe raha za duniani, LAT, KakaKiiza, The Finest, Mwenzetu, Jrated, LD, Husninyo, Newmzalendo, Babalao, Manundu, Carmel etc.

Hao madenti wenzako ni masharobaro, wanahisi unanuka vumbi la mkoa si unajua tena! lol

Hee! yaani hutaki hata zawadi za nsansa,matobolwa,ntwili na mihogo..
Watu tunamitikasi yetu tuhangaike na Data wanini?? Usitupotezee wakati wewe watujua???

HA ha haa ha ha mweeeeeeeeeeee kalale na kesho uende zako

Pole sana, hao marafiki zako ndio washamba, mie marafiki zangu wa mkoa wakitua dar ni juu kwa juu, hoteli wanalipia lakini hawakai kabisa ,maana ni kufurahi kwa kwenda mbele

Sisi tumefunzwa ukarimu, nakupa majina ya wafuatao ukifika dar uje tukupe raha za duniani, LAT, KakaKiiza, The Finest, Mwenzetu, Jrated, LD, *Husninyo*, Newmzalendo, Babalao, Manundu, Carmel etc.

heee! kwani husninyo yupo dar?

afu hii kweli, nafikiri maisha pia yanachangia.ila wa mikoani bado wakarimu sana,ukienda mtu anatoa muda wake wote ufurahi kipindi chote.

Hee! yaani hutaki hata zawadi za nsansa,matobolwa,ntwili na mihogo..

aafu ngoja nnikueleze kitu.. mtu wa ukimwambia .. yani ukimpa taarifa kwamba nataka kuja Dar... anakuagiza mambo ya kijingajinga meengiiiii.... mara Unga wa ugali, .... mafuta ya kupikiaa, .... etc... sasa mie ua najiuliza hawa viumbe vipiii!!!?? Ivi Dar hamna mafuta ya kupikia? hamna unga wa Ugali.. Waache Upuuzii.

May b ni swala la muda jijini mambo mengi mkubwa

Mambo mengi yapi Mkuu.... na hawa jamaa wakija mkoa wala hawatoi taarifa.. unashangaa tu mtu anagonga mlango wa Ghetto...!!!!!!!!! Wanajifanya waheshimiwa hiiviii!!!!!!!! kumbe njaa tu.

aafu ngoja nnikueleze kitu.. mtu wa ukimwambia .. yani ukimpa taarifa kwamba nataka kuja Dar... anakuagiza mambo ya kijingajinga meengiiiii.... mara Unga wa ugali, .... mafuta ya kupikiaa, .... etc... sasa mie ua najiuliza hawa viumbe vipiii!!!?? Ivi Dar hamna mafuta ya kupikia? hamna unga wa Ugali.. Waache Upuuzii.
he he....halahala data....tafadhali kama unatokea kigoma kuja Yaeda....chonde chonde baba.....dagaa na mawese ndio mpango mzima....ukinyunyizia na kitenge cha wax

Bro. mimi nipo Dar na support kweli marafiki wa Dar siyo hata mimi marafiki zangu baada ya miaka fulani niliona wanabadilika na kujifanya wako busy for nothing na ukukitana nao watajifanya wao dili zao ni maongezi ya pesa kama huna kampuni wanakuona wewe ufai lakini ukuwaangalia nao hawana dili zozote za maana ni full frastration tu sijui kwa sababu ya foleni au utandawazi wenyewe

he he....halahala data....tafadhali kama unatokea kigoma kuja Yaeda....chonde chonde baba.....dagaa na mawese ndio mpango mzima....ukinyunyizia na kitenge cha wax

sio ishu kabisa... kwa taarifa yao watu wa Dar.. maisha magumu kotekote.

Wana JF ... hili limekaa vipi?.. Mie nimetoka Mkoani nimekuja Jijini(DAR).. kwa Mapumziko kidogo, kusalimia ndugu na marafiki zangu.... sasa jamani ugumu nimeukuta ktk ishu moja... Rafiki zangu wa Ukweli,,nimesoma nao kabisa,,,tumeishi pamoja chuoni... tumekula bata(kujirusha) pamoja wakati nipo nao chuo...!!! Maajabu nimewatafuta niwaone wamekua watu wa ma promise yasiyokua na fulfilment... Sasa mie nikajiuliza hawa vijana wanaoishi dar... wanatuchukulia vipi sie tunaotoka Mkoa... wanadhani ua tunakuja lia NJAA..kwao auuu??? Acheni ujinga bana, tunakuja na hela zetu za mavuuno ...!!!
Mbona unalaumu sana ? hujui wana hali gani,sasa kama umekuja na hela yako nzuri tatizo nini ? chukua chumba self-contained full a/c mitaa ya Sinza,piga laga zako,ukijiskia vuta kifaa na ukifika muda ondoka 'kimya kimya' ndio Darisalama hii au ulikuja na hela mbuzi ukitegemea wenyeji wakupokee Ubungo ?

sikuja omba hifadhi kwao ..wote wamepanga.. sometimes hata walojenga ua wanadai wamepokea wageni ..."recently''...wakimaanisha ndugu zao..

sikuja omba hifadhi kwao ..wote wamepanga.. sometimes hata walojenga ua wanadai wamepokea wageni..."recently''
...wakimaanisha ndugu zao..
ukiona wote wanakukwepa hivyo TATIZO liko kwako mkuu na unavyolalamika hapa inadhihirisha hilo, ukija tena wasalimie kwenye simu tu chukua chumba,usiku nenda club ukacheze kwaito,pata urithi wetu,ukipendezwa na kizazi hiki cha Carolight jipongeze na mmoja mchezo kwisha jumapili wahi ubungo.

Similar Discussions

Back
Top Bottom